KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, January 21, 2010

Al Faisal akosa kufikishwa mahakamani Kenya


Al Faisal akosa kufikishwa mahakamani Kenya

Serikali ya Kenya imekosa kutii amri ya mahakama ya kumwasilisha mhubiri wa kiislamu kutoka Jamaica Shaikh Adulla Al Faisal mahakamani.
Mahakama kuu mjini Nairobi ilikuwa imemuagiza waziri wa uhamiaji kumwasilisha Sheikh Al Faisal baada ya Shirika la kutetea haki za jamii ya waislamu nchini Kenya, kwasilisha kesi mahakamani ya kutaka muhubiri huyo aachiliwe iwapo serikali imeshindwa kumrudisha Jamaica. Kesi hiyo itasikilizwa baadaye aleo alasiri.Huku hayo yakijiri shirika hilo la kutetea haki za jamii ya waislamu imekanusha madai kuwa imepanga maandamano mengine hapo kesho katika miji mikuu nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment