KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Vyanzo vya maji vyachafuliwa Sudan


Shirika la kutoa misaada la Ujerumani limeushutumu muungano wa kampuni za mafuta kusini mwa Sudan kwa kuvichafua vyanzo vya maji vinavyotumiwa na watu wasiopungua laki tatu.
Shirika hilo, Sign of Hope, linasema lilipima visima viwili vilivyo karibu na maeneo mawili makuu ya mafuta-Mala na Thar Jath-baada ya wakaazi kulalamika kwamba maji hayo yaliwadhuru kiafya.

Shirika hilo linasema lilikuta madini yanayohatarisha maisha ya watu ndani ya maji na limeikabidhi taarifa hiyo kwa Serikali ya Sudan na kampuni ya the White Nile Petroleum.

Kampuni hiyo imesema kulinda ubora wa maji ni jambo walilolipa kipaumbele na imejenga kiwanda cha kuyasafisha maji kwa wakaazi wa eneo hilo

No comments:

Post a Comment