KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Amnesty yashutumu mauaji Msumbiji


Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeshtumu polisi wa Msumbiji kwa kufanya mauaji kinyume cha sheria.
Shirika hilo limesema kuwa takriban watu 46 wameangamia mikononi mwa polisi tangu mwaka 2006.

Shirika hilo linasema mauaji mengi hayakuchunguzwa na kuwa mara nyingi maafisa wa polisi hawashitakiwi.

Msemaji wa polisi nchini Msumbiji ameeleza kuwa ripoti hiyo ya shirika la Amnesty International, iliegemea upande mmoja.

Amesema kuwa maafisa wa polisi waliofanya mauaji kinyume cha sheria walishtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka ishirini.

No comments:

Post a Comment