KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, November 13, 2009

Uganda kuchunguza kifo cha Jenerali Kazini


Uganda kuchunguza kifo cha Jenerali Kazini

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ameamuru uchunguzi kufuatia kifo cha mkuu wa zamani wa jeshi James Kazini aliyeuawa siku ya Jumanne.
Mpenzi wa meja Jenerali Kazini amekiri kumuua afisaa huyo wa zamani wa jeshi kwa kumgonga na chuma kichwani siku ya jumanne katika mauaji yaliwashtua wengi.

Kwa mujibu wa duru, kuna wasiwasi kuwa mauaji hayio hayakutokea kwa sabau ya tofauti nyumbani bali ilikuwa njama iliyoangwa kumuua Kazini.

Marehemu Jenerali Kazini aliachishwa kazi mwaka 2003 baada ya tuhuma za umoja wa mataifa kuwa alipora mali asili katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, wakati akisimamia operesheni za kijeshi.

mwaka jana pia alipatikana na hatia ya kuliletea hasara kubwa jeshi.

No comments:

Post a Comment