KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Nigeria yaingia nusu fainali U17


Wenyeji Nigeria walifuzu kuingia nusu fainali ya michuano ya kugombea kombe la dunia kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17 baada kuitandika Korea Kusini huko Calabar.
Ramon Azeez aliwapatia Nigeria goli la kwanza kunako dakika ya 23, hata hivyo dakika tano kabla ya mapumzik, Son Hueng Min alipata goli la kusawazisha.

Abdul Ajagun aliongeza la pili kwa Nigeria dakika ya 50 na Terry Envoh alikamilisha ushindi kwa kutikisa goli la tatu ilipotimia dakika ya 85.

Nigeria, ambao ni mabingwa watetezi sasa watachapana na Hispania katika nusu fainali siku ya Alhamisi.

No comments:

Post a Comment