KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 2, 2009

Sudan ya kusini yasisitiza kujitenga


Kiongozi wa jimbo la kusini mwa Sudan Salva Kiir ametetea nia yake ya kutaka uhuru kamili hatma ya jimbo hilo itakapoamuliwa kwa kura ya maoni mnamo mwaka 2011.
Amesema kua kupiga kura ya kutaka muungano na Sudan ya kaskazini daima kutawafanya raia wa kusini kuwa raia wa hadhi ya pili nyumbani kwao.

Upigaji kura ya maoni kwa jimbo hili lenye utajiri wa mafuta ni sehemu ya mpango wa maafikiano wa mwaka 2005 uliomaliza miaka mingi ya vita vya wenyewe.



Hapo awali viongozi wamekuwa wakifanya tahadhari ya kuzungumza kuhusu umoja baina ya kaskazini na kusini, kama inavyohitajika chini ya muafaka wa amani.

Akizungumza kwenye sala maalum zilizofanyika kuomba amani, Bw.Kiir aliwataka raia wafanye chaguo lao binafsi. Aliongezea kusema kuwa unachagua kwa ajili ya amani, lakini kufanya hivyo unajikuta ukiwa raia wa hadhi ya pili, ni chaguo lako.

No comments:

Post a Comment