KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

Rais Barack Obama wa Marekani amesifu na kutaja uwamuzi juu ya mswada wa sheria ya afya


Rais Barack Obama wa Marekani amesifu na kutaja uwamuzi juu ya mswada wa sheria ya afya kama wa Kihistoria. Aliongezea kusema kuwa ana imani kwamba baraza la senate litaupitisha mpango huo na kwamba utaidhinishwa kuwa sheria kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Mswada ulipitishwa kwa kura chache na bunge ikiwa ni 220 kwa 215. Mswada huo unakusudia kueneza huduma ya afya kwa raia wengine milioni 36 wa Marekani.

Bwana Obama amefanya mageuzi katika huduma ya afya kuwa kiini cha utawala wake katika masuala ya nchini. Wanachama wa chama tawala cha Democratic inawabidi watafakari mswada wao ili waweze kufanikiwa utakapofikishwa katika Senate ambako wanahitaji kura 60 kati ya 100 kufanikisha mswaada huo kuwa sheria.


Katika baraza la Senate kuna wawakilishi 57 wa chama cha Democratic pamoja na wawili wasioegemea upande wowote. Wawakilishi wawili wa chama cha upinzani cha Republican wamesema kuwa wataunga mkono mswaada unaokubalika na wote.Endapo utaidhinishwa wanasheria kutoka pande zote za baraza watajaribu kusawazisha mapendekezo kutoka pande hizo kabla ya mpango mzima kutiwa sahihi na kuidhinishwa kuwa sheria na Rais Obama.

No comments:

Post a Comment