KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 4, 2009

Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Cheki imetupilia mbali pingamizi dhidi ya mkataba wa Lisbon wa Muungano wa Ulaya


Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Cheki imetupilia mbali pingamizi dhidi ya mkataba wa Lisbon wa Muungano wa Ulaya na kukataa madai kwamba mkataba huo utaunda taifa moja kuibwa la Ulaya na kwa hiyo kuvuruga mamlaka ya Cheki..

Mkataba wa Lisbon ambao unaweka marekebisho kadhaa ya kimsingi sasa unahitaji kutiwa saini tu na Rais wa nchi hiyo Vaclav Klaus .

Hivi sasa bara la Ulaya linakaribia kutekeleza mradi mkubwa uliochukua miaka minane kuutayarisha na ambao umeshuhudia vizingiti na vikwazo kadhaa.

Kilichosalia ni saini ya Rais Vaclav Klaus, kiongozi pekee aliyeelezea upinzani dhidi ya muungano wa Ulaya ambaye aliupiga vita vikali mkataba wa Lisbon lakini sasa inaelekea yuko tayari kusalimu amri..

No comments:

Post a Comment