KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 9, 2009

China kuikopesha Afrika dola billioni 10


Waziri Mkuu wa Uchina
Uchina inapanga kuzidisha misaada, uwekezaji na biashara na mataifa ya Afrika, licha ya athari za msukosuko wa kiuchumi duniani.
Akizungumza kabla ya mkutano wa viongozi wa Afrika na Uchina, unao-anza leo nchini Misri, Waziri Mkuu wa Uchina, Wen Jaibao, alisema, nchi yake ina azma ya kuisaidia Afrika kwa moyo mkunjufu, kwa dhati, na bila masharti au maslahi ya kisiasa.

Kuna fursa kubwa sasa katika bara la Afrika. Wakati mabenki ya kigeni yanaondoka na kurejea katika masoko yao ya nyumbani, nchi zinazoendelea zinatafuta rasilamli kwa haraka, ili kugharimia ujenzi wa miundo mbinu. Hiyo ni fursa nzuri sana kwa Uchina, ambayo inatafuta nafasi ya kutumia akiba kubwa iliyonayo.

Biashara ya Uchina Afrika imeongezeka mara kumi katika miaka minane iliyopita. Kutoka Afrika, Uchina inataka madini, mafuta na gesi nyingi ilioko katika bara hilo, ili kuendesha uchumi wa Uchina unaokuwa kwa haraka.

No comments:

Post a Comment