KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 18, 2009

Arsenal yasubiri majibu ya kuumia Gibbs


Kieran Gibbs anasubiri majibu ya vipimo vya X-ray baada ya kuumia alipoichezea England dhidi ya Lithuania chini ya umri wa miaka 21.
Mlinzi huyo wa kushoto wa Arsenal aliumia kiwiko cha mguu wa kuume na kulazimika kutolewa nje dakika ya 21 England walipocheza kuwania kufuzu ubingwa wa Ulaya kwa vijana walio na umri wa miaka chini ya 21 huko Vilnius.

Siku ya Jumatano alifanyiwa uchunguzi na daktari wa Arsenal.

Gibbs, mwenye umri wa miaka 20, amekuwa akicheza badala ya Gael Clichy aliyeumia mgongo katika nafasi ya ulinzi wa kushoto.

Msemaji wa chama cha soka cha England ameiambia BBC haionekani kama Gobbs ameumia vibaya kiwiko cha mguu.

Lakini iwapo Gibbs mzaliwa wa Lambeth atalazimika kukaa nje ya uwanja kutokana na tatizo hilo, inaweza kumpa matatizo makubwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kwa upande wa ulinzi.

No comments:

Post a Comment