KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 20, 2009

Wenger aondoa hofu kwa Walcott


Wenger aondoa hofu kwa Walcott

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amepinga mawazo kuumia kwa Theo Walcott ni suala linaloelekea kuzoeleka baada ya kufahamika atakuwa nje kwa wiki nne.
Walcott aliyekosa michezo ya awali msimu huu kutokana na maumivu ya mgongo, katika mchezo wa Jumamosi ilibidi atolewe nje baada ya kucheza kwa dakika 33 kutokana na kuumia goti.

Walcott pia katika msimu uliopita alikuwa nje kutokana na kuumia, lakini hata hivyo Wenger amepuuza mashaka hayo.

Wenger amesema"Yeye bado ni kijana mdogo na katika baadhi ya nyakati kwa umri wake lazima apitie kipindi kama hicho".

Walcott alirejea kuchezea klabu yake msimu huu akiwa mchezaji wa akiba Arsenal ilipocheza na Blackburn tarehe 4 Octoba na akaichezea England chini ya miaka 21 walipoilaza Macedonia mabao 6-3.

No comments:

Post a Comment