KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 16, 2009

rais jakaya kikwete ndani ya musoma


rais jakaya kikwete ndani ya musoma leo
Mama Maria Nyerere akimkaribisha JK muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Musoma jioni hii.

JK yupo mkoani Mara kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo pamoja na shughuli nyingine atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge siku ya Jumatano ambayo pia itakuwa ni kuadhimisha siku ya Nyerere.Mwanafunzi Godbless Buluhya wa shule mpya ya sekondari ya Chifu Oswald Man’gombe iliyopo musoma vijijini akifanya jaribio la kisayansi wakati JK alipokagua maabara ya shule hiyo jana jioni.Wengine katika kutoka kushoto ni Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mstaafu Enos Mfuru(wapili kushoto) na wanne kulia ni Mbunge wa Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono.

No comments:

Post a Comment