KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 20, 2009

Niger kuchagua bunge jipya
Rais Mamadou Tandja kusalia madarakani
Raia wa Niger wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa kwanza wa ubunge tangu rais Mamadou Tandja kulazimisha mageuzi ili kuendelea kusalia madarakani, mapema mwaka huu.
Kiongozi huyo amekosolewa kwa kulazimisha katiba yake ambapo atawania urais kwa mhula wa tatu.

Pia amelalamikiwa kwa kuvunja bunge la awali, mahakama ya juu na kutangaza utawala bila kufuata utaratibu wa sheria.

Upande wa upinzani PNDS umetaka wapiga kura kususia shughuli ya leo.Chama hicho kimesema ikiwa raia watapiga kura ya leo itakuwa kumpa idhini isiyo halali bw. Tandja.

No comments:

Post a Comment