KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 20, 2009

7 wathibitishwa kufa Kenya


7 wathibitishwa kufa Kenya

Watu 7 wamethibitishwa kufa katika ajali ya kuanguka kwa jengo, mjini Kiambu, nje kidogo ya jiji la Nairobi, nchini Kenya.
Kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu, kazi ya uokozi imekuwa ngumu kutokana na kutokuwepo na orodha ya watu waliokuwa wakifanya kazi katika jengo hilo.

Shirika hilo linasema zaidi ya watu kumi bado wamenaswa katika mabaki ya jengo hilo.

Shutuma zimeelekezwa kwa mmiliki wa jengo hilo, kuwa hakufuata kanuni za ujenzi.

Polisi inamtafuta mmiliki wa jengo hilo.

No comments:

Post a Comment