KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 27, 2009

Mazungumzo Zimbabwe yaisha bila 'muafaka'


Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amemaliza mazungumzo juu ya ugawanaji madaraka na rais Robert Mugabe, bila ya kufikia makubaliano yoyote.
Mkutano huo uliodumu kwa saa 4, umewakutanisha kwa mara ya kwanza waziri mkuu wa rais, tangu bw Tsvangirai ajitoe kutoka katika serikali ya muungano Oktoba 16.

Msemaji wa bw Tsvangirai amesema viongozi hao wawili wameonekana kutofautiana katika masuala mengi.

Bw Tsvangirai alijiondoa kutoka katika serikali ya muungano kutokana na mvutano wa kisiasa na pia kwa sababu ya mashitaka dhidi ya afisa wa ngazi ya juu wa chama cha MDC.

No comments:

Post a Comment