KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 14, 2009

Majeruhi wa risasi wapata ahueni Nigeria


Nigeria imeondoa sheria iliyolazimisha hospitali kutotoa huduma za dharura kwa watu wanaoshambuliwa kwa kupigwa risasi mpaka kupokea ripoti ya polisi.
Maafisa walibatilisha sheria hiyo iliyokuwepo tangu miaka ya 80 kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu waliofariki dunia kwa majeraha ya risasi.

Sheria hiyo imeondoshwa baada ya mhariri wa gazeti moja, Bayo Ohu alipofariki dunia kutokana na majeraha ya risasi baada ya hospitali kusubiri ripoti ya polisi badala ya kumtibu.

Nigeria ina matukio mengi ya uhalifu unaohusu matumizi ya bunduki ikiwemo utekaji nyara na ujambazi

No comments:

Post a Comment