KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 30, 2009

Afungwa kwa kuwasaidia magaidi


Mahakama moja nchini Marekani, imetoa hukumu ya kumfunga miaka minane mtu mmoja, kwa kuwasaidia magaidi.
Wakati wa kesi hiyo huko Ilinois, Ali al-Marri alikiri kuwasiliana na Khaled Sheikh Mohamed, mtu aliyehusika kupanga mashambulio ya Septemba kumi na moja.

Bw al-Marri, ambaye ni raia wa Saudi na vile vile Qatar, alikiri kuhudhuria kambi za mazoezi za Al Qaeda, kabla ya kukamatwa kwake mwaka 2001.

Kulikuwa na uwezekano wa Al-Marri kufungwa jela miaka 15.

Lakini badala yake, alikabidhiwa hukumu ya miaka minane jela, na huenda akaachiliwa chini ya miaka sita, ikiwa atakuwa na tabia nzuri.

No comments:

Post a Comment