KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 29, 2009

Wanajeshi Guinea wazidiwa na wananchi
Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Kapteni Moussa Dadis Camara amekiri baadhi ya wanajeshi nchini humo wameshindwa kujidhibiti wakati wa kukabiliana na ghasia za wapinzani katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Katika mahojiano na radio ya Ufaransa na nyingine ya Senegal, amesema vikosi vya usalama vilikuwa vimekasirishwa na hali ya mkanyagano iliyotokea.

Takriban watu 130 wamekwishauawa baada ya wanajeshi kufyatua risasi za kutawanya watu waliokuwa wakiandamana kutokana na uvumi kuzagaa kwamba Kapteni Camara anataka kugombea urais katika uchaguzi mkuu mwakani.

Watu walioshuhudia wamesema wanajeshi pia walishambulia watu kwa kutumia visu na singe za bunduki zao.

Waathirika wa ghasia hizo pamoja na watu walioshuhudia, wameliambia Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lenye makao yake mjini New York, baadhi ya wanawake walioshiriki maandamano hayo walidhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na kuwekwa utupu na vikosi vya usalama.

No comments:

Post a Comment