KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 29, 2009

Njaa yaikumba Afrika Mashariki


Shirika la Oxfam limewasilisha ombi la msaada wa dharura wa dola za kimarekani milioni 15.
Fedha hizo zina nia ya kusaidia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa nchini Ethiopia na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Uingereza limesema idadi kubwa ya wanyama wamekufa kutokana na ukame, ambao umeleta athari kubwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Dalili zinaonyesha kuwa maisha ya watu milioni 23 yako hatarini, ambapo ni mara dufu ya hatari kama hiyo iliyotokea mwaka 2006.

Nchi saba zimeathirika na baa hilo la njaa, nusu walio katika hatari hiyo wakiwa wanaishi Ethiopia.

Nchi nyingine zilizoathirika ni pamoja na Kenya, Uganda, Somalia, huku Sudan, Djibouti na Tanzania zikionekana nazo kukumbwa na tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment