KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, September 25, 2009

NILIPOPEWA THAMANI NA UTUKUFU WA KUUMBWA NA KUISHI MAISHANI MWANGU


ASALAMU ALAYKUM MAISHANI?
KWAJINA NAITWA ERITREAN BEAUTY.
UMRI WANGU NI MIAKA 15 (YEARS). NAPENDA SANA NCHI YANGU, NDIO MAANA NAJIHISI KUWA NAFURAHA MAISHANI MWANGU.
NILIPOPEWA THAMANI NA UTUKUFU WA KUUMBWA NA KUISHI MAISHANI MWANGU NI KIWA NA JINSIA YA KIKE. NAFURAHIA JINSIA YANGU, KWAKUWA NDILO CHAGUO LA MUUMBA(MWENYEZI MUNGU) WANGU. HAKUNA JAMBO AMBALO LITATENDEKA AU KUWEPO DUNIANI BILA MATAKWA YAKE(MUNGU). NAJIVUNIA KUWA NA RANGI NYEUSI KAMA NNAVYOJIVUNIA KUZALIWA KATIKA NCHI YA AFRICA. SINA IMANI WALA MTAZAMO WA KUBADILI RANGI YANGU YA NGOZI, NAKUIFANYA IWE NYEUPE, KWASABABU SHUKURANI YA NAFSI YANGU JUU YA MUUMBA WAKE ITAKUWA HAINA MAANA. IKIWA MWENYEZI MUNGU ALINIUMBA NA AKANICHAGULIA RANGI NYEUSI KAMA PAMBO LANGOZI NA KISHA AKANIFANYA NIZALIWE NDANI(AFRICA) YA ASILI YAKE (RANGI NYEUSI). BASI NASEMA ASANTE MUNGU, WEWE NDIE NNAE KUABUDU MILELE NA MILELE WALA HUNA MSHIRIKA KATIKA UTAWALA WAKO.
NAFURAHI SANA NA KUJISIKIA, NNAPOITWA JINA LANGU(ERITREA BEAUTY), KWA SABABU LINANIFANYA NIENDELEE KUJIPENDA NA KUPENDA NCHI YANGU. NAYOTE SIWEZI KUWA NAYO, BILA KUMSHUKURU MUNGU, KWA KUNIPA WAZAZI WAZURI NA WALIOVUMILIA KULINDA ASILI YAO YA UAFRIKA NA KISHA WAKANIPA KIJISEHEMU KATIKA ASILI (MUAFRICA) YAO. NNA MSIFU MUNGU KWA KUNIPA RANGI AMBAYO SIRAHISI KUKUMBANA NA MARADHI YA KILA AINA, NGOZI YANGU NAIFURAHIA SANA HASA PALE AMBAPO, NIONAPO KWAMBA INA RANGI AMBAYO SI RAHISI KUPATIKANA KOKOTE AFRICA, BALI BADHI YA SEHEMU DUNIANI ZIKIONGOZWA NA AFRICA.
NAIPENDA AFRICA KWASABABU NDIO ASILI YA MAISHA YANGU NA CHIBUKO LA RANGI YANGU.
NAWATAKIA KILA LAGHERI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI. INSHALLAH MWENYEZI MUNGU ATUPE MOYO WA KUPENDANA BILA KUJALI RANGI, UKABILA, KOO, LUGHA, CHEO…….N.K.
NABII MUHAMMAD (S.A.W) ANASEMA:
“MWENYEZI MUNGU HUPENDA KUMWONA MJA WAKE AMECHOKA KWA KUTAFUTA HALALI
(RIZIKI YA HAKI HAINA DHULMA NDANI YAKE)”
MPOKEAJI: DAYLAMI

No comments:

Post a Comment