KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 11, 2009

KWA NINI, NNAMPENDA MAMA MZAZI?


KWA NINI, NNAMPENDA MAMA MZAZI?

UPENDO NI KIFAA CHENYE KITUO MOYONI MWA NAFSI. KAZIKUBWA YA UPENDO, NI KUHIFADHI MAPENZI YA NAFSI.
MAPENZI YA NAFSI YANAJENGWA NA MSINGI MZURI WA MANENO NA MATENDO VYA MTU HUSIKA, KATIKA UKUMBI WA MAPENZI.

MAMA MZAZI ANACHUKUWA NAFASI KUBWA SANA KATIKA ULINZI WA MAISHA YANGU. KUNA DALILI NYINGI ZENYE KUONESHA UMUHIMU WA MAMA MZAZI.

BAADHI YA DALILI HIZO, MOJAWAPO NI :

1. KUKUBALI KUPOKEA MBEGU YANGU YA MAISHA YANGU, NA KUIHIFADHI KWA MDA WA MIEZI TISA.
2. KUNILISHA NA KUNINYWESHA NDANI YA HIFADHI YANGU TUMBONI MWAKE NA KUNILINDA JAMBO BAYA KATIKA MDA WAKE WA KUBEBA MIMBA YANGU.
3. MAMA ALIWEZA KUVUMILIA TAABU YA KUBEBA MIMBA NA KUNYIMA MENGI MAZURI KATIKA MDA WA MAISHA YANGU YA TUMBONI, NA AKWEZA KUHIMILI NA KUVUMILIA KATIKA MDA WAKE WA KUJIFUNGUA
(KUTOA NAFSI YANGU KATIKA TUMBO LAKE KWA HAKI NA SALAMA).
NNAMENGI YA KUTAJA KUHUSU MAMA MZAZI LAKINI KUYAMALIZA SIO RAHISI NA MENGI MAZURI ALIYATENDA JUU YA NAFSI YANGU NI SIRI YAKE.
MAMA ALIWEZA KUPUNGUZA MDA WAKE WA USINGIZI, KULA NA KUNYWA VIZURI, KWASABABU YA ULINZI WA MAISHA YANGU.

MAMA HAJANIWEKA MBALI NA MAAMUZI YAKE, ALIKUWA NI MWINGI WA KUFUATILIA MAISHA YANGU KATIKA MUONO MAKINI. VILE VILE MAMA NI MSINGI WANGU WA MUONGOZO MAISHANI MWANGU.

MAMA ALIWEZA KULINDA AHADI YAKE NA BABA, KWA ULINZI BORA WA MBEGU YAKE (MAISHA YANGU).USIPOFUNZWA NA MAMA HUFUNZWA NA DUNIA KATIKA MSINGI WA MACHUNGU NA WIVU WA MAENDELEO. MAMA HANA MSINGI WA WIVU JUU YA MWANAE, BALI HUPENDA KILA JAMBO ZURI APATE MWANAE.

NAKUPENDA MAMA, WALA SITAKUSALITI MAISHANI MWANGU. ALINZI WAKO KATIKA UTU WA KIBINADAMU, NTAUFANYA KATIKA MUUNDO WA MAOMBI MAZURU. SINTAKUSAHAU KWASABABU NIJAMBO
AMBALO HUJANIFUNDISHA MAISHANI MWANGU. MUNGU YUPO NAWE MAMA. MAPENZI YAKO JUU YANGU NDIO MSINGI WA MAPENZI YANGU JUU YAKO MAMA. DOA SINA JUU YAKO, NDIO MAANA NAKUPENDA MAMA.

No comments:

Post a Comment