KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 11, 2009

Kuondolewa kwa mkuu wa kikosi cha Polisi nchini Kenya


Hisia na maoni mbali mbali yamejitokeza kufuatia kuondolewa kwa Mkuu wa Kikosi cha Polisi nchini Kenya Meja Jenerali Hussein Ali.


Meja Jenerali Ali ameteuliwa kuwa Msimamizi Mkuu wa Shirika la Posta nchini Kenya na nafasi yake kuchukuliwa na Mathew Kirai Iteere aliyekuwa kamanda wa kikosi cha polisi wa kupambana na ghasia – GSU.

Ali ambaye alikuwa katika wadhifa huo wa ukuu wa polisi kwa muda wa miaka sita amekumbana na changamoto nyingi zikiwemo kukabiliana na kundi haramu la Mungiki, sifa mbaya ya kikosi cha polisi na tuhuma za kikosi hicho kuhusika katika mauaji ya kiholela. Shutuma kuu aliyoipata ni kushindwa kuzuia machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu mwanzoni mwa mwaka uliopita.

Kutoka Nairobi Alfred Kiti ametutumia taarifa ifuatayo...

Imetayarishwa na Alfred Kiti

Mpitiaji:Aboubakary Liongo

No comments:

Post a Comment