KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 25, 2009

“ KWA NINI KILA MTU ANAWEZA KUSEMA UONGO?”


A.W.W
MAMBO VIPI MAISHANI CLUB?
NATUMAI WOTE MNAENDELEA VIZURI KATIKA MFUNGO WA RAMADAN.
UJUMBE WANGU KWA LEO, UNAHUSU “ KWA NINI KILA MTU ANAWEZA KUSEMA UONGO?”
UONGO MFUMO WAKE, UNAMSINGI WA KWENDA KINYUME KATIKA MATENDO NA MANENO. MARANYINGI, BAADHI YA BINAADAMU WANACHUKIA KUAMBIWA AU KUSEMA UONGO, LAKINE KWA UPANDE MWINGINE, HUJIKUTA WAKITUMIA UONGO KAMA KINGA YA KUENDELEZA MFUMO WA UHUSIANO HUSIKA. TUNAPOSEMA MFUMO WA UHUSIANO, TUNAMAANISHA KULINDA MASLAHI YA NAFSI YAKO.
LICHA YA KILA NAFSI KUCHUKIA KUAMBIWA UONGO, KUNA SIKU AMBAYO NAFSI HIYO YENYE KUCHUKIA UONGO, NAYO HUJIKUTA KATIKA NJIA YENYE MATUMIZI YA UONGO, MOJA WAPO YA NJIA YA KUJIHAMI AU KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUPATA JAMBO FULANI KUTOKA SEHEMU FULANI.
KWAMFANO:
UHUSIANO WA MWANAMKE NA MWANAUME (BOY FRIEND OR GIRLY FRIEND).
KWA UTAFITI ULIOFANYWA NA MAISHANI CLUB. UNAONESHA KWAMBA ASILIMIA TISINI 90%, YA UHUSIANO WA VIJANA WENYE UMRI KUANZIA MIAKA 12 HADI 35 WA JINSIA ZOTE (WANAUME NA WANAWAKE), HUJIKUTA KATIKA UHUSIANO WENYE MSINGI WA PENZI LA UONGO. MSINGI WA PENZI LA UONGO UNA MAANA GANI?
• MAANA YA UHUSIANO WENYE MSINGI WA PENZI LA UONGO, NI KUMDANGANYA MWANAMKE AU MWANAUME, ILI AWEZE KUKUPENDA. WANAUME WANABEBA ASILIMIA THEMANINI 80%, KATIKA UHUSIANO WA MBINU YA UONGO NA WANAWAKE WANABEBA ASILIMIA 20%.
• WANAUME WANAMFUMO WA KUTUMIA, MBINU ZA KULAGHAI KUPITIA MILIKI (MAGARI, NYUMBA, PESA YA MSIMU, MAVAZI YA KUAZIMWA, MANENO MAZURI NA YENYE VIONJO VINGI VYA KUJENGA IMANI YA MWANAMKE…..N.K). MWANAUME HUCHUKUWA NAFASI HII, KWA KUMSHAWISHI MWANAMKE, NA KUGENGA MSINGI WA KULAZIMISHA PENZI NDANI YA MOYO WA MWANAMKE, KUPITIA NJIA YA VISHAWISHI VYA MATENDO NA MANENO. MWANAMKE MWENYE UPUNGUFU AU MAHITAJI YA FEDHA, HUJIKUTA KATIKA MTEGO WA VISHAWISHI VYA MWANAUME. MARANYINGINE KUNA WANAWAKE WENYE HIFADHI YA TAMAA NDANI YA NYOYO ZAO, HAWA HUWA NI RAHISI KUJIKUTA KATIKA MTEGO HUO. KWASABABU WANAPENDA KUONEKANA KATIKA JAMII WAKILA AU KUTEMBELEA SEHEMU ZA KIFAGHARI. NA MARANYINGINE WANAWAKE HAO, HUWA NI WENYE TAMAA YA KUVAA AU KUMILIKI VIFAA VYA MAWASILIANO VYENYE BEI KUBWA NA MARANYINGINE HUJIKUTA WAKIHITAJI KUISHI KATIKA NYUMBA ZA KUPANGA AMBAZO NI NZURI, NA KUMBUKA KWAMBA UZURI WA NYUMBA NDIO UKUBWA WA GHARAMA YA KODI NA UENDESHAJI (UMEME, MAJI, KULIPA MFANYAKAZI….N.K). HAYO YOTE NI BAADHI YA MAMBO AMBAYO YANAMVUTIA MWANAMKE MWENYE TAMAA YA MALI. NJIA HII YA MWANAUME KUTUMIA PESA AU MALI YAKE KUMSHAWISHI MWANAMKE AU WASICHANA WADOGO NA WENGI WAO WAKIWA NI WENYE UKOSEFU AU KIPATO CHA CHINI, HUWA NI YENYE KUSABABISHA MAGONJWA YA ZINAA NA KUONGEZA WATOTO WA HARAMU (WATOTO WALIOPATIKANA BILA MKATABA WA NDOA HALALI), MTAANI AU MAJUMBANI. NA NJIA HII HUONDOA HESHIMA YA FAMILIA AU UKOO FULANI. VILE VILE NJIA HII, HUMTEGENEZEA MSICHANA HUSIKA, KUSHINDWA KUPATA ULINZI WA NGONO, KWASABABABU ANAPOTOSWA, HUWA NI MWENYE KUONGEZA IDADI YA WANAUME, ILI APATE MATUMIZI YAKE NA MATUNZO YA MWANAE. NA MARANYINGINE HUJIKUTA KATIKA UKINGO WA KUONGEZA IDADI YA WATOTO HARAMU NA MARANYINGINE, ANAPOAMBUKIZWA UKIMWI HUJIKUTA AKIACHA WATOTO RUKUKI, BILA MAANDALIZI YA MAZINGIRA YAO YA HIFADHI.
• KWA UPANDE WA VISHAWISHI VYA UONGO KUTOKA KWA MWANAMKE KUELEKEA KWA MWANAUME, HUWA NI VYENYE(VISHAWISHI) NGUVU NA VYENYE KUPENDEZA KATIKA MDA MUAFAKA.
• KWA SABABU, MWANAUME ANATEGEMEA NGUVU NA AKILI YAKE, ILI AWEZE KUFANIKISHA NDOTO YAKE MAISHANI. MWANAUME MWENYE KUKATA TAMAA, HUWA NI MWENYE ROHO MBAYA NA KUFIKIA HATUWA YA KUWEZA KUJITOWA NAFSI YAKE, KUTOKANA NA KUSHINDWA KUENDESHA MAISHA YAKE. MWANAUME MWENYE UPUNGUFU AU UKOSEFU WA KIPATO, HUWA NI MWENYE KUTAWALIWA NA UDHAIFU WA MAAMUZI.
• NJIA HII YA UDHAIFU, HUMPA MWANAMKE WENYE MAHITAJI YA PENZI, RAMANI YA KUMPATA MWANAUME HUYO, BILA HATA UGUMU WA MAJADILIANO. KWASABABU, KIJANA (MWANAUME) HUYO, YEYE HUONA KAMA ZARI AU BAHATI ILIOMDONDOKEA KUTOKA MBINGUNI. KIJANA HUYO KUMSHAURI AU KUMUOMBA AJIESHE NA VISHAWISHI VYA UONGO VYA MWANAMKE HUSIKA,HUWA SIO RAHISI. KWASABABU KIJANA, ATAMUONA MWANAMKE HUYO NI MKOMBOZI WASHIDA ZAKE (CHAKULA, MAVAZI, MARAZI, MATIBABU, NAULI AU KUPEWA USAFIRI, KUPEWA KIASI FULANI CHA PESA AU MALI……N.K). YOTE HAYA KIJANA HUYO (MWANAUME) ALIKUWA HAWEZI KUYAPATA KATIKA JAMII ILIOMZUNGUUKA, BALI HUONA MWANAMKE HUYO ALIYE JITOKEZA KATIKA JAMII, NA KUJALI HISIA ZAKE ZENYE MSINGI WA TAABU NA MAUMIVU HADI KUFIKIA HATUWA YA KUPOTEZA MUELEKEO WA MAISHA, NDIE MTU MWENYE THAMANI NA UMUHIMU MAISHANI MWAKE.
• NJIA HII HUWA NDICHO CHANZO CHA VIJANA WENGI WENYE KULELEWA NA SHUGA MAMI, KUAMBUKIZWA MAGONJWA YA ZINAANA MOJAWAPO KATIKA MSINGI WA MAGONJWA HAYO NI UKIMWI( HAIV/ AIDS).

No comments:

Post a Comment