KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, September 25, 2009

JE! SIRI ISINGEKUWEPO WATU WANAFIKI WANGEISHIJE?


SIRI NA BAADHI YA NJIA ZAKE

SIRI NI KIFAA CHENYE MFUMO WA MAFICHO YA MATENDO NA MANENO YA NAFSI. KILA NAFSI HUPENDA KULINDA NA KUTETEA MASLAHI YAKE, KATIKA MISINGI YA UTULIVU NA AMANI.
NAFSI INAWEZA KUHIFADHI SIRI NDANI YAKE NA MARANYINGINE NAFSI INAWEZA KUAMUA KUCHANGIA SIRI YAKE NA MTU AU WATU, KWA MASHARITI FULANI.
TUNAPOZUNGUMZIA SIRI YA NAFSI MOJA, HATUMAANISHI KWAMBA KILA JAMBO LA NAFSI HALINA UWAZI SEHEMU NYINGINE. BINAADAMU ANAO UWEZO WA KUFICHA MAMBO YAKE NA MTU MWINGINE ASIJUWE, LAKINI KUNA NJIA NYINGINE YA MVUJO WA SIRI YAKE.

UWEZO WA MWENYEZI MUNGU JUU YA SIRI YA MTU


KWAMFANO, MWENYEZI MUNGU ALIUMBA KILA KITU KWA UWEZO WAKE, BILA KUMSHAURI AU KUHITAJI MSAADA KUTOKA KWA MTU MWINGINE AU KIUMBE CHOCHOTE.HUU NI UWEZO WA MUNGU NA NI MKUBWA KATIKA KUANGALIA KILA TENDO LA MASHA YA VIUMBE WAKE. KWA NJIA HII MWANADAMU HAWEZI KUMFICHA MWENYEZI MUNGU JAMBO LOLOTE, LAKINI BINADAMU ANAWEZA KUWAFICHA BINAADAMU WENZAKE SIRI AU SIRI ZAKE, LAKINI SIO MWENYEZI MUNGU.

VIPI KUHUSU MALAIKA ?

KILA BINADAMU ANATEMBEYA NA MALAIKA WA WILI AMBAO NI WAANDISHI WA MATENDO YAKE. MALAIKA WA KULIA YEYE KAZI YAKE NI KUANDIKA KILA TENDO NA NENO ZURI, LITOKALO KWENYE NAFSI HUSIKA.
MALAIKA WA KUSHOTO YEYE KAZI YAKE NI KUANDIKA KILA NENO NA TENDO BAYA KUTOKA KWENYE NAFSI HUSIKA.
HII NI NJIA MOJAWAPO MWENYEZI MUNGU AMEIWEKA ILI KUWEKA KUMBUKUMBU ZA KILA NAFSI KATIKA MAANDISHI.

KWA MUJIBU WA MWENYEZI MUNGU, SIKU YA MALIPO (BAADA YA KIFO KUNA UKAGUZI WA MATENDO NA MANENO YA KILA NAFSI ), KILA NAFSI ITAKABIDHIWA KITABU CHAKE CHENYE TAARIFA KAMILI YA MATENO NA MATENDO ILIOYATUMIA ENZI ZA UHAI WAKE, HII NJIA YA MAANDISHI ITAKUWA NI USHAHIDI TOSHA KATIKA MAANDISHI NA MWENYEZI MUNGU ATAAMUSHA KUMBUKUMBU YA KILA NAFSI ILI IWEZE KUKUMBUKA KILAJAMBO LILILOMO KITABUNI MWAKE.KITABU KITATOLEWA KATIKA NJIA MBILI, AMBAZO KUNA NJIA YA MKONO WA KULIA. WATAKAOPEWA KITABU CHAO KATIKA NJIA HII, YENYE THAMANI YA UPANDE WA KULIA, ATAKUWA MIONGONI MWAWATU WENYE MALIPO BORA YA PEPO. NA WENYE KUPOKEA KITABU CHA MALIPO SIKUYA KIAMA, KATIKA MKONO WA KUSHOTO, HAO NDIO WENYE KHASARA YA MALIPO YA MWENYEZI MUNGU. KILA JAMBO MAISHANI NI MTIHANI, KWA BINAADAMU.
UNAPOTENDA MEMA UNAJENGA AMANI DUNIANI, NA KUJIWEKEA NAFASI NJEMA YA KUPOKEA KITABU CHAKO CHA MALIPO SIKU YA KIAMA, KATIKA MKONO WA KULIA.
NA UBAGHILI NI UJENZI WA CHUKI DUNIANI NA UKARIBISHO WA MAPOKEZI YA KITABU CHA MALIPO SIKU YA KIAMA, KATIKA MKONO WA KUSHOTO.

NDIO MAANA TUNASEMA UNAWEZA KUMFICHA BINAADAMU MWENZIO SIRI LAKINI MUNGU ANASIKIA NA KUONA KILA JAMBO NA AMEKUWEKEA WA KAGUZI KATIKA KILA NENO NA KILA JAMBO ULIFANYALO.


SIRI BAINA YA NAFSI NI MAUMIVU

SIRI BAINA YA NAFSI NI MAUMIVU. MAUVU YA NAFSI JUU YA SIRI FULANI, YANATOKANA NA MSINGI MGUMU WA KUFUTA ILE SIRI MOYONI MWAKE. KIFUTIO CHA SIRI KINAHITAJI MATUMIZI YENYE MSINGI WA UAMINIFU NA NGUZO YA UTULIVU MAISHANI MWETU.
UKITUMIA KIFUTIO CHA SIRI VIBAYA BILA UANGALIFU, UTAJIKUTA UKIWA NI MTU MWENYE NAFSI YA KUHANGAIKA, KHOFU, LAWAMA……...NK.

MIFANO :

UNAJISIKIAJE UNAPOMPA SIRI RAFIKI YAKO WA KARIBU ?

JIBU LAKE NI KWAMBA UNAJISIKIA VIZURI NA LENGO LAKO LINAHITAJI MSAADA KWAKE, WA MAWAZO YA MANENO NA VITENDO. RAFIKI YAKO ANAPOKUSAIDIA KIMAWAZO AU KIVITENDO AU VYOTE, KWA KWELI UTAHISI WEPESI KATIKA MOYO WAKO NA UTAENDELEA KUMPENDA ZAIDI YA MWANZO. LICHA YA RAFIKI YAKO KUKUSAIDIA MAWAZO NA MATENDO, KUNA JAMBO LINGINE LILILOBAKI, NALO NI KUHIFADHI, KUTETEA NA KULINDA SIRI YA RAFIKI YAKE KWA HALI NA MALI. HUU NDIO MFUMO WA HIFADHI YA SIRI BAINA YA NAFSI MBILI.

KINYUME CHAKE

UNAJISIKIAJE, UKIMPA RAFIKI YAKO SIRI YAKO NA AKASHINDWA KUKUSAIDIA KIMAWAZO NA KIVITENDO, NA MWISHO WAKE UKAANZA KUSIKIA MAZUNGUMZO YA SIRI YAKO MTAANI ?

KWA KWELI, UTAJISIKIA VIBAYA NA UTATAABIKA NA UTAMCHUKIA RAFIKI YAKO NA KUANZA KUJUTA UKIILAUMU NAFSI YAKO KWANINI ILIWEZA KUTOA SIRI YAKE, NA KUIPELEKA KATIKA NJIA MBOVU YA RAFIKI AU YA HIFADHI.
NDIO MAANA TUNASEMA UNATAKIWA UTATUWE SIRI YAKO KATIKA MSINGI WA ELIMU. SIRI AU AIBU YA MTU INAPOVUJA NA KUSIKIKA MTAANI, ATAJIKUTA MTU HUSIKA AKIINGIA KATIKA VITA VYA CHUKI YENYE KUTOKANA NA MAZUNGUMZO YA MTAANI, YATAMFANYA MWENYE AIBU ASIWEZE KUWA NA AMANI NA UTULVU NAFSINI MWAKE.
UKOSEFU WA AMANI NA UTULIVU JUU YA NAFSI HUSIKA, UMESABABISHWA NA SIRI, NA UMESAMBAZWA NA RAFIKI MNAFIKI MWNYE UKOSEFU WA UADILIFU NDANI YA MOYO WAKE. RAFIKI AU HIFADHI MBOVU YA SIRI NI CHANZO KIBAYA KABISA CHA MAGONJWA YA MOYO NA PURESHA, CHUKI NA LAWAMA, HASIRA NA UPUNGUFU WA UZITO WA MWILI NA AKILI…..N.K.

USHAURI KUHUSU SIRI

JITAHIDI KATIKA MAISHA YAKO KUMTAFUTA RAFIKI AMBAE SI MNAFIKI, NA UTAMTAMBUA KWA MANENO NA MATENDO YAKE. JIEPUSHE NA RAFIKI AMBAE ANATUMIA MDA WAKE KUWAONGELEA WATU AU MAMBO YASIYOMUHUSU, HUYO SIO RAFIKI BORA. KWASABABU NAWE UKISHAMPA MGONGO AU NAFASI, ANAWEZA KUONGEA MENGI KUKUHUSU KWA WATU WENGINE NA KWAMAANA HII, KUTAKUWA HAKUNA SIRI BAINA YENU NA KITAKACHO TAWALA BAADAE NI CHUKI NA MAUMIVU.

TAFUTA RAFIKI, AMBAE ANAWAZA KUHUSU MAZINGIRA YA MAENDELEO YA DUNIA SIO YULE MWENYE KUWAZA FULANI KASEMAJE?, KALANINI?, AMEENDA WAPI?, AMENENEPA AU AMEKONDA?, MKE…?….MME….?..N.K.

HUYU ATAKUPOTEZEA NIA HATA KAMA ANA MANENO YA ASALI NA HARUFU YA UBANI, MWISHO WAKE ATAKUFANYA UPOTEZE THAMANI NA MALENGO YA NAFSI YAKO.
KUWA NA RAFIKI MWENYE MAWAZO MAZURI NA MWENYE MSAADA KATIKA MANENO NA VITENDO. RAFIKI MWENYE MSAADA KATIKA MANENO NA VITENDO, MARANYINGI HUWA NA HIFADHI NZURI YA SIRI MOYONI MWAKE. MPE SIRI YAKO AKUWEKEE.

JE, UKIMKOSA RAFI MUADILIFU UFANYEJE ?

HALI YAKO ITAKUWA NGUMU KIDOGO KWASABABU HUNA MTU MUAMINIFU WA KUBADILISHANA NAYE MAWAZO. UNATAKIWA KUSOMA SANA VITABU
( TORATI, ZABURI, NJIRI NA QURAN ) VYA MUNGU, VITAWEZA KUPOOZA MOYO WAKO KWA NJIA YA UTULIVU NA MSINGI WA UVUMILIVU.

UTAWEZA KUSOMA NA KUELEWA KWAMBA KILA JAMBO MAISHANI LINA WAKATI WAKE, NAWE KUNA SIKU AMBAYO MUNGU AMEKUPANGIA KUISHI KATIKA MAUMIVU NA MWISHO WA MAUMIVU NI FARAJA.
UNATAKIWA KUWA MVUMILIVU SANA TENA SANA, KWASABABU UNAWEZA KUJIKUTA, UKIMUASI MUNGU NA KUFUATA WALE MARAFIKI WA BAYA, TENA MARANYINGINE UNAWEZA KUJIKUTA KATIKA MATENDO YA UBAYA ZAIDI YA WALE ADUI ZAKO,
KWASABABU UTAJIKUTA UKIINGIA KATIKA VITA YA KUJIHAMI KATIKA MSINGI WA MANENO NA MATENDO.
KUJIHAMI KWAKO KUNAWEZA KUPUNGUZA HURUMA NA KUJENGA MSINGI WA KULIPIZA KISASI, NA MWISHO WAKE WEWE UTAONEKANA MBAYA KATIKA JAMII, WAO (MAADUI) WANAWEZA KUONEKANA VIVURI KATIKA JAMII, KWASABABU WAO (ADUI) TAYARI HUJIPANGA TENA KATIKA VITA BARIDI YENYE UTULIVU MBELE ZA WATU NA WENYE MASHAMBULIZI KATIKA NJIA YA MAFICHO(MAPAMBANO YA WENYE KUNDI AU MTU NA ADUI ZAKE). NA UTAWAPA VIGEZO VYA MANENO NA MATENDO KUTOKANA NA HASIRA ZAKO,. SIKU ZOTE UKIMIA NI PIGO KUBWA KATIKA VITA BARIDI, NA NI USHINDI KWA MSHAMBULIWAJI.
UKOSEFU WA UKIMIA KATIKA VITA BARIDI, NI UPUNGUFU WA NGUVU NA HOJA KATIKA MANENO NA VITENDO NA NI NJIA BORA YENYE MSINGI WA UPENYO WA MAADUI ZAKO. KWASABABU WATU HUTAFAKARI KILE ULICHOKIONGEA NA KUKITENDA, NA KUMBUKA KWAMBA KILA MTU HUWA NA MAONI YAKE JUU YA JAMBO HILO. NJIA HII INAWEZA KUWAFANYA ADUI ZAKO KUTENGENEZA AU KUUNGANISHA HOJA ZAO, NA KUANZISHA UZUSHI MKUBWA NA WENYE MADHARA KWAKO BILA KUSAHAHU BAADHI YA WATU KATIKA JAMII.

CHANZO CHA MAUMIVU NI NINI ?

CHANZO CHA MAUMIVU NI MATENDO NA MANENO KUTOKA KWENYE NAFSI YA MTU FULANI. BINAADAMU HAJENGI UADUI NA MIMEA AU MAJI, BALI BINADAMU NI MAADUI WENYEWE KWA WENYEWE.

FAIDA YA SIRI

FAIDA YA SIRI NI ULINZI WA MASRAHI YA NAFSI HUSIKA. KWASABABU KUNA WATU AMBAO UKIWAAMBIA MPANGO WAKO WA KIMAENDELEO, HUCHUKUWA HATUWA YA KUKUHARIBIA KILA NJIA YA KUFANIKISHA JAMBO LAKO. NA MARANYINGINE WAKISHINDWA KUKUSIMAMISHA KATIKA HATUWA ZA MAENDELEO, HUCHUKUWA JUKUMU AU MAAMUZI YENYE MSINGI WA MADHARA.
KAMA : MATUMIZI YA UCHAWI AU KULOGA, SABABU YA KIFUNGO AU KIFO. YOTE HAYA YAPO NA YANASIKIKA KILA KUKICHA NA TUNAYASHUHUDIA KWENYE LUNINGA NA MAGAZETI. WATU WANACHAFUANA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI,ILI MRADI WAPOTEZE THAMANI YA MTU (NAFSI) HUSIKA.

NDIO MAANA WATU WENGI KWASASA WANAFANYA MABO YAO KWA UFICHO WA HALI YA JUU, NA NJIA HII NI NJIA YENYE MSINGI WA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA IMANI NA UADILIFU BAINA YA BINAADAMU.

YOTE HAYA NI NJIA AU MBINU ZA MAISHA YA BINAADAMU, KATIKA KARINE HII YA UTANDA WAZI.
MWENYEZI MUNGU NDIE HAKIMU BORA, KWA SABABU YEYE NI MTOWAJI WA RIZIKI NA UHAI NA MWISHO WAKE RIZIKI INAONDOKA NA KIFO KUTAWALA.
NA KUMBUKA LICHA YA VURUGU HIZI MAISHANI MWETU MWISHO WAKE TUNAKUFA, NA MARANYINGI WATU HUFA NA SIRI ZAO. KIFO CHA SIRI NI KIBAYA KWASABABU ILE SIRI ILIOONDOKA NA ROHO YAKE, INGEWEZA KUSAIDIA WATU WENGI DUNIANI, LAKINI KUTOKANA NA VURUGU ZA MATENDO MABOVU YA BINAADAMU TUNAKOSA AU KUPUNGUZA NJIA ZETU ZA MAFANIKIO BILA KUJITAMBUA.

KIFO CHA BINAADAMU KINAONDOKA NA SIRI NYINGI SANA ZIKIWEMO ELIMU, NJIA ZA BUSARA UTENDAJI BORA WA KAZI…….N.K.

KUNA BAADHI YA WARITHI AU WANA FAMILIA KATIKA KUNDI LA BINAADAMU, MARA NYINGINE HUJIKUTA KATIKA UTATA WA KURITHI MALI ZINAZOONEKANA, LAKINI MWANZO HAWAJAWEZA KUFIKIRI KURITHI HEKIMA, SIRI AU ELIMU YA MAREHEMU KABLA YA KIFO CHAKE. KUTOKANA NA TAMAA ZETU BINADAMU, SIKU ZOTE TUNAJIKUTA TUKIPOTEZA KILA JAMBO ZURI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA AMANI NA UTULIVU KATIKA NAFSI ZETU, TUMETAWALIWA NA CHUKI, HUSDA, LAWAMA, ………MAISHANI MWETU. UKOSEFU WA AMANI NA UTULIVU NDIO NJIA BORA YA UPUNGUFU WA MAENDELEO, KWASABABU MAENDELEO YANATOKANA NA UMOJA KATIKA JAMII, IKIWA JAMII IMEGAWANYIKA KATIKA MGAWANYIKO WA CHUKI, LAANA, FITINA, UKOSEFU WA UADILIFU……..LAZIMA MAENDELEO YATAPUNGUA KATIKA MFUMO WA KUTUMIA GHARAMA KUBWA YA PESA, MDA,….KATIKA VITA VYA MANENO NA UPUNGUFU WA UTEKELEZAJI WA UADILIFU KATIKA KILA KUNDI.

HUU NDIO MFUMO WA BINADAMU AMBAYE HUJIWEKA KATIKA CHEO KIKUBWA NA KUJIITA MAJINA NA KUJIPA ULINZI WA DUNIA AU KUTOA MAAMUZI BILA KUJALI HASARA ITAKAYOJITOKEZA.
NA MARANYINGINE AKISAHAU KWAMBA MWISHO WA UHAI WAKE ANASAHAULIKA HARAKA NA KINACHO KUMBUKWA NA WATU WAKE NI PESA NA MALI ZAKE AU MATENDO YAKE KWA WALE WATENDEWAJI.

SIRI NI HAZINA KUBWA NA MUHIMU KATIKA MAISHANI.
BINADAMU AKIWEZA KUFICHUWA SIRI NA KUILINDA NA KUIFANYIA KAZI KATIKA NJIA YA MAENDELO ISIWE NJIA YA FITINA NA KUJENJA CHUKI NA KUSABABISHA LAWAMA NA VIFO, BASI DUNIA YETU ITAKUWA NA MSINGI BORA KATIKA HAKI.

QURANI :

MWENYEZI MUNGU ANASEMA “ KWA HAKIKA MWENYEZI MUNGU NI MJUZ WA SIRI ZA MBINGUNI NA ARDHINI; BILA SHAKA YEYE NI MJUZI WA YALIYOMO VIFUANI (SEUZE YALIOMO NJE)
(35:38)

ZINGATIA UKIWA NA SIRI YA UBAYA, MWENYEZI MUNGU ANAIJUA NA IKIWA NI YA KHERI MWENYEZI MUNGU ANAIJUA.

BIBLIA :

YESU AKASEMA “ANGALIENI MSIFANYE WEMA WENU MACHONI PA WATU, KUSUDI MTAZAMWE NA WAO; KWA MAANA MKIFANYA KAMA HAYO, HAMPATI THAWABU( THAWABU NI MALIPO YA MWENYEZI MUNGU JUU YA WACHA MUNGU) KWA BABA YENU ALIYE MBINGUNI.

BASI WEWE UTOAPO SADAKA, USIPIGE PANDA MBELE YAKO, KAMA WANAFIKI WAFANYAVYO KATIKA MASINAGOGI NA NJIANI, ILI WATUKUZWE NA WATU. AMIN, NA WAAMBIENI, WAMEKWISHA KUPATA THAWABU YAO. BALI WEWE UTOAPO SADAKA, HATA MKONO WAKO WA KUSHOTO USIJUE UFANYALO MKONO WAKO WA KUUME; SADAKA YAKO IWE KWA SIRI; NA BABA ( MWENYEZI MUNGU) YAKO AONAYE SIRI ATAKUJAZI”.

(MATHAYO MTAKATIFU 6 : 1….4)

KWA MAANDIKO HAYA TUNAONA YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU HAWAPENDI WANAFIKI, WANAOTOA ILI WAONEKANE NA KUJIJENGEA MSINGI WA SIFA.
IKIWA UNA JAMBO LA KUMSAIDIA BINADAMU MWENZAKO UNATAKIWA UMSITIRI KATIKA NJIA YA SIRI. SIO UMEMPA MTU NA KUMTANGAZA KWA WATU KWAMBA CHAKULA AU SHATI AU NAULI UMEMPA WEWE, HII NI NJIA MBAYA NA YA KUMCHUKIZA MWENYEZI MUNGU.
KWA KARINE YA SASA WATU WANATOA, ILI WAONEKANE
(KUUZA SURA KATIKA NJIA YA SADAKA). YOTE HAYA TUNAYASHUHUDIA KATIKA VYOMBO VYA HABARI NA KUYASIKIA MIDOMONI MWA WATU NA KUYAONA AU KUYATENDA MAISHANI MWETU. SIRI NI NJIA BORA YA STARA, KWA WATU WENYE ELIMU BORA KUHUSU SIRI.
KILA JAMBO LA GHERI NI GUMU KULITEKELEZA, ISIPOKUWA JUU YA WACHA MUNGU. MTU AMBAYE NI MCHA MUNGU, ANA HAZINA BORA YA SIRI. LAKINI MTU MNAFIKI HAZINA YAKE YA SIRI INAVUJA KILA KUKICHA.

HEBU FIKIRI :

• NI WATU WANGAPI AMBAO WAMEKUPA SIRI ZA WATU WENGINE?
• NI MAMBO MANGAPI AMBAYO YAMEKUELEMEA MAISHANI MWAKO, NA UMEMKOSA MTU WA KUKU SAIDIA KUBEBA MZIGO WA SIRI ZAKO?
• NDOA NGAPI ZINAZO VUNJWA, NA MVUJO WA SIRI?


• JE! SIRI ISINGEKUWEPO WATU WANAFIKI wANGEISHIJE?

CHAGUA RAFIKI BORA, ILI UWEZE KUMPA SIRI ZAKO NA JIEPUSHE NA SIRI YENYE MADHARA JUU YA NAFSI NYINGINE. KUWA NA SIRI YA MAENDELEO MAISHANI MWAKO NA UTABARIKIWA.
KUMBIKA NI VYEMA KUFICHA AIBU YAKO KULIKO KUITANGAZA. NA RAFIKI YAKO AKIKUPA MAWAZO YAKE KATIKA MFUMO WA SIRI, BASI KUWA MWENYE KULINDA SIRI YAKE KATIKA MAZINGIRA YA UAMINIFU. URAFIKI WA UKWELI NI HAZINA BOARA YA SIRI.

No comments:

Post a Comment