KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 13, 2009

Sudan yakanusha kusaidia wanamgambo



Mapigano ya kikabila yauwa wengi kusini mwa Sudan
Maofisa wa serikali kaskazini mwa Sudan wamekanusha kuwapatia silaha wanamgambo walioendesha mashambulio yaliyouwa mamia ya watu katika mapigano ya kikabila hivi karibuni mwa nchi kusini.
Waziri wa masuala ya kibinadamu Abdelbagi Gailani ameyaelezea mapigano hayo kama "vita baina ya makabila" na akasema serikali ya Sudan imejizatiti kuyakomesha.

Takriban watu 185 wa kabila la Lou Nuer waliuawa katika jimbo la Jonglei baada ya wapiganaji wa kabila la Murle kuwashambulia wiki iliyopita.

Kwa mwaka huu pekee mamia ya watu waliuawa katika mapigano kama hayo.

Makamanda wa jeshi eneo la kusini mwa Sudan wameitupia lawama serikali kaskazini mwa Sudan kwa kuwapatia silaha wanamgambo hao.

Lakini Bwana Gailani ameiambia BBC madai hayo hayana mantiki.

Maofisa katika jimbo la Jonglei wamesema watu wa kabila la Lou Nuer walikwenda kuvua samaki kusini mwa mji wa Akobo kutokana na kukabiliwa na upungufu wa chakula ndipo wakashambuliwa.

Wanajeshi saba wa serikali kaskazini mwa Sudan nao ni miongoni mwa watu waliouawa walipokuwa wakilinda ngome yao.

No comments:

Post a Comment