KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, August 13, 2009
Mwanamke mmoja raia wa Sudan anayekabiliwa na kesi ya kuvaa suruali hali inayoonekana ni kwenda kinyume na utamaduni na silka ya nchi hiyo amezuiliwa
Mwanamke mmoja raia wa Sudan anayekabiliwa na kesi ya kuvaa suruali hali inayoonekana ni kwenda kinyume na utamaduni na silka ya nchi hiyo amezuiliwa kusafiri nje ya nchi hiyo.
Mwanamke mmoja raia wa Sudan anayekabiliwa na kesi ya kuvaa suruali hali inayoonekana ni kwenda kinyume na utamaduni na silka ya nchi hiyo amezuiliwa kusafiri nje ya nchi hiyo.
Mwanamke huyo Lubna Hussein amesema alijaribu kutoka nje ya Sudan siku ya Jumanne kwenda Lebanon ambako amealikwa kuonekana katika kituo kimoja cha televisheni.
Amesema afisa mmoja katika uwanja wa ndege alimwabia jina lake limo katika orodha ya watu wabaya tangu siku ya Ijumaa iliyopita, siku ambayo alialikwa na Rais wa Ufaransa Nicholas Sarkozy.
Iwapo atapatikana na hatia katika kipindi cha mwezi mmoja, atakabiliana na hukumu ya kuchapwa viboko hadi 40.
Bi Hussein alijiuzulu kazi yake katika Umoja wa Mataifa ambayo ilikuwa inamkinga asishtakiwe hali iliyodhihirisha anapendelea kesi yake iwe ni jaribio kuudhihirishia ulimwengu juu ya haki za wanawake nchini Sudan.
Mwanamke huyo amesema alikuwa anakwenda Lebanon kushiriki katika kipindi cha mazungumzo kilichoandaliwa na kituo cha televisheni cha Al-Arabiya.
Bi Hussein ameliambia shirika la habari la Associated Press" iwapo lengo ni kunizuia kuzungumza au kuchuja maneno yangu, basi ni wajinga, kwa sababu naweza kuzungumza kwa njia ya simu, kupitia setelaiti au kitu chochote kile.
Chini ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 baina ya Waislamu wengi wanaoishi kaskazini na Wakristo waliopo kusini, sheria za Kiislamu maarufu kama Sharia hazina nafasi kutekelezwa kwa watu ambao si Waislamu wanaoishi mjini Khartoum.
Mwandishi wa BBC James Copnall aliye katika mji mkuu, Khartoum, amesema sio ajabu kuwaona wanawake Waislamu na wasio Waislamu wakiwa wamevalia suruali mjini humo.
Bi Hussein amesema hajafanya jambo lolote kinyume na sheria, lakini anaweza kutolewa kafara kutokana na kifungu katika sheria za uhalifu za Sudan zinazokataza mavazi yasiyokubalika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment