KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 18, 2009

Marekani yazungumzia hatma ya Megrahi


Maseneta wa Marekani wanapinga kuachiliwa kwa mfungwa Abdelbaset Ali al-Megrahi aliyepatikana na hatia kushambulia kwa bomu ndege ya abiria huko Lockerbie katika anga ya Scotland.
Maseneta hao saba wamemhimiza waziri wa maswala ya sheria katika serikali ya Scotland kutomwachilia Bwana Megrahi ambaye ni raia wa Libya.

Megrahi, ndiye Mtu pekee aliyehukumiwa kwa shambulio hilo la ndege ya Pan Am 103, lililowaua watu 270 huko Lockerbie, mwaka 1988.

Maseneta hao, John Kerry na Edward Kennedy, Frank Lautenberg, Charles Schumer, Robert Menendez, Partick Leany na Kristen Gillibard wanadai kwamba kumuachilia huru Megrahi ni kinyume na jitihada za kupambana na ugaidi.

Waziri wa maswala ya kisheria wa Scotland Kenny MacAskill, anatarajiwa kuamua ikiwa Megrahi anayeugua saratani ataachiliwa au kurejeshwa nchini kwake Libya, chini ya mkataba wa ubadilishanaji wafungwa.

Mwaka uliopita, mawakili wa Megrahi waliwasilisha ombi la kuwachiliwa kwa dhamana katika mahakama ya rufa lakini ombi lake lilitupiliwa mbali.

Pendekezo la kumuachia Megrahi limepingwa vikali huko Marekani.

Kati ya abiria 270 waliokufa katika ndege hiyo ya Pan Am, 189 walikuwa raia wa Marekani.

Katika Barua waliomuandikia Bw. MacAskill, maseneta hao wa Marekani walimhimiza ahakikishe kwamba Megrahi anatimiza kifungo chake nchini Scotland.

Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani pia ameongeza uzito wake katika mvutano huu, akikariri kwamba Megrahi anastahili kumalizia kifungo chake Scotland.

No comments:

Post a Comment