KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 17, 2009

Idadi ya vifo Taiwan yaongezeka


Rais wa Taiwan amesema idadi ya watu waliokufa katika maporomoko na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga huenda ikazidi 500, ambapo takribani 400 wanatoka katika kijiji kimoja.
Eneo la Hsiaolin lilikumbwa na maporomoko makubwa yaliyofunika nyumba zote isipokuwa mbili tu. Serikali inasema imekata tamaa ya kuwapata watu waliotoweka wakiwa hai.

Idadi rasmi ya watu waliokufa imefikia 118 lakini inahofiwa ikaongezeka zaidi.

Siku ya Ijumaa, jeshi limekuwa likitarajia kuwahamisha takribani watu 2,000 waliokwama katika maeneo hayo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kimbunga hicho kilisababisha mafuriko makubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 50.

Maeneo ya kati na kusini mwa Taiwan, barabara zimeteketezwa kabisa, madaraja kusombwa na maji na majengo kadhaa katika miinuko kusombwa na mito. Maeneo mengi ya vijiji vilivyo milimani yanaweza kufikiwa tu kwa njia ya anga.

Eneo la tukio

Mwandishi wa BBC Cindy Sui aliyeko Hsiaolin anasema: 'Nikiwa nimeona kwa macho yangu mwenyewe, hatimaye kwa sasa naelewa kwa kina maafa yanini hasa kilchotokea. Inaonekana kama ni eneo tambarare kabisa lisilokuwa na chochote kabisa - nyumba zote zimezolewa an daraja la urefu wa mita 17 lilikuwepo hapa haliwezi kuonekana tena'.

Zaidi ya watu 400 wamefunikwa na chini ya matope ya urefu wa kati ya mita 20 - 30 chini kabisa ardhini.

Serikali inasema haijui wapi pa kuanzia iwapo watafukua matope, kwani sio eneo imara kwa sasa kwasababu inaweza kusababisha upotevu wa maisha ya watu wengine zaidi.

Matope ni mengi sana kiasi cha kwamba hata waokozi wangalikuweko hapa, wasingeweza kuondoa au kufukua.

Mamia wanahofiwa kufa kutokana na kimbunga hicho cha Morakot, lakini serikali awali haikuweza kutoa idadi halisi ya watu wanaokadiriwa kufa.

Akizungumza katika mkutano wa usalama wa taifa siku ya Ijumaa, rais Ma Ying - jeou, alisema kuwa pamoja na vifo ambavyo tayari vimethibitishwa, ' na baadhi ya watu 380 wanahofiwa kufukiwa katika maporomoko katika kijiji cha Hsiaolin, ambapo kwa Taiwan idadi ya vifo inaweza kufikia zaidi ya 500''.

No comments:

Post a Comment