WATOTO NI ULIMWENGU WA UPENDO,UTULIVU NA AMANI.
KUTOKANA NA UWEZO WAO WA KUKUSANYIKA NA KUCHEZA BILA KUJALI JINA,RANGI,KABILA,JINSIA,UKOO,CHEO…..N.K.
UKITAZAMA MTOTO KWA MAKINI UTAONA PICHA YA UTUKUFU WA MUNGU. MTOTO HANA ADUI WA KUDUMU KATIKA KUNDI LA WATOTO WENZAKE. LAKINI MTOTO ANAWEZESHWA KUTENGENEZEWA ADUI NA MZAZI AU WAZAZI WAKE KUTOKANA NA CHUKI YAO JUU YA FAMILIA,UKOO,KABILA,RANGI……..N.K.
WAZAZI AU WALEZI WANAWEZA KUMFUNDISHA MTOTO WAO KUCHUKIA MTU AU WATU FULANI KUTOKANA NA UMASIKINI,TABIA MBAYA,DINI,UKOO,RANGI,KABILA…..N.K.
KWA UPANDE WA MTOTO HUONA JAMBO HILO NI KUNYIMWA HAKI YAKE YA KUCHANGIA MAWAZO NA VITENDO NA WENZAKE.
MTOTO MASIKINI,TAJIRI,KIWETE,MWEUPE,MWEUSI,MFUPI,MREFU……….UTAMKUTA AKICHEZA NA WENZIE BILA KUJALI KULA,KUNYWA,KUJICHAFUA…….N.K.
WATOTO WANA MFUMO WAO WA MAISHA YA KITOTO, NA HUWA NA MIPANGILIO YA MICHEZO HUSIKA. BAADHI YAO UTAKUTA WA KIPIKA,KURUKA KAMBA,KUTENGENEZA AU KUENDESHA GARI ZA MABOXI AU NYAYA NA WENGINE WAKICHEZA MICHEZO YA AINA MBALIMBALI.
MZAZI ANAPOMNYIMA MTOTO WAKE UHURU WA KUCHEZA NA WENZAKE, HUMWEKA KATIKA HALI YA MAWAZO MAKUBWA NA KUMPA (MTOTO ) CHANZO CHA KUJISHUGHULISHA NA MICHEZO YA WATU WAZIMA WALIOKO NDANI AU KATIKA ENEO HUSIKA. MTOTO ATAANZA KUSIKILIZA MAZUNGUMZO,KUANGALIA PICHA,……NK,VYENYE UWEZO MKUBWA ZAIDI YA UMRI WAKE. MATOKEO YAKE MZAZI AU WATU WATAANZA KUMSHANGAA MAONGEZI YAKE NA MATENDO YAKE, NAKUONGEA MENGI JUU YA MALEZI YA MTOTO HUSIKA.
MARANYINGINE MTOTO ANAWEZA KUWA NA TABIA ZA AJABU, NA WA ZAZI WA KAANZA KUMTAFUTA MCHAWI, KUMBE WACHAWI WAKUBWA NI WAO WENYEWE.
KWASABABU
WAMESHINDWA KUTAMBUA HAKI YA KUCHEZA JUU YA MTOTO WAO, NA MWISHOWE WANAJIKUTA WAKITENGENEZA MAZINGIRA YA KUMKUZA MTOTO WAO KIFIKIRA BILA WAO KUJITAMBUA.
NIVYEMA KILA MZAZI KUWA MAKINI KATIKA KUTAMBUA HAKI YA MTOTO WAO,ILI WAEPUKE KUWALANI NA KUTUMIA MANENO
( MATUSI ) NA VITENDO ( KIPIGO ) VISIVYO FAA.
NA NDIO MAANA YESU ( NABII ISA ) ALISEMA ATAKAEMPOKEA MTOTO AMEMPOKEA YEYE.
KWASABABU WATOTO HAWANA DHAMBI KABISA WALA HAWASEMI UONGO, ISIPOKUWA WAKIFUNDISHWA AU KUPEWA SILAHA YA UONGO.
MTOTO HUFUNDISHWA UONGO NA WATU WAZIMA ,KATIKA HARAKATI ZAKULINDA MASILAHI YAO.
MTU MZIMA ANAWEZA KUMWAMBIA AU KUMFUNDISHA MTOTO KUSEMA UONGO NA KUWA SHAHIDI JUU YAKE.
IKIWA UTAFANYA HIVYO TAYARI UMEMFUNDISHA MTOTO NJIA YA MADHARA YA UONGO.
KUNA BAADHI YA WAZAZI WANAOWAFUNDISHA WATOTO WAO KWAMBA, FULANI AKIJA MWAMBIENI MIMI SIPO?????????
HII SIO TABIA NZURI YA KUMFUNDISHA MWANAO AU MTOTO WA MWENZIO. KWABAADAE, ELIMU HIYO YA UONGO MTOTO ANAWEZA KUITUMIA KAMA SILAHA YA KUANGAMIZA UKWELI BAINA YAKE NA WATOTO WENZIE AU NA WAZAZI WAKE.
MTOTO ATAKUWA NAYO NA ANAWEZA KUITUMIA AU KUWAFUNDISHA WATOTO WENZIE NA KUSABABISHA KIPIGO JUU YAO.
TUWAPENDE WATOTO NA TUJITAHIDI SOTE KUJALI SHERIA ZAO ZA MICHEZO KATIKA HALI NA MAZINGATIO YENYE MIPAKA SALAMA.
UTOTO NI NJIA YAKILA BINAADAMU ISIPOKUWA BABA YETU SOTE
( ADAMU ) NA MAMA YETU SOTE ( HAWA ) HAWAKUWEZA KUPITIA NJIA YA UTOTO AU KUZALIWA AU KUMWITA MTU YEYOTE BABA AU MAMA.
KWASABABU ADAMU NA HAWA HAWANA BABA WALA MAMA WALA BABU WALA SHANGAZI WALA KAKA WALA DADA……N.K.
YOTE HAYO YALITOKANA NA UWEZO WAKE MWENYEZI MUNGU MUUMBA WA VYOTE KWA MAPENZI YAKE.
No comments:
Post a Comment