KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, July 10, 2009
SIMBA MLA WATU.
SIMBA NI MNYAMA MWENYE NGUVU NA MWENYE KUPENDEZA SANA MACHONI MWA BINADAMU WENGI. SIMBA NI NEMBO YA MNYAMA MWENYE NGUVU AFRICA.CHAKULA CHA SIMBA NI NYAMA NA ANAPOKULA HULA NUSU YA UZITO WAKE. SIMBA ANAKULA MARA MOJA KWA SIKU TANO AU SITA. SIMBA MWENYE JINSIA YA KIKE, NDIO WAWINDAJI WAKUBWA NA WATUZAJI WA WATOTO WAO.
LICHA YA KUWA SIMBA NI MNYAMA MZURI NA WAKUPENDEZA ANAWEZA KUWA HATARI JUU YA MAISHA YA BINAADAMU.
MIBUYU SABA NA HISTORIA YA SIMBA MLA WATU
HII NI HISTORIA AMBAYO WAKAZI WA SELOUS (MIBUYUSABA ) HAWAWEZI KUISAHAU. SIMBA ALIWEZA KUINGIA KATIKA MAKAZI YAO NA AKAWEZA KUWALA AU KUWAUA WATU ZAIDI YA 39 NA WENGINE KUWAJERUHI.
WAKAZI WA MIBUYU SABA BAADHI YAO WALIACHWA YATIMA,WAJANE……..N.K
MAISHANI MNA MAMBO MENGI YANAYO HITAJI ELIMU YA KUTOSHA, ILI TUWEZE KUKABILIANA NAYO.
WAKAZI HAO WALIOMBA MSAADA WANGUVU KUTOKA SEREKALINI NA WAKAPEWA UWEZO HUO ULIOWAWEZESHA KUMWUA YULE SIMBA. NA BAADA YA KIFO CHA YULE SIMBA KILA MKAZI ALIHAKIKISHA YA KWAMBA ANAKATA KIPANDE CHA NYAMA YA SIMBA NA KUKILA KIKIWA KIBICHI NA WENGINE WAKICHOMA NYAMA NAWENGINE WAKITAZAMA MZOGA WA YULE SIMBA MLAWATU KWA HASIRA.
KILA HALI KATIKA MAISHA NI FUNDISHO KWA WALE WALIOBAKI.
SIMBA NI MNYAMA MZURI LAKINI ANAWEZA KUWA HATARI KWA BINAADAMU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment