KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, June 28, 2009

Wamarekani wajiandaa kuondoka Iraq



Jummanne ni tarehe ya mwisho ya vikosi vya Marekani kuondoka miji ya Iraq
Hatua za ziada za kiusalama zinaimarishwa nchini Iraq, siku tatu kabla ya tarehe ya mwisho ya vikosi vya vikosi vya Marekani kuondoka kutoka sehemu za miji nchini humo, siku ya jumaanne.
Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya mabomu kadiri siku hiyo inavyokaribia, na kuna hofu za mashambulizi zaidi yakilenga kuchochea chuki za kidini.

Waziri mkuu Nouri al Maliki ametoa wito wa kuwepo umoja wa kitaifa, huku tishio la mashambulizi hayo likiendelea kuwepo.

Maafisa wote wa Polisi wameagizwa kufuta likizo zao , na wanajeshi wa usalama wa ziada wameandikishwa kujaribu kuzuia ghasia zaidi huku tarehe hiyo ikiendelea kukaribia.

Ulinzi zaidi umeimarishwa katika mapito ya kuingia kwenye masoko kwa sababu yamekuwa yakilengwa na wanamgambo wakitaka kuuwa watu wengi iwezekanavyo.

Mashambulizi mengi yanalenga maeneo ya waumini wa madhehebu ya kishia na sehemu za kufanyia ibada.

Waziri mkuu Nouri Al Maliki amewalaumu wapiganaji wa Kisunni kutoka Al Qaeda na makundi mengine yenye uhusiano nao akisema yanajaribu kuanzisha tena chuki za kidini.

Ametoa wito kwa watu kuungana na kuonyesha mshikamano wa kitaifa dhidi ya uchokozi wa aina hiyo na akaelezea ana imani kwamba vikosi vya usalama vya Iraq vitaweza kuthibiti hali vikosi vya Marekani vinapoondoka.

Vikosi vya Marekani tayari vimeondoka kutoka vituo vingi vyao katika miji kama vile Baghdad lakini viko nje kidogo tu ya miji muhimu, ambako viko tayari kuingilia endapo vikosi vya Iraq vitaitisha msaada.

No comments:

Post a Comment