KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 26, 2009

Tanzania imekuwa ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo la mauaji ya albino














Tanzania imekuwa ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo la mauaji ya albino, ambalo limesababisha mauaji ya watu wasiopungua 45 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Vitendo vya mauaji ya albino vimeenea zaidi katika maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria. Uovu huo umejikita katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera.


Bonyeza hapa kumfuatilia Vicky Ntetema katika blogu yake

Maeneo hayo ya historia ya kisirani cha kuwaua vikongwe katika miaka ya 1970, hasa kutokana na macho yao mekundu.

Mapema mwaka 2008, mwandishi Vicky Ntetema wa BBC alianza uchunguzi kudadisi kiini cha mauaji ya albino katika maeneo hayo ya Ziwa Victoria.

Ilikuwa safari ndefu, nyeti, yenye utelezi na hatari huku ikihitaji subira na ujasiri. Siku baada ya siku, Vicky alikutana na wahusika mbalimbali katika biashara hiyo ya kiza.

Kwa taarifa za kina, ukitaka kujua wanaohusika na mauaji ya albino, basi soma blogu ya Vicky Ntetema. Unapewa fursa ya kuchangia mada kwa kutoa maoni.

No comments:

Post a Comment