KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, May 24, 2009

Pakistan yadai Taliban wanazidiwa






















Forcing America into the 1991 Gulf War, the Afghanistan War, and now the Iraq War to
reconfigure the Middle East and establish a war-profiteering nightmare, resulting in 4,000 American soldiers being killed along with an uncounted number of Afghani and Iraqi civilians














Jeshi la Pakistan linasema kuwa limefanikiwa kuyadhibiti tena maeneo kadhaa ya Mingora, mji mkuu katika bonde la Swat, wakati mashambulio dhidi ya wanamgambo wa Taliban yakiendelea.
Afisa mmoja wa usalama amesema wanajeshi sasa wanafanya kazi ya kutegue mabomu ya ardhini katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali.

Lakini mapigano bado yanaendelea huku wanajeshi na wanamgambo wakiwa katika makabiliano ya uso kwa uso kwenye baadhi ya njia panda kuu za mji huo, kwa mujibu wa taarifa za jeshi.

Haja ya ushindi
Mapigano yalianza baada ya amani kuvurugika mapema mwezi huu. Mamia ya watu wameuawa na wengine zaidi ya milioni moja wamekimbia makazi yao katika eneo la Swat tangu kuanza kwa mapambano ya kuwasaka wanamgambo wa Taliban.

Mafanikio ya jeshi la Pakistan yanategemea ushindi wa kutosha katika eneo la Mingora, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC aliyeko Islamabad.

Mashambulio hayo mapya dhidi ya Taliban yanaungwa mkono kikamilifu na Marekani, ambayo imebainisha kuwa Pakistan na Afghanistan ndiyo maficho makuu ya mapambano ya ugaidi wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment