KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, May 22, 2009

Mheshimiwa Raisi na jitihada za maendeleo ya nchi yetu

Hizi ni baadhi ya harakati mbalimbali za Raisi wetu akiwa nje ya nchi yetu katika kututafutia maendeleo ya sekta mbalimbali za kijamii. Akiwa kama mpatanishi(katika migogoro kama Kenya, Komoro,rwanda na burundi, kongo darfur...nk) hili ni jambo la pongezi sana, raisi wa umoja wa afrika(mstaafu) ameweza kutuletea mabadiliko makubwa katika kuhakikisha nasi tunapata exposure kwa watu na taasisi mbalimbali za nje ya mipaka yetu. Na hivi karibuni alikuwa nchini Marekani akikutana na wataalamu wa maswala ya habari na teknolojia za kompyuta na kuwashawishi kuja kuwekeza katika nchi yetu, hili ni jambo la msingi tukizingatia ya kwamba maendeleo haya ni muhimu kwa kipindi hiki cha sasa cha sayansi na teknolojia! pia ameweza kwenda mashariki ya kati na asia ili kuweka mahusiano muhimu kwa maendeleo ya sekta mbalimbali.









































































Maendeleo haya ni kwetu sote kwani kwa kuwezeshwa kiteknolojia sote tutaweza pata huduma muhimu za mawasiliano kwa uhakika na ufanisi zaidi, na pia khali hii itatoa fursa za kazi kwa watanzania mbalimbali watakaokuwa waajiriwa wa miradi mbalimbali itakayoletwa na wawekezaji kutoka nje. Kwa haya tunampongeza sana raisi wetu na kumtakia kila la kheri katika harkati zake za kutuletea maendeleo katika nyanja mbalimbali za kimaisha!
Hongera Mheshimiwa raisi wetu na Mungu akujalie Kheri na Baraka Tele!Mungu ibariki Tanzania! Mungu ibariki Africa!

No comments:

Post a Comment