KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 28, 2012

Nigeria imesitisha safari zake za ndege za Mahujaji

Mzozo kuhusu Hajj watokota Nigeria imesitisha safari zake za ndege za Mahujaji
ji Saudi Arabia baada ya nchi hiyo kuwarejesha zaidi ya wanawake mia moja na sabini waliowasili huko bila kufuatana na wanaume. Spika wa Bunge nchini humo ataongoza Ujumbe kwenda Saudi Arabia kulalamika rasmi kwa jinsi Mahujaji wake walivyotendewa. Taarifa zinazohusianakesi Mwanamke mmoja kati ya hao waliorejeshwa ameiambia BBC kuwa wakati wakiwa kizuizini hawakupewa chakula. Hapo awali, bunge la Nigeria lilitoa wito kwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan kuwasiliana na mfalme wa Saudia, Abdullah kujaribu kumaliza mzozo uliozuka kati ya nchi hizo mbili kufuatia sakata ya Hajj. Serikali ya Saudia iliwarejesha nyumbani zaidi ya wanawake miamoja na sabini ambao waliwasili nchini humo waliokwenda Hajj bila (Mahram) au mwanaume ambaye ni jamaa yake au mume wake Wanawake wengine elfu moja wamezuiliwa hadi watakaporejeshwa nyumbani kwao. Saudi Arabia imekuwa ikielezea wasiwasi kuhusu waafrika wanaokwenda nchini humo na kusalia huko baada ya kuhiji na hivyo kujiweka katika hali ya kuombaomba au hata kujiingiza katika biashara ya ukahaba.

No comments:

Post a Comment