KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, August 1, 2012

Uingereza ina majeshi ndani Somalia

Serikali ya Uingereza kwa mara ya kwanza imethibitisha kuwa ina kikosi maalum cha jeshi ndani ya Somalia. Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba katika makao makuu wa jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia kuna washauri 10 wa kijeshi toka Uingereza. Taarifa zinazohusiana Afrika, alshabab, Somalia Jeshi hilo la Umoja wa Afrika limekuwa ndani ya Somalia likipambana na wapiganaji wa Al shabaab ambao wanadhibiti maeneo mengi nchini Somaia lakini mwandishi wa BBC amesema kuwa baadhi ya maafisa hao wanaosemekana kuwa ni washauri wameonekana maeneo ya Afgoye ambao hivi majuzi ulutekwa kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab. Kundi la al-Shabab ambalo mapema mwaka huu lilijiunga na al-Qaeda linadhibiti maeneo mengi nchi Somalia.##mengi ya maeneo hayo yako Kusini na katikati mwa Somalia. Hata hivuo Al shabaab kwa wakati huu wamebanwa kutoka pande zote

No comments:

Post a Comment