KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 13, 2012

Serikali ya Uingereza imeeleza shuruti zinazofaa kutekelezwa kabla ya kuanza tena kuipa Rwanda msaada

Serikali ya Uingereza imeeleza shuruti zinazofaa kutekelezwa kabla ya kuanza tena kuipa Rwanda msaada, moja kati ya nchi rafiki wa Uingereza kwenye maswala ya maendeleo
Akizungumza na BBC, Waziri wa Maendeleo wa Uingereza, Andrew Mitchell, alisema anataraji serikali ya Rwanda itashirikiana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye ni mwenyekiti wa mazungumzo kuhusu msuko-suko wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo. Bwana Mitchell alisema Rwanda inatakiwa kueleza msimamo wake kuhusu ghasia za Congo, zilizosababishwa na wapiganaji wa kundi la M23 - kundi ambalo serikali ya Rwanda inatuhumiwa kulisaidia. Serikali ya Kigali imekanusha mara kadha kuwa ina uhusiano na wapiganaji hao. Mwezi uliopita, Uingereza ilitangaza kuwa inaahirisha msaada kwa Rwanda hadi shuruti fulani zitekelezwe.

No comments:

Post a Comment