KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, May 13, 2012

KWA NINI, NIMPENDE MAMA MZAZI MAISHANI?

UPENDO NI KIFAA CHENYE KITUO MOYONI MWA NAFSI. KAZIKUBWA YA UPENDO, NI KUHIFADHI MAPENZI YA NAFSI NDANI YA MOYO WAKE. MAPENZI YA NAFSI YANAJENGWA NA MSINGI MZURI WA MANENO NA MATENDO YA MTU HUSIKA.
MAMA MZAZI ANACHUKUWA NAFASI KUBWA SANA KATIKA ULINZI WA MAISHA YANGU. KUNA DALILI NYINGI ZENYE KUONESHA UMUHIMU WA MAMA MZAZI. BAADHI YA DALILI HIZO, MOJAWAPO NI : KUKUBALI(MAMA) KUPOKEA MBEGU YA MAISHA YANGU, NA KUIHIFADHI (MBEGU YA UHAI) KWA MUDA WA MIEZI TISA. MAMA MZAZI ALIWEZA KUHIMILI MAMBO MENGI, MOJAWAPO NI KUTAPIKA, KUPUNGUA KWA NGUVU MWILINI MWAKE, ALIWEZA KUVUMILIA HASIRA KATIKA WAKATI MGUMU WA MIMBA YANGU, LAKINI NILIPOZALIWA YOTE ALIYASAHAU, AKAFURAHI ZAIDI YA WATU WOTE NA AKAMSHUKURU MUUMBA KWA UWEZO WAKE JUU YAKUZALIWA KWANGU. MAMA UNA HAKI YA KUNIONGOZA KATIKA MSINGI WA MAISHA BORA MAISHANI MWANGU. KUNILISHA NA KUNINYWESHA NDANI YA HIFADHI YANGU TUMBONI MWAKO NA KUNILINDA JAMBO BAYA KATIKA MUDA WAKO WA KUBEBA MIMBA YANGU, NDIO MAANA NASEMA NAKUPENDA MAMA. MAMA ULIWEZA KUVUMILIA TAABU YA KUBEBA MIMBA NA KUJINYIMA MENGI MAZURI KATIKA MUDA WA MAISHA YANGU YA TUMBONI, NA UKAWEZA KUHIMILI NA KUVUMILIA KATIKA MUDA WAKO WA KUJIFUNGUA (KUTOA NAFSI YANGU KATIKA TUMBO LAKO KWA HAKI NA SALAMA). UVUMILIVU KATIKA MACHUNGU YA KUJIFUNGUWA UHAI WANGU, LICHA YA MAUMIVU KUYAPATA NA KUKUTESA KWA MUDA, BAADA YA KUHISI KUTOKA KWANGU, TUMBONI MWAKO, ULITAMANI KWA HARAKA KUANGALIA SURA YANGU, KISHA UKATABASAMU KATIKA MSINGI WA KUMSHUKURU MUUMBA WA WOTE. YALE MACHUNGU YALIOKUPATA YALISITA, NA UKAENDELEA KUWA KARIBU NAMI KATIKA MSINGI WA TAHADHARI(ULINZI WA NJAA NA MAUMIVU MENGINE). MWANZO ULIKUWA UKILALA USINGIZI KWA RAHA ZAKO, LAKINI ULIPOBEBA MIMBA YANGU NA KUJIFUNGUWA(KUZALWA KWANGU) , ULIPATA SHIDA SANA YA USINGIZI NA UTULIVU WA KUFANYA MAMBO YAKO, KISA UNAVUMILIA KELELE YA MLIO WANGU, KATIKA MFUMO WA KUKUKERA, LAKINI ULIVUMILIA YOTE NA MARANYINGINE UKIBUNI NYIMBO ZA KUNIBEMBELEZA ILI NILE, KULALA AU KUNYAMANZA, NDIO MAANA NASEMA ASANTE MAMA.
NNAMENGI YA KUTAJA KUHUSU MAMA MZAZI LAKINI KUYAMALIZA SIO RAHISI KUYAKUMBUKA NA KUYAMALIZA. MAMA ALIWEZA KUPUNGUZA MUDA WAKE WA USINGIZI, KULA NA KUNYWA VIZURI, KWASABABU YA ULINZI WA MAISHA YANGU.

No comments:

Post a Comment