KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 26, 2012

UHALISIA WAKITU UNATOKANA NA MAZINGIRA YAKE KWA WAKATI HUSIKA.

UHALISIA WAKITU UNATOKANA NA MAZINGIRA YAKE KWA WAKATI HUSIKA.




Mfano:
Ukipenda inamaana utakuwa katika mazingira yenye haja ya kupendwa, na tayari upondani ya ukumbi wa mapenzi.
Mapenzi ni kifaa chenye uwezo wa kumbadilisha binaadamu, wanyama…………… na kuwaingiza katika mfumo wa mabadiliko ya utii kwa vipenzi vyao au wapenzi wao.



Mfano:
Lazima utapokutana na Yule umpendae, utajihisi kuwa mwenye faraja na mwili wako kuingia katika wakati wa mapumziko ya maumivu ya nafsi (muungano wa roho na mwili).


UHALISIA WA KUPENDWA MAISHANI



Uhalisia wa kupendwa maishani ni kuwa na mpenzi mwenye dhati ya mapenzi juu yako.

Mfano:





Unaonaje! Ukiambiwa neno namtu”nakupenda kwa dhati ya moyo wangu”? kwa ukweli maneno haya yatakushangaza na maranyingine unaweza kuwa na uhuru wa kuyakubali ama kuyakataa.


Kwanini?


Kwasababu kila mtu anakuwa huru katika kuamuwa kukupenda ama kutokupenda. Jambo hilo linatokana na chaguo la moyo. Chaguo la moyo katika kupenda au kupendwa linatokana na kuridhishwa na matendo, maneno, hisia na muonekano wa nafsi baina ya nafsi mbili zenye mada husika.



Kukumbuka kwamba unaweza kumpenda mtu, kutokana na mavazi, umbo na matendo yake. Ustarabu unatokana na kuishi katika mazingira yenye kukupa utulivu na kuleta amani katika jamii. Lazima ukubali kwamba unapoombakitu si lazima upewe kutokana nakosa hili, watu wengi wamejikuta katika utata wa kulazimisha penzi kwa maneno, vitisho ama kwa zawadi.



Hakuna upendo wa kufosiwa (kulazimishwa), bali upendo unatokana na maridhiano yaliopo baina ya nafsi mbili zinazopendana maishani. Ukilazimisha penzi mwisho wa siku utajikuta ukiishi kwa malalamiko ya kusalitiwa. Kusalitiwa kunatokana na upungufu wa faida ya nafsi inayo kusaliti. Kuwa huru katika kumchagua mpenzi wala usilazimishe penzi, usije ukajikuta katika utata wa maumivu ya kusalitiwa baadae.





Mfano:

Kila mtu anafuata maslahi ya nafsi yake maishani.

UKIWA HAI UTAPENDWA KUTOKANA NA FAIDA ULIONAYO



Huwezi kujua kupenda ama kupendwa bila kuwa hai, lazima uwe hai ili uweze kushuhudia ulimwengu wa kupenda na kupendwa maishani. Huwezi kumpenda mtu bila faida juu yake, lazima faida iwepo.





Mfano:

Unaweza kupenda kutokana na maneno, matendo, umbo au hisia juu ya yule unaemtamani. Unaweza kumtamani mtu kutokana na anavyo vaa, anavyotembea, matendo yake katika jamii, uaminifu ama hisia yako, unapokuwa nae.
AKILI NA NGUVU YAKO NDIO MUONGOZO WA MAISHA BORA
Akili ni kiungo ambacho kinamwezesha binadamu kutambua UMUHIMU, FAIDA NA HASARA ya jambo Fulani. Ili Akili iwe salama na kuishi katika mtiririko mzuri wa maisha, lazima akili iwe imara. Uimara wa akili unatokana na utulivu wa moyo na mwili kisha fanya mazoezi kula vizuri na uhakikishe unakunywa kinywaji salama. Utakapo fanya hivyo utaingia katika kundi la kujiimarisha kinafsi. Uimara wa nafsi (muungano wa roho na mwili) unatokana na uimara wa akili maishani. Ukiwa na akili timamu na yenye elimu ya kutosha juu ya kila jambo lenye faida, lazima utaona kwamba

UHALISIA WA KUPENDWA UNATOKANA NA UHAI WAKO MAISHANI.



KIFO CHAKO NI MKATE WA MWENZIO

Mfano:

ukifa lazima ofisi yako imtafute mtu mwingine azipe pengo lako.
AKUPENDAE HUONESHA DALILI UKIWA HAI
Mfano:
Maiti inapozikwa haizikwi na mtu mwingine ambae yuko hai, bali mke/mme, ndugu jamaa na marafiki hurudi nyumbani kwa masikitiko makubwa. Na kuanza kujiuliza mengi kuhusu dunia bila wewe.

NINGELIJUA HANA MSAADA KWAKO

Mfano: kujua kunatokana na ujuzi ulionao juu ya jambo husika. Upungufu wa elimu juu ya lile ulifanyalo ndio njia ya masikitiko kama “ningelijua nisingemuamini au kufanya au kurudia……)!?

Maishani
BY: Ismado (ismail)

No comments:

Post a Comment