KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, June 6, 2011

Spika wa Nigeria nguvuni





Dimeji Bankole

Mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Nigeria amekamatwa na polisi wa kupambana na ufisadi.

Spika wa bunge la wawakilishi linalomaliza muda wake Dimeji Bankole alizuiliwa kuhusiana na madai ya ubadhilifu wa mamilioni ya dola,fedha za serikali.

Alikamatwa baada ya makao yake katika mji mkuu Abuja kuzingirwa.
Atakamatwa

Alipoapishwa kuchukua madaraka wiki iliyopita, Rais Goodluck Jonathan aliahidi kukabiliana ufisadi uliokita mizizi nchini Nigeria.

Mwandishi wa BBC Jonah Fisher anasema kukamatwa kwa Bw Bankole si suala ambalo halikutarajiwa, baada ya wiki kadhaa za tetesi zilizochapishwa katika magazeti ya nchi hiyo kwamba atakamatwa.

Msemaji wa tume ya kukabiliana na uhalifu wa kiuchumi na kifedha nchini humo(EFCC),alisema kuwa tume hiyo ilipokea taarifa kwamba Bw Bankole alikuwa akipanga kutoroka nchini.
Shutma

Sawa na wabunge wengine, muhula wa Bw Bankole unamalizika Ijumaa- na bunge jipya linatarajiwa kuapishwa Jumatatu.

Alipoteza kiti chake katika uchaguzi wa mwezi Aprili.

taarifa ya EFCC inasema Bw Bankole anatafutwa kujibu shutma zinazomkabili.

Miongoni mwa shutma hizo ni pamoja na matumizi mabaya ya dola milioni 60, na kuchukua dola milioni 65 kama mkopo binafsi akitumia akaunti ya bunge kama dhamana.

Awali msemaji wa Bankole Idowu Bakare, alitoa taarifa akisema kuwa "hakuwahi kunufaika" kwa kutumia nafasi yake. Liliripoti shirika la habari la AP.








Gharama za chanjo kupungua







Dawa

Chanjo kupungua bei

Kampuni kadhaa za kutengeneza dawa zimetangaza kupunguza bei za chanjo muhimu za magonjwa katika mataifa yanayoendelea.

Chanjo hizo zilizopunguzwa bei zinanuiwa kukinga na kutibu magonjwa ya kuhara na kupatika, kichomi , kifua kikuu na magonjwa mengine.

Mpango huo utasaidia shirika la kimataifa linalohusika na chanjo za tiba na elimu ya kukinga maradhi GAVI kufikia malengo yake, ya kutoa dawa kwa mamilioni ya watoto wanaokabiliwa na tisho la kuangamia kutokana na maradhi.
Malengo ya Milenia


Moja ya malengo ya milenia ya Umoja wa Mataifa, ni kupunguza vifo vya watoto wadogo kwa asilimia 60 ifikiapo mwaka wa 2015.

Lakini hii itategemea kujitolea kwa shirika la kimataifa, GAVI, linalohusika na kutoa chanjo na elimu ya kukinga maradhi kwa watoto milioni ishirini na nne kote duniani ambao hawajapata chanjo yoyote.
Faida

Inakadiriwa kuwa watoto milioni 9 walio na umri wa chini ya miaka mitano hufa kila mwaka kutokana na magonjwa ambayo yangezuiwa kwa kutumia Chanjo.

Gharama ya juu ya chanjo hiyo ni kizingiti kikubwa katika harakati za kutibu magonjwa hayo, na shirika la Gavi amabalo pia hushughulika na kununua dawa zitakazo tumika katika mataifa masikini, linakabiliwa na upungufu wa karibu dola bilioni 4

Na tangazo la kutoka kwa kampuni za kutengeneza dawa kuwa zitapunguza bei ya chanjo hiyo kwa hadi asilimia 75 kwa mataifa yanayostawi ni afueni kwa shirika hilo.






Jaji awashangaa washukiwa Kenya





Mahakama


Mahakama ya Uingereza


Mahakama kuu ya Kenya imekataa ombi la mbunge mashuhuri nchini humo

Chris Okemo na aliyekuwa mkurugenzi Mkuu wa shirika la umeme la kitaifa Samwel Gichuru la kiuzuia serikali kuwakamata na kuwapeleka Uingereza kujibu mashtaka ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.

Jaji Nicholus Ombiji ameshangaa kwanini wawili hao wanababaika kwa kufika mahakamani wakati serikali ya Kenya yenyewe bado haijawasilisha kesi ya kuomba wakamatwe na kufikishwa katika mahakama ya visiwa vya Jersey nchini Uingereza.

Mahakama imemwambia Okemo ambaye wakati mmoja alikuwa waziri wa nishati na pia waziri wa fedha wa Kenya pamoja na mwenzake kwamba hawana uwezo wa kumzuia mkuu wa sheria nchini humo kuagiza wafikishwe mbele ya mahakama ya Uingereza ili kujibu mashtaka ya ufisadi.

Mahakama ya Jesey imetoa agizo la kukamatwa kwa Okemo na Gichuru na kufikishwa mbele yake kutokana na madai ya kupokea mamilioni ya pesa kwa kutumia nyadhifa zao serikalini wakati huo na kuzificha katika taasisi mbali mbali za kifedha Uingereza.






UN yachunguza mapigano Sudan




Umoja wa Mataifa umesema kuwa unafanyia uchunguzi mapigano yaliyozuka katika eneo linalozalisha mafuta katika jimbo la South Kordofan nchini Sudan.


Mwanajeshi wa UN Sudan.


Eneo hilo tete liko kaskazini mwa mpaka wa Sudan Kusini lakini linakaliwwa na watu wengi waliopigana kwa niaba ya Sudan kusini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2005.
Maswala nyeti


Hali ya wasiwasi imekuwa ikikumba eneo hilo wakati Sudan Kusini ikitazamiwa kujitangazia rasmi uhuru wake kutoka kaskazini kuanzia mwezi Julai.

Maswala nyeti katika mzozo huo yanajumuisha eneo kamili la mpaka kati ya kaskazini na kusini na mustakabal wa jimbo la Abyei linalozozaniwa.

Ramani ya Sudan

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa watu waliojihami kwa bunduki wamepora silaha kutoka katika kituo cha polisi cha Kadugli, katika mji mkuu wa jimbo la South Kordofan.

Saa chache baadaye kulitokea ufyatulianaji risasi katika kijiji kimoja kilichoko kilomita 48 kutoka mji wa Kadugli.

Haikubainika ikiwa matukio hayo mawili yalikuwa na uhusiano.


Jimbo la South Kordofan linadhibitiwa na serikali ya Khartoum lakini linakaliwa na wanajeshi wengi wanaoegemea upande wa kusini.







Aliyedai kubakwa Libya aenda Marekani






Eman al Obeidi

Mwanamke mmoja nchini Libya ambaye alisema amebakwa na wafuasi wa Kanali Muammar Gaddafi ameondoka magharibi mwa Libya kuelekea nchini Marekani Kwa mujibu wa dada yake.

Eman al-Obeidi alikuwa akitoka katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi hadi mjini Washington DC, alisema dada yake Marwa.

Eman al Obeidi



Aliomba ukimbizi huko, baada ya ya kutioka Libya, kupitia Tunisia.

Dada yake bi Obeidi, Marwa alisema shirika la kutetea haki za binadamu likisaidiwa na waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton lilikuwa limewaandalia Ema na baba yake ndege binafsi ambayo ingewapeleka mjini Washington, kupitia Malta na Austria.

Dada yangu amepitia mengi

Marwa

Pia alisema maafisa wa Qatar walikuwa wema kwa dada yake hadi saa chache kabla ya kumrejesha Libya.

"Tunataka tu fursa kwake ya kupatiwa matibabu ya kisaikolojia na apumzika" alilieleza shirika la habari la Associated Press. " dada yangu amepitia mengi "
alisema maafisa wa Qatar walikuwa wema kwa dada yake hadi saa chache kabla ya kumrejesha Libya.
Kutoroka


Wakati bi Obeidi akielezea taarifa yake kwa waandishi wa habari mwezi March, wafuasi wa serikali walimvuta na kumsukuma mbali.
Alipotea kwa siku kadhaa kabla ya kuonekana nchini Tunisia.

Bi Obeidi alisema alisaidiwa na askari walioasi kutoroka.



Unamfahamu Oprah Winfrey?

Oprah Winfrey, Rais Obama na mkewe Michelle



Moja ya vipindi vinavyotazamwa sana katika historia ya Marekani, The Oprah Winfrey Show, kinamalizika baada ya miaka 25. Kipindi chake kimegusa wengi na kuvuka mipaka ya televisheni.

Kipindi chake cha kwanza, kilichoitwa Namna ya Kumwoa au Kuolewa na mtu wa Chaguo lako, kilipendekezwa kiwe kipindi kinachorushwa mchana kama kipindi chengine chochote cha kawaida.

Lakini baada ya vipindi 4,560, watu maarufu kama Madonna, Beyonce na Tom Hanks wanatarajiwa kutokea kwenye kipindi chake cha mwisho cha kuagwa, kinachorushwa hewani siku ya Jumatano.

Wakati wa miaka hiyo 25, Winfrey limekuwa jina maarufu sana, anayekubalika na wengi na ni mmoja wa matajiri katika ulimwengu huu.

Akimaliza na kuendelea kufanya kazi katika televisheni yake mwenyewe, uwezo wa kupata wageni wanaovutia kwenye habari haliwezi kudharauliwa.

Mwezi huu, Rais Obama alizungumzia kwanini alihitaji kutoa cheti chake cha kuzaliwa hadharani.

Na Sarah Ferguson alizungumzia kwanini hakualikwa kwenye harusi ya kifalme Uingereza.

Kwahiyo ni namna gani ambavyo Winfrey ameweza kufanikiwa? Mambo 10 yanajumuisha ushawishi wake.ATOA MADAI YA KUDHALILISHWA KIJINSIA, 1986


Oprah Winfrey

Katika hatua yake ya kukiri ambapo baadae ikaja kuwa namna ambavyo anafanya kazi, Oprah aliwaambia watazamaji wake kuwa alibakwa alivyokuwa mtoto.

Si kwamba tu ilisababisha mwanzo wa kampeni isiyo rasmi kuhusu udhalilishaji, iliweka njia kwa msururu wa watu-maarufu wenye mtawaliwa, watu wa kawaida wenye mambo ya kueleza- kukaa kwenye kochi lake na kukiri.

Mwandishi wa vitabu Bonnie Greer, aliyeondoka kwao Chicago mwaka huo huo ambao Oprah alianza kupanda chati mjini humo, alisema: " Amefanya mawazo yaliyo ya wengi yakubalike kirahisi lakini anaielezea kama inamhusu moja kwa moja mwanamke wa Kimarekani mweusi.

"Imekuwepo siku nyingi katika utamaduni wa Kimarekani, lakini Oprah aliileta kwenye televisheni wakati wa mchana. Alianzisha utamaduni wa "mwathirika" kwa mantiki ya uzuri na ubaya.

"Aliingia wakati wa msukosuko wa uchumi katikam iaka ya mwisho ya 80 na mwanzo wa 90, jambo ambalo Wamarekani walitaka kuhakikishiwa: namna ya kuhimili na uzuri wetu.

"Oprah alizungumzia vitu kwa waliokuwa wakitazama vipindi vyake kwasababu alitaka kuonyesha 'uzuri' na 'uaminifu' yana malipo yake hapa duniani.
MKOKOTENI WA MAFUTA, 1988

Akiwa amevaa jeans ya saizi 10, Winfrey aliyekuwa mwembamba aliingia kwenye jukwaa wakati wa kipindi chake na mkokoteni wa mafuta kuonyesha namna alivyopoteza kilo 30 kwa kipindi cha miezi minne kwa kutokula kitu zaidi ya Optifast.

Lakini uzito ukaanza kurudi na ikawa mwanzo wa miongo miwili ya kupunguza kiwango cha kula na kupambana ili kukifanya kiuno kiwe kidogo.

Tim Teeman, mwandishi wa Marekani wa gazeti la Times, alisema: " Ikiwa Oprah atakumbukwa kwa lolote, basi ni umbo lake."

"Unaweza kusema haitoi ujumbe wa kweli lakini unatoa ujumbe sahihi. Jinsi Oprah alivyozungumzia uzito ni hali halisi ya namna watu mbalimbali wanavyopambana na uzito wao.
MICHAEL JACKSON ATOBOA, 1993

Idadi kubwa ya waliokuwa wakiangalia kipindi cha Winfrey illiongezeka alipomhoji Michael Jackson wakati umaarufu wake ulipozidi kupamba moto.

Takriban watazamaji milioni 62 walimwona ndani ya Neverland mtu aliyenaswa kwenye utoto wake, kabla ya madai ya kudhalilisha watoto kuibuka na kumharibia sifa yake.

Wakati wa mahojiano yaliyochukua dakika 90, alimwambia alikuwa akiumwa maradhi ya ngozi na alikana kuwa alilala kwenye chumba chenye gesi ya oksijeni.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michael kuzungumza kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka mingi na ilionekana kuwa jambo la kipekee kwa kipindi cha Winfrey, na kuandikwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali duniani na kusaidia kuimarisha sifa yake.
ELEN DEGENERES AJITOA HADHARANI, 1997

Mchekeshaji wa Marekani, mwendesha kipindi kwenye televisheni na muigizaji Ellen DeGeneres alisema hadharani kuwa anafuata mapenzi ya jinsia moja kwenye kipindi hicho.

Mahojiano hayo yalifungua mlango upya kwa kazi ya DeGeneres ambaye alianzisha kipindi chake mwenyewe cha mahojiano.

Mvuto wa Winfrey kwa wanawake wengine umejadiliwa sana.

Greer alisema, " Ni mtetezi wa wanawake kwa minajil ya kwamba amejenga milki yake mwenyewe na mfano wake umesababisha wanawake wengine kuiga."

"Ni wazi kwa hakika anakupa msukumo, hodari sana na mwerevu na amefanya mambo mazuri. Kila mmoja anamtakia kheri, pamoja na mimi.

Licha ya kukiri kuhusu masuala yake ya uzito na udhalilishaji, na uwezo wake wa kufanya wengine kama DeGeneres kuwa wazi, inashangaza namna ambavyo tunajua machache kuhusu Winfrey mwenyewe, alisema Greer.

" Kila mmoja aliye karibu yake hazungumzii mambo yake. Ni miongoni mwa watu maarufu Marekani ambao tunajua kila kitu na hatujui kitu vile vile.
TOM CRUISE JUU YA KOCHI, 2005

Huenda wakati utakaokumbukwa zaidi kwa Oprah ni pale Tom Cruise alipoanza kuchekacheka, akiruka juu na chini kwenye kochi lake alipoelezea penzi lake kwa mpenzi wake mpya, Katie Holmes, ambaye kwa sasa ni mke wake.

Teeman alisema tangu wakati huo tendo lake hilo limekuwa likifanyiwa dhihaka na kuigwa kwa kubezwa. Huu ni wakati ulioainisha kazi yake, baada ya filamu kama Top Gun, Cocktail au Mission Impossible.

"Oprah alionekana kumahanika, akifikiria 'Anafanya nini?' Kazi yake iliporomoka kwa muda lakini amerudi."

Watu maarufu hushiriki kipindi cha Oprah kuondosha pepo mbaya au kukiri jambo la kimapenzi, alisema, na wanajua hatowapa wakati mgumu.
JAMES FREY ALAANIWA, 2006

Moja ya ushawishi mkubwa aliokuwa nao Winfrey umekuwa katika ulimwengu wa uchapishaji vitabu, klabu yake ya vitabu imekuwa kisifiwa kwa kutengeneza mamilioni kwa waandishi ambao vitabu vyao hujadiliwa kwenye klabu yake.

Hakuna pahala ambapo ushawishi wake ulionekana kama katika kesi ya James Frey. Kitabu chake cha A Million Little Pieces, iliyoelezea hadithi yake ya kujikwamua kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, ambapo ilikuwa kitabu kilichouzwa kwa kiwango kikubwa baada ya kutokea kwenye kipindi chake.

Lakini mwaka 2006, baada ya kuwa na shaka na maisha yake aliyoyaeleza Frey, Winfrey alimwalika tena mwandishi huyo ili kumhoji, iliyosababisha mabishano makali na kuvua nguo hadharani kwa Frey.

Licha ya Winfrey kuelezea hivi karibuni kujuta kwa namna alivyolishughulikia suala hilo, alichojifunza si kukereka, alisema Teeman.

Kipindi chake ni kuhusu nia njema, na kitendo cha kusaliti uaminifu huo ni kuaibika.SHULE YA AFRIKA KUSINI YAFUNGULIWA, 2007


Oprah na wanafunzi Afrika Kusini

Shule ya uongozi ya Winfrey, karibu na Johannesburg, ilifunguliwa mwaka 2007 kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 40.

Aliahidi kujenga shule hiyo baada ya kukutana na aliyekuwa rais wa Afrika kusini Nelson Mandela mwaka 2002.

Winfrey mwenyewe aliwahoji wasichana wengi wa Afrika kusini waliotoka kwenye familia maskini walioomba nafasi 150 za mwanzo katika shule hiyo.

Mwaka jana, aliyekuwa matroni wa chuo hicho alifutiwa mashtaka ya kudhalilisha mabinti chuoni hapo.

Winfrey alieleza namna alivyosikitishwa wakati hukumu ilipotolewa lakini alisema anajivunia kwa namna wasichana hao walivyopata ujasiri wa kutoa ushahidi.

Ufadhili wake unajulikana, na wakfu wake wa Oprah Winfrey umechangia mamilioni ya dola kwa miradi Marekani na nchi za nje, huku shirika lake la ihsani Oprah's Angel limechanga kiasi cha dola za kimarekani milioni 80.
BARACK OBAMA, SI CLINTON, 2007

Katika mkutano Iowa mwaka 2007, Oprah Winfrey alimwuunga mkono Barack Obama ambaye kwa wakati huo alikuwa akigombea nafasi ya urais kupitia chama cha Democrat na Hillary Clinton.

Kuunga mkono kwake Winfrey kulionekana kuwa muhimu sana katika mpambano wa karibu wa nafasi hiyo kutokana na ushawishi mkubwa alionayo. Lakini chaguo lake liliacha maswali mengi.

" Alipomwuunga mkono Obama kwa nafasi ya urais watazamaji wake, ambao ni wanawake wazungu wa makamo, walikuwa wakimwuunga mkono Hillary Clinton na akakuta wengi wakimwacha mkono kwa kudhani anachagua asili au jamii yake kuliko jinsia yake. Alisema Eric Deggans, mkosoaji kupitia televisheni ya Petersburg Times huko Florida.

Umaarufu wake mkubwa ulitikisika kwenye jamii ya watu weusi alipokosoa muziki wa miondoko ya rap kwa mashairi yaliyo na chuki kwa wanawake.

Mara zote amekuwa akijiwakilisha kama mweusi lakini si kiais hicho cha kuwapoteza watazamaji walio wengi, alisema Deggens.

Lakini Winfrey ameonyesha, kama alivyofanya Bill Cosby kabla yake na Barack Obama baadae, kinachowezekana kwa Mmarekani mweusi.

"Kwa kufikia kiwango hicho kwenye televisheni, Oprah ameonyesha unaweza ukang'ara kama mtu mweusi.

"Amekuwa sauti ya wanawake weupe wa makamo kwa namna ambavyo haijawahi kufanywa na mtu yeyote, na kwa watu weusi kuona Mmarekani mweusi anakubalika kwa moyo mmoja ni muhimu sana."KUAGWA NA WATU MAARUFU, 2011


Tom Hanks akimuaga Oprah

Moja ya vipindi vya mwisho vya Oprah Winfrey huko Chicago uligeuka kuwa usiku uliojaa machozi, shukrani na watu mashuhuri kama vile Tom Cruise, Will Smith na Madonna.

" Jambo kuhusu Oprah ambalo linapendeza ni kwamba ameweza kuunda alama inayojumuisha utata mkubwa.

" Ni rafiki yako halisi ambao marafiki zake ni Julia Roberts na Tom Cruise. Ni kiongozi wa dini anayefanya kazi kupita kiasi na hufanya kipindi kwa mwaka kuhusu vitu vyote vya gharama anavyopenda.

"Ni kiongozi wa dini asiyechagua kanisa lipi aende. Ni mwanamke anayeteta wazazi wa kike na desturi za kifamilia lakini binfasi hana watoto."

Utata huu unavutia wanawake, alisema." Wanashukuru kwamba wanaweza kumwangalia Oprah na kuona mtu kama rafiki yao wa karibu lakini pia huwapa nafasi katika ulimwengu huu mzuri."






Jaji wa Mahakama nchini Serbia ametoa uamuzi kwamba kamanda wa majeshi ya Waserb wa Bosinia kwa afya yake anaweza kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya The Hague.



Amekuwa mafichoni kwa miaka 16 kabla ya kukamatwa kwake siku ya Alhamis.Lakini, Je watoro wanaotafutwa wa barani Afrika wako wapi? Na kwanini bado wanakimbia mkono wa sheria?


Bosco Ntaganda

Wengi kati ya wanaotafutwa ni wale inaodaiwa walihusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Kwa mfano mahakama ya jinai ya kimataifa kuhusu Rwanda ICTR ina orodha ya watu tisa .

Wa kwanza kabisa katika orodha hiyo ni Felicien Kabuga, ambae alikuwa ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Rwanda.

Upande wa mashtaka ulidai kwamba mnamo mwaka 1993 alinunua mapanga laki kadhaa, alikifadhili kikundi cha wanamgambo cha Interahamwe na kusaidia matangazo ya kituo cha redio kilichotumika kuchochea mauaji ya Watutsi.

Upande wa mashtaka unaamini kuwa Felicien Kabuga anajificha nchini Kenya, madai yanayokanushwa vikali na wakuu wa serikali ya Kenya.

Nchini Uhispania Jaji anayewakilisha familia za Wahispania watatu waliokuwa wakitumikia shirika moja la misaada la Hispania waliouawa nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa mauaji ya Rwanda anatamfuta Justus Majyambere na wengine 39.
Joseph Kony


Alikuwa ni mfuasi wa kundi la waasi wa Rwanda RPF chini ya rais wa sasa Paul Kagame, na anashutumiwa kuhusika na vitendo kadha vya jinai ikiwemo mauaji ya kimbari.

Justus Majyambere sasa anatumikia jeshi la taifa nchini Rwanda.

Mtoro mwingine anayetafutwa na mahakama ya jinai ya kimataifa kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu ni aliyekuwa kiongozi wa waasi Jean Bosco Ntaganda wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Serikali ya Congo imekataa kumtoa kwa sababu inasema ni mtu muhimu katika juhudi za kutafuta amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Yeye pia sasa ni afisa wa cheo cha Jenerali katika jeshi la taifa.

Nchini Uganda pia kuna mshukiwa wa uhalifu wa kivita. Yeye ni kiongozi wa kundi la Lords Resistance Army , Joseph Kony, ambae inadhaniwa yuko mafichoni katika mipaka ya Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kideokrasia ya Congo.

Anashutumiwa na mahakama ya jinai ya kimataifa kwa kuhusika na jinai katika vita, ikiwemo mauaji, chinjachinnja na kuzuia wanawake kwa minajili ya vitendo vya ngono.








Libya inashambulia helikopta za NATO






Helikopta za Uingereza zilizotumika kwa mara ya kwanza kurusha makombora dhidi ya sehemu za Libya zimeshambuliwa na jeshi la Kanali Gaddafi.
Mashua wanawaondoa wakimbizi kutoka lIbya


Mwandishi wa BBC kwenye manuwari ya jeshi la wanamaji la Uingereza, Royal Navy, katika pwani ya Libya, anasema helikopta mbili za aina ya Apache katika manuwari hiyo, zilishambulia kituo cha radar na kituo cha ukaguzi cha jeshi, karibu na mji wa Brega.


Helikopta hizo zilirudi kwenye manuwari salama na rubani mmoja alisema ametosheka na matokeo:


"Tumefurahi namna operesheni ilivotekelezwa.

Hizi helikopta zimeundwa hivo, zinakutumikia sawa-sawa na kukurudisha ardhini salama".

Helikopta za Ufaransa zilishiriki katika operesheni hiyo na kuzilenga shabaha nyengine.

NATO inasema inatumia helikopta kufanya mashambulizi, ili kuweza kuzuwia jeshi la serikali ya Libya kuwalenga raia wanaopigana nalo.









UN inataka msaada uruhusiwe Abyei





Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani kitendo cha serikali ya Sudan kuuteka mji wenye mzozo, wa Abyei, na kutaka wanajeshi waondoshwe huko.

Jeshi la Sudan, lilivamia eneo hilo baina ya mpaka wa Sudan Kaskazini na Kusini, na kufanya wakaazi maelfu kadha kukimbia.


Mbali ya kulaani kutekwa kwa Abyei na jeshi la Khartoum, taarifa piya inatoa wito kwa pande zote mbili kuruhusu msaada upelekwe kwa wale walioathirika na mapigano, na wakaazi waliohama waruhusiwe kurudi.

Maelfu ya wakaazi wa Abyei walikimbilia kusini, jeshi la serikali ya Sudan lilipouteka mji na kuuchoma moto na kupora mali.


Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wana wasi-wasi kuwa mapigano ya kuania Abyei, yanaweza kuzusha mapambano makubwa zaidi baina ya Kaskazini na Kusini, kabla ya uhuru wa Sudan Kusini tarehe 9 July.

Taarifa hiyo piya inalaani shambulio lilofanywa na Sudan Kusini dhidi ya askari wa Umoja wa Mataifa, waliokuwa wakiwasindikiza wanajeshi wa Kaskazini.

Serikali ya Sudan inasema hiyo ndiyo sababu ya kuchukua hatua ya kijeshi.

Baraza la Usalama linataka pande zote mbili zikubali jeshi la Umoja wa Mataifa libaki Abyei.






Amnesia International?




'Protecting the Human'? UN peacekeepers in Somalia, 1993.

Don't get me wrong. As NGOs go, Amnesty International does important and necessary work, highlighting human rights abuses around the world. However, does anyone else find its latest campaign to send UN Peacekeepers into Sudan slightly nauseating? This is their rational for sending in troops to stop the horrific killing that is currently going on:

'How can it be stopped?
Sudan must consent to an effective peacekeeping force. At the current time the best option is provided under UN Security Council Resolution 1706 which calls for the deployment of UN peacekeeping force with a strong mandate to protect civilians. Global pressure on governments to see this happens quickly must be continued.'

As a result, local groups of Amnesty in the UK have been really busy collecting petitions urging support for UN Peacekeepers, and even doing protests with placards reading 'Protect the Human - UN Peacekeepers Now'. What bothers me about all this is two things. Firstly, after the disasters of Iraq and Afghanistan, surely the last thing the world needs is Western troops occupying another Muslim country through force under the guise of 'humanitarianism'? Any foreign troops would inevitably be resisted by sections of the population of Sudan - quite legitimately - and so the violence and killing would not 'be stopped' but rather would likely continue. The record of UN interventions historically is appalling, from Somalia in 1993 where as the photo above shows, Belgian paratroopers committed appalling human rights abuses, to the forgotten bloody UN occupation of Haiti more recently. Put simply, UN troops are not the military wing of Amnesty International, as some seem to think, they are part of the military wing of capitalist globalisation.

Secondly, if Amnesty can take to the streets to protest for troops to go in to a country for 'humanitarian' reasons without being accused of being 'political', surely they can also now call for troops to come out of Iraq and Afghanistan? After all, Kofi Annan as Secretary General of the UN declared the Iraq war illegal - so why didn't the UK branch of Amnesty International affliate to the Stop the War Coalition and join the demonstrations before and during the war?





Wareno wapiga kura katika uchaguzi




Wagombea Coelho na Socrates

Wagombea Coelho na Socrates

Watu wa Ureno wanapiga kura katika uchaguzi ulioitshwa mapema, baada ya serikali ya kisoshalisti, kuomba mikopo kutoka vyombo vya fedha vya kimataifa, kusaidia uchumi wa nchi hiyo.

Kampeni ya uchaguzi imegubikwa na sera za kukata matumizi na kuzidisha kodi, shuruti iliyopewa Urenu ili kupata msaada.

Kura za maoni zinaonesha mashindano ni makali baina ya chama tawala cha kisoshalisti, na cha mrengo wa kati, cha Social Democrats.

Mwandishi wa BBC, anasema yeyote atayeshinda uchaguzi, atakuwa na tatizo kubwa la kutekeleza sera hizo.







Waandamanaji wafyatuliwa risasi Golan




Waandamanaji mpakani mwa Syria na Israel

Waandamanaji mpakani mwa Syria na Israel

Wanajeshi wa Israel wamewafyatulia risasi waandamanaji wanaowaunga mkono Wapalestina, kuwazuwia wasivuke mpaka wa Syria, kuingia katika eneo la milima ya Golan, linalokaliwa na Israel.

Waandamanaji kadha walionekana wakibebwa; na kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa kama wanne wameuwawa.

Israel ilesema itazuwia maandamano hayo yasiwe kama yale yaliyotokea mwezi uliopita, ambapo watu zaidi ya 10 waliuwawa.

Leo ni siku ya kukumbuka kuanza kwa vita vya siku 6, vya mwaka wa 1967, ambapo Israel ililiteka eneo la Golan.







UKIMWI uligunduliwa mwaka 1981




HIV



Mwaka wa 1981, daktari mmoja wa California Marekani aliona vijana wa kiume watano, walioshiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wakiwa na ugonjwa usiokuwa wa kawaida.


Walikuwa na homa ya pneumonia na saratani ya ngozi.

Dakta Gottlieb hakujua kuwa ripoti zake, ndio zitakuwa historia ya kwanza kuandikwa juu ya ugonjwa ambao baadae utakuja kuwa janga kubwa la AIDS, au UKIMWI.

Virusi vya HIV viligundulikana miaka miwili baada ya ugunduzi huo wa Dakta Gottlieb.


Tena damu ikaweza kupimwa kama ina virusi vya HIV, na baadae zikapatikana dawa kadha za kudhibiti ugonjwa huo.

Umoja wa Mataifa unakisia kuwa tangu mwaka wa 1981, UKIMWI umeuwa watu milioni 30, na idadi kama hiyo hivi sasa wanaishi na virusi vya HIV.


Lakini juma lilopita, umoja huo uliripoti kuwa idadi ya watu wanaoambukizwa inapungua katika nchi kadha, lakini mamilioni ya wagonjwa bado hawapati dawa wanazohitaji.

Matabibu wanasema virusi vya HIV sasa wanavifahamu sawasawa, na wagonjwa wanaofululiza kula dawa kwa wakati, wanaweza kuishi karibu maisha ya kawaida.







Rais Saleh huenda atarudi Yemen

Afisa mmoja mwandamizi alisema atarudi nyumbani baada ya siku chache, lakini upinzani umeahidi kuwa watamzuwia, na kuna tetesi nyingi kuwa utawala wake wa miaka 30, pengine ndio umekwisha.



Waandamanaji wakisheherekea kuondoka kwa Rais Saleh

Maelfu ya Wayemen wanasherehekea kuondoka kwa Rais Saleh nchini.

Vijana wengi walisherehekea katika Medani ya Chuo Kikuu cha Sanaa, na wengine walitoka barabarani wakipepea bendera.

Lakini milio ya bunduki na miripuko ilisikika.

Piya kuna taarifa kutoka Taiz kuwa mapambano yamezuka, na watu kadha wameuwawa.

Waliyemuona Rais Saleh Saudi Arabia, wanasema Rais Saleh aliteremka mwenyewe kwenye ndege lakini majaraha ya kichwani, usoni, na shingoni yakionekana.



Rais Ali Abdullah Saleh

Rais Ali Abdullah Saleh alijeruhiwa katika shambulio la kombora dhidi ya ikulu, ambapo rais na baadhi ya maafisa wake walijeruhiwa.

Rais Saleh, akifuatana na jamaa zake, aliwasili Saudi Arabi usiku wa Jumamosi.

Lakini mwanawe wa kiume na mpwa wake, ambao wanaongoza jeshi, inaarifiwa wamebaki nchini, na hao ndio walioisaidia Marekani kupambana na ugaidi nchini Yemen.

Rais Saleh alijeruhiwa chini ya moyo katika shambulio la kombora siku ya Ijumaa.


msikiti katika ikulu ya Rais Saleh ulioharibika katika shambulio la Ijumaa.

Maafisa wa serikali wamewalaumu watu wa makabila yenye silaha, wanaoshirikiana na wapinzani wa rais, kwa shambulio hilo, lakini makabila hayo yamekanusha kuwa yalihusika.

Mdadisi mmoja aliye karibu na Rais Saleh, anaona shambulio la Ijumaa lilitokana na bomu lilotegwa na mtu kati ya watu wanaomzunguka rais, lakini ni shida kuthibitisha hayo.

Swala ni jee, Rais Saleh, ambaye ameongoza nchi kwa miaka 3

3, ndiyo ameondoka kabisa, au atarudi?.

No comments:

Post a Comment