KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, April 12, 2011
Mkutano kujadili Libya waanza Qatar
Kwa mara ya kwanza waasi wanaotaka kumpindua Kanali Gaddafi
wanajitokeza katika ngazi ya kibalozi na watakutana na na tume maalum iliyoundwa hivi punde inayohusika moja kwa moja na masuala la Libya.
Masuala yanayojadiliwa ni pamoja na kuwapa msaada wa kisiasa, kijeshi na fedha waasi hao pamoja na kuelezewa mchango wa Nato.
Kabla ya mkutano huo, Mawaziri wa Ufaransa na Uingereza walidokezea kuwa wangependa kuona Nato ikijitahidi zaidi kuitenga serikali ya Kanali Gaddafi.
Tume maaulm iliundwa kwenye mkutano wa Mawaziri mjini London tareh 29 Machi na ina wajumbe kutoka Mataifa makuu ya Ulaya, Marekani, Mataifa washirika kutoka Mashariki ya kati pamoja na mashirika kadhaa ya Kimataifa.
Akiwa njiani kuelekea mkutano huo wa Qatar, Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza William Hague ameiambia BBC kuwa itabidi shinikizo zaidi za kijeshi na kisiasa dhidi ya Kanali Gaddafi.
Mkutano Qatar kujadili Libya
Ufaransa na Uingereza zinataka mataifa wanachama wa Nato
kutoa ndege zaidi za kijeshi kwa shughuli ya Libya ambapo Waziri wa Ufaransa wa mashauri ya kigeni,Allain Juppe alisema siku ya jumanne kuwa juhudi za Nato hadi sasa hazitoshi.
Msemaji wa Wizara ya mashauri ya kigeni wa Italy Maurizio Massari amesema kua
''suala la kuwapa silaha waasi lipo kwenye agenda bila shaka''.
Hadi sasa mashambulizi ya anga bado yameshindwa kubadili hali ya mambo kwenye medani ya vita.
Mkuu wa operesheni za Nato nchini Libya Brigadier Generali Mark Van Uhm
amesema kuwa anahisi kuwa Nato inajitahidi ''ikizingatiwa zana ilizo nazo''.
Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa haijapokea ombi kutoka Nato kuongezea shughuli zake huko Libya.
Serikali ya Libya ikarudia shutuma zake za mara kwa mara ikikemea fikra za magharibi.
Msemaji wa serikali Moussa Ibrahim alisema kuwa
''Tuko tayari kupigana ikibidi. Siyo dhidi ya jeshi la Libya tu bali kila mtu na kila kabila la Libya.Akaongezea kwa kulitaja Taifa la Qatar kama shirika tu la mafuta na siyo Taifa halisi.
Washukiwa wa shambulio la Belarus wakamatwa
Polisi nchini Belarus imewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio la bomu katikati ya jiji la Minsk na kusababisha vifo vya watu 12,akijumuishwa mtu ambae anadaiwa kutega bomu hilo katika kituo cha usafiri wa treni wa chini ya ardhi.Naibu Mwendesha Mashitaka Mkuu nchini humo, Anderi Shvad amesema uchunguzi wa awali dhidi ya watuhumiwa hao unafanywa na kwamba ushahidi wa kwanza umepatikana. Ameongozea kwamba kuna uwezekano mkubawa sana kwamba mmoja kati ya waliokamatwa ni muhusika wa uhalifu huo, kwa kutokana na ushahidi uliopatikana katika kanda ya video kwenye stesheni hiyo ya treni.
"Msichana wa Kitunisia" Blogu iliyopata DW BOBS Award 2011
Lina Ben Mhenni mwenye umri wa miaka 27
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Lina Ben Mhenni msichana kutoka Tunisia amepata tuzo ya blogu ya kimataifa ya DW BOBS Award.
Blogu iliopewa jina la "A Tunisia Girl" (Msichana wa Kitunisia) imeshinda tuzo ya blogu ya kimataifa ya THE BOBs inayotolewa na Deutsche Welle-BOB. Tuzo hiyo ilitolewa Aprili 12 mjini Bonn kwa kupitia anuani ya internet http://atunisiangirl.blogspot.com.
Lina Ben Mhenni amepata zawadi ya BOB Awards ya Deutsche Welle mhadhiri wa chuo kiku cha Tunis. Blogu yake hiyo ilihusika pia ukandamizaji na uchujaji wa habari wakati wa utawala wa rais wa zamani Zein el-Abidinne Ben Ali.
Blogu yake ikatoa mchango wakati wa vuguvugu la upinzani Desemba 2010 na Januari 2011 katika mji wa Sidi Bouzid na Kasserine na kuripoti kuhusu ukandamizaji wa vyombo vya dola na machafuko. Tangu wakati huo Mhenni anaandika juu ya matatizo yanayoikabili Tunisia kuelekea Demokarasia. Kwa muda mrefu blogu yake ilipigwa marufuku nchini Tunisia, na ikiwezekana tu kusomo yaliomo ikiwa uko nje ya nchi hiyo.
Kutokana na uteuzi huo wiki hii jopo la kimataifa tuzo hiyo itatolewa katika fani sita tofauti, wakati wa kongamano la Deutsche Welle la vyombo vya habari duniani tarehe 20 Juni mwaka huu 2011 mjini Bonn.
Mubarak wa Misri apelekwa hospitali
Bw Hosni Mubarak
Vyanzo vya usalama vimesema, aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak amepelekwa hospitali huko Sharm el-Sheikh.
Chanzo cha usalama kimeiambia shirika la habari la AFP, " Mubarak alilazwa katika hospitali ya kimataifa Sharm el-Sheikh mchana huu, huku kukiwa na ulinzi mkali kwenye eneo hilo."
Bw Mubarak, mwenye umri wa miaka 82, aliachia madaraka Februari 11 kufuatia maandamano ya siku 18 yaliyopata umaarufu dhidi ya uongozi huo.
Aliripotiwa kuwa na hali mbaya lakini washirika wake walikataa hilo.
Aliitwa na mwendesha mashtaka kuhojiwa juu ya madai ya rushwa na mauaji ya waandamanaji.
Bw Mubarak, watoto wake wa kiume na wake zao wamezuiwa kuondoka nchini humo na mali zao zimepigwa tanji.
Waandishi walisema amekuwa kimya huko Sharm el-Sheikh, kufuatia hatua yake ya kukimbilia katika jumba lake la kifahari baada ya kutolewa madarakani.
Ajitapa kutengua ndoa ya bosi wake
MSICHANA Jacklin [24] mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam amejitokeza na kutoa ushuhuda mbele ya wanawake kwa kujisifia kuvunja ndoa ya bosi wake kwa kujiita ni mwanamke wa kuigwa katika jamii.
Hayo aliyasema katika hafla fupi ya kumfunda mwali wa kike maarufu kama “Kitchen Party” iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita huko maeneo ya Kibaha mkoani Pwani.
Msichana huyo alitoa ushuhuda huo kwa kuwafundisha wanawake waliokuwa na tabia ya kuwaachia kila kitu wasichana wao wa kazi na hivyo kujenga tabia ya kutozishughulikia nyumba zao.
Akitoa mada aliyoiita "mwanamke bora" alifafanua neno hilo na kujipa mfano yeye mwenyewe alivyokuwa bora katika familia ya mume wake wakati alipokuwa akifanya kazi za ndani kabla hajaweza kuolewa na mwanaume huyo.
Alisema kuwa” jamani wanawake wenzangu tujitahidi kuangalia nyumba zetu sio tunawaachia wasichana wa kazi kila kitu hiyo ni hasara jamani, unaweza ukahatarisha ndoa yako”
“Mimi nilikuwa msichana wa kazi za ndani miaka miwili iliyopita bosi wangu wa kike alikuwa hashughuliki na nyumba yake kabisa na kuniachia kila kitu mimi na yeye ilikuwa kila kukicha anakwenda kwenye shughuli zake na akitoka anaranda na huwa anarudi usiku na wala alikuwa hana hata muda wa kumungalia mume wake na hata mtoto wake alikuwa hamshuhulikii".
Aliendelea kwa kusema kuwa tabia hiyo ilimchosha mume wa mwanamke huyo ambaye alikuwa sio msemaji na kila anapomkanya alikuwa hamsikii kabisa.
Mume wa mwanamke huyo alichoshwa na vitendo vya mke wake vya kutokumjali hata hajui mke wake kama anajua kupika ama la kwa kuwa alikuwa hashughuliki na mapishi.
"Hivyo mume huyo alinitaka mimi niondoke kwa muda kwa kuwa mke wake alikuwa hajishughulishi kwa kuona alikuwa na msaidizi".
Katika hali hiyo mwanamke huyo hakukubaliana na kitendo cha kumuondoa msichana huyo na kumwambia mtoto angepata shida na kumtaka msichana huyo asiondoke
Hali hiyo iliendelea na baadae baba huyo alidai alimtaka kumuoa msichana huyo kwa kuona kuvutia na utendaji wake kazi lakini msichana huyo alidai hakuafiki kabisa kwa kumlindia heshima bosi wake wa kike.
Hata hivyo mwanaume alimlazimisha amuoe na alituma washenga nyumbani kwa msichana huyo kwa lengo la kumuoa bila ya mke wake kujua na hatimaye alipomaliza hatua za awali alimtaka msichana huyo amuage mke wake kuwa anahitajika nyumbani kwao mkoani Morogoro kwa muda wa siku mbili ili akamuoe.
Hata hivyo bosi wake hakufahamu hilo alimruhusu na kumsihi asizidishe siku tatu arudi na alipoenda kwao alienda kuolewa na mume wa mwanamke huyo na aliporudi alimtambulisha mke wake kuwa kuanzia sasa msichana huyo ni mke mwenzake.
Ndipo mwanamke huyo alianza vurugu za hapa na pale akimtaka mume wake ampe talaka ili ampishe aweze kuishi na msichana huyo.
Na hatimaye mwanamke huyo alidai talaka kinguvu na aliweza kuondoka nyumbani hapo.
‘Jamani tutunze nyumba zetu, tuwatunze waume zetu, tutunze watoto wetu na si kuwaachia wasichana wa kazi kila kitu mtavunja nyumba zetu’ alimalizia msichana huyo
Hata hivyo baadhi ya wanawake ukumbini hapo walivutiwa na msichana huyo huku wengine wakiwa wanamlaani kwa kitendo chake cha kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake bila hata huruma.
Ufaytuaji risasi waendelea Ivory Coast
Ufyatuaji risasi wa hapa na pale ulisikika katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, siku moja baada ya aliyekuwa Rais Laurent Gbagbo kukamatwa.
Mwandishi wa BBC Mark Doyle alisema haijulikani iwapo ni majeshi yanayomwuunga mkono Gbagbo au ni wahalifu ndio wanahusika na ghasia hizo.
Lakini alisema makombora nayo yanarushwa.
Majeshi ya Ouattara yakipiga doria Abidjan
Bw Gbagbo alikamatwa baada ya kukataa kushindwa katika uchaguzi wa mwaka jana. Aliyemrithi Alassane Ouattara, amesihi vurugu zisitishwe.
Mwandishi wetu alisema kurejesha usalama ndio kitakuwa kipaumbele cha Bw Ouattara.
Harakati za pamoja za majeshi ya Ouattara, Umoja wa Mataifa na Ufaransa yalimkamata Bw Gbagbo kutoka kwenye makazi yake, ambapo alikuwa amezingirwa kwa zaidi ya wiki moja.
Bw Ouattara alisema Bw Gbagbo atashtakiwa, na tume ya ukweli na maridhiano itaundwa.
Takriban watu 1,500 waliuawa nchini humo na milioni moja walilazimishwa kukimbia makazi yao wakati wa mapigano yaliyokuwepo kwa miezi minne katika nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa kakao duniani.
Majeshi ya Umoja wa Mataifa na Ufaransa yaliingilia baada ya kuyashutumu majeshi ya Bw Gbagbo kutumia makombora mazito dhidi ya raia.
Umoja huo ambao umesaidia kuandaa uchaguzi huo, ulisema Bw Ouattara alishinda, lakini Bw Gbagbo alikataa kukubaliana na kushindwa huko.
Majeshi ya Malawi
Wakati huo huo Malawi inapeleka askari 850 kujiunga na majeshi ya kutunza amani ya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast.
Kamanda wa jeshi la ulinzi la Malawi Jenerali Marko Chiziko alisema wanajeshi hao wamepata mafunzo ya majeshi ya Marekani, Uingereza na Canada kaika shughuli za kuweka amani.
Aliyasema hayo katika sherehe za kuwaaga wanajeshi iliyofanyika mjini Lilongwe siku ya Jumanne
"Tuko tayari kutimiza majukumu yetu nchini Ivory Coast," alisema .
Rais Bingu wa Mutharika, ambae pia ni Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Malawi, aliwaambia wanajeshi hao kwamba ujumbe wao Ivory Coast hautakuwa rahisi.
"Mnakokwenda hali ni ngumu ," alisema " Hamtajua nani hasa ni adui kwani wote ni wananchi wa Ivory Coast, wanazungumza lugha moja, mavazi ya aina moja na wanakula chakula cha aina moja."
Alipokuwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Bw Mutharika alikwenda Abidjan mwezi Februari mwaka jana kushinikiza suluhisho la amani katika mgogoro kati ya Laurent Gbagbo na Alassane Quattara, mtu ambae wengi wanaamini alishinda uchaguzi uliozusha utata wa Desemba mwaka jana.
Akielezea mgogoro wa Ivory Coast "Ni vita miongoni mwa ndugu na wajomba, na ni changamoto kubwa.
Jenerali Chiziko alisema kikosi kingine cha askari 600 wa Malawi watajiunga na jeshi la kuweka amani la Umoja wa Mataifa baadae mwaka huu.
Jeshi la Malawi limeshawahi kushiriki katika shughuli za kuweka amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jimbo la Darfur nchini Sudan, Msumbiji, Rwanda, Burundi na Liberia na lililokuwa eneo la Serbia -la Kosovo.
Libya itakuwa 'Somalia mpya' aonya Koussa
Waziri wa ngazi ya juu aliyekimbia Libya ameonya kuwa Libya huenda ikaingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na nchi hio kuwa "somalia mpya".
Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuingia Uingereza, Moussa Koussa ameambia BBC umoja wa Libya ni muhimu sana.
Ametoa matamshi hayo huku waasi wakikataa pendekezo la Muungano wa Afrika wa kusitisha mapigano.
Muungano wa Afrika unasema Kanali Muammar Gaddafi amekubali mpango huo,
lakini siku ya Jumatatu vikosi vyake vilivamia mji wa Misrata.
Baada ya majuma nane ya mapigano,majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi yamefanikiwa kuwazidi nguvu waasi na kuwasukuma upande wa mashariki mwa Libya,lakini vikosi vya Nato vimezuai majeshi hayo kwenda mbele zaidi.
Bwana Koussa alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Kanali Muammar Gaddafi hadi siku 12 zilizopita,alipohamia London.
Ajiunguza na maji moto ili aweze kuomba barabarani
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina moja la Alamba anayekadiriwa kuwa na miaka 30 hadi35 mkazi wa Vingunguti, ameushangaza umma kwa kitendo chake cha kujiunguza kwa kutumia maji ya moto ili aweze kupata sababu ya kuweza kuombea fedha barabarani.
Mwanamke huyo alidiriki kujiunguza na maji ya moto katika mguu wake wa kushoto ili aweze kupata mbinu ya kutafutia pesa kwa nia ya kuomba msaada barabarani.
Katika hali ambayo iliwashangaza wengi mwanamke huyo siku ya pili baada ya kuunguza mguuu huo na maji alionekana akiwa amekaa barabarani ili kuomba msaada wa hali na mali ili aweze kujitibia kidonda chake hicho.
Mwanamke huyo aliketi pembezoni mwa barabara ya Uhuru maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam akiwa na jeraha lake kutumia fursa hiyo kuombea fedha.
Katika hali ya kushangaza mwanamke huyo alitakiwa kuondoka mahali hapo na baadhi ya ndugu zake waliopata taarifa hiyo lakini aligoma na kuendelea kuketi hapo kuomba msaada wa fedha.
Nifahamishe iligundua hali hiyo baada ya watu wawili ambao walikuwa wakimfahamu wakimtupia maneno ya kejeli na kumtaka aache kujidhalilisha kwa kuwa umasikini si kikwazo cha kujizalilisha barabarani na kuanza kuomba kama wafanyavyo wengine.
Wakati watu hao wakiwa wanamshambulia kwa maneno kadhaa mara walitokea wanawake wawili wakiwa wameongozana na mwanamme mmoja majina yao hayakupatikana mara moja walijitambulisha kuwa mwanamke huyo ni ndugu yao walifika mahali hapo kumtaka ndugu yao huyo aache kitendo hicho cha kuomba na kumuahidi wangempa kiasi ambacho alikuwa akikihitaji.
Ndipo mwanamke huyo alikubali kuondoka mahali hapo akitarajia atapewa kiasi ambacho alikuwa akikihitaji.
Hata hivyo nifahamishe ilipojaribu kumsogelelea mama huyo na kumuuliza yaliyomsibu hadi kufanya kitendo hicho alikiri kujiunguza kwa makusudi kwa kutumia maji moto ili aweze kupata kigezo cha kuombea kwa kuwa alikuwa ana shida ya kiasi cha shilingi laki mbili ili aweze kuanza biashara.
“Nilidiriki kufanya hivi kwa makusudi sababu kila nilipokuwa nikiwaomba msaada ndugu zangu waweze kunisaidia mtaji nifanye biashara walikuwa hawanisikilizi, sasa wameona nimekuja kuomba barabarani wameona ni kweli nina shida ya hizo fedha” alisema mwanamke huyo.
“Nilianza kuomba jana na naamini ningeomba muda wa wiki mbili Mungu angenisaidia ningepata kiasi ambacho nilikuwa nahitaji” alimalizia mwanamke huyo.
Pia ndugu hao walipotakiwa kuhakiki afya ya akili ya ndugu yao huyo walikiri kuwa ndugu yao ni mzima na timamu hakuwa na mapungufu ya akili hata kidogo na kufafanua aliamua tu kufanya kitendo hicho.
Mkama Amrithi Makamba
WILSON Mkama ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM mpya
baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa uteuzi uliotangazwa jana usiku.
Nafasi hiyo hadi kufika jana ilikuwa ikishikiliwa na Yusuf Makamba na alitemwa na kamati hiyo.
Bw. Mkama alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN).
Katika nafasi nyingine ya juu ni Katibu Uenezi na Utikadi amepewa Nape Nnauye nafasi iliyokuwa ikishikiwa na John Chiligati hivyo Chiligati kuwa makamu katika nafasi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Zanzibar ni Vuai Ali Vuai, Januari Makamba anakuwa Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Mwigulu Mchemba anakuwa Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Aisha Abdallah Juma anakuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni, na Nnauye anakuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Kwa mujibu wa Nnauye, Kamati Kuu mpya ya CCM ina wajumbe 14, wajumbe kutoka Tanzania Bara ni Abdulrahman Kinana, Zakhia Megji, Abdallah Kigoda, Pindi Chana, Stephen Wassira, Costansia Bugie na William Lukuvi.
Wajumbe kutoka Zanzibar ni Dk. Hussein Mwinyi, Dk. Maua Daftari, Samia Suluh Hassan, Shamsi Vuai Nahodha, Omary Yusuf Mzee, Profesa Mnyaa Mbarara, na Mohamed Seif Khatib.
Katika kujiimarisha, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, amewateua wajumbe saba wa NEC ili kukamilisha idadi ya wajumbe 10 anaoruhusiwa kuwateua.
Walioteuliwa ni Anna Abdallah, Peter Kisumo, Mwigulu Mchemba, Januari Makamba, Wilson Mkama, Ali Juma Shamhuna na Dk. Emmanuel Nchimbi.
Kikao hicho kilianza mapema juzi katika mchakato wa kuleta safu hiyo mpya
Baadhi ya wanachama wamefurahia uteuzi huo na kusema sasa CCM imeitendea haki chama hicho huku wengi wakifurahi kuondolewa kwa Makamba.
Watano Wafa Baada ya kulipukiwa na Mafuta ya Petrol
WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 46 kujeruhiwa vibaya baada ya kuungua na moto petrol walipokuwa wakijaribu kuiba mafuta hayo wakati ajali ilipotokea huko mkoani Singida.
Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 11 jioni ambalo lori liligongana injini ya tareni katika Stesheni ya Manyoni Singida
Akizungumzia ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Bw. Ally Rufunga alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika makutano ya reli na barabara iendayo Singida na Itigi.
Alisema lori hilo lilikuwa limebeba mafuta aina ya petrol yapatayo lita 40,000 likiwa linatoka Dar-es-Salaam kwenda Shinyanga na lilipofika kwenye makutano hayo liligongana na injini ya kichwa cha treni kilichotoka kusindikiza treni ya mizigo kituo cha Aghondi.
Hivyo kusababisha matenki ya mafuta kutoboka na kuanza kutiririsha na wananchi waliokimbilia na madumu na nyenzo nyingine kwa lengo la kuiba mafuta hayo walifariki baada ya tenki kulipuka kwa kuwa askari walizidiwa nguvu na wananchi waliofika kuiba mafuta hayo.
Katika waliokufa wawili ni askari waliofia hospitalini baada ya kuungua na moto wakati walipokuwa wakiwakataza wananchi wasiibe mafuta.
Matukio kama haya ya kupoteza uhai yanajitokeza mara nyingi licha ya serikali kukataza wananchi kukimbilia matukio kama haya kwa kuwa yanahatarisha maisha
Zaidi ya Mil.5 zakusanywa kufanikisha 40 ya wasanii 5star
IMEDAIWA kuwa kiasi cha shilingi zaidi ya milioni tano za kitanzania zimekusanywa katika michango mbalimbali waliyochanga wadau na wapenzi wa taarabu nchini kufanikisha shughuli ya kumalizia msiba wa wasanii wa kundi la 5Star waliofariki katika ajal
Akizungumzia shughuli hiyo, Mkurugenzi wa kundi hilo ambaye nae aliponyeka katika ajali hiyo Bw. Ali Juma maarufu kama‘Ali J’ alisema shughuli ya kumalizia msiba huo inatarijiwa kufanyika Aprili 17, mwaka huu katika ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
Amesema shughuli ya kumalizia msiba huo unatarajiwa kufanyika kwa pamoja katika ukumbi huo ili kukutanisha ndugu, jamaa na marafiki kwa pamoja kumalizia msiba huo.
Amesema wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho ambacho wanatarajiwa kuzitumia katika kumalizia msiba wa wasanii hao 13 waliofariki katika ajali nya pamoja Mikumi Morogoro.
Hivyo aliwataka kwa yeyote atakayeguswa ama atayetaka kujumuika katika shughuli hiyo anakaribishwa
Nyumba 73 tu kujengwa Gongolamboto
NYUMBA zipatazo 73 tu ndizo zimethibitishwa kujengwa upya baada ya tathimini iliyofanyika katika milipuko y mabomu ya Gongolamboto.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Said Meck Sadik katika taarifa yake.
Amesema nyumba 73 zitakazojengwa upya ambapo nyumba 26 wamiliki wake watajengewa nyumba hizo maeneno mengine kutokana na nyumba hizo zilikuwa mabondeni.
Amesema na nyingine zitajengwa mahali zilipobomoka nyumba hizo kwa kuwa maeneo hayo yameonekana kuwa sakama.
KAtika t aarifa yake hiyo amesema kuwa nyumba hizo ndizos zimethitishwa kumobolewa na mabomu hayo aktika utafiti uliofanyika kwa muda mrefu.
Amesema nyumba nyingine zipatazo 1,693 ambazo zilipata uharibifu kidogo zitakarabatiwa na si kujenga upya.
Amesema ujenzi wa nyumba hizo unatarajia kuanza muda wowote kuanzia sasa kwa kuwa tayari wamekwisha kuikabidhi kampuni ya Suma-JKT kiasi chaShilingi. milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa saruji ili kufyatua matofali na usagaji wa kokoto
zaidi ya billion 1 imetengwa kuteketeza kunguru
KUTOKANA na kero na uharibifu unaosababishwa na kunguru weusi nchini zaidi ya billion 1 imetengwa kuteketeza kunguru hao katika mradi utakaofanyika katika kipindi cha miaka miwili.
Mbinu mpya za kupambana na kuwamaliza kunguru hao imeandaliwa na imedaiwa hadi ifikapo mwaka 2013 kunguru hao wasionekane kabisa nchini.
Hii imekuja baada ya kuonekana kunguru hao kuchangia kupoteza kasia jamii ya ndege na viumbe vingine wadogowadogo waishio maeneo ya Pwani.
Hayo yalijulikana hivi karibuni baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira Tanzania (WCST), Bi. Anne Lema alipiokuwa akitoa taarifa kuhusiana na mradi huo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema, msaada kutoka balozi za Dernmark, Finland na Shirila la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID) ambao kwa pamoja wamechangia Dola za Marekani 748,200 sawa na Sh bilioni 1.12 kufanikisha mradi huo kwa muda wa miaka miwili.
Mbali na hao pia Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Wanyamapori imetoa kiasi cha Shilingi milioni 150 ambazo zimetumika kuendesha shughuli za awali za mradi huo.
Amesema mikakati iliyowekwa na serikali kwa kushirikana na wadau hao watateketeza ndege hao kwa kutumia sumu, risasi na mitego mingine kuwaangamiza kunguru hao.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment