KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, March 11, 2011

Wanafunzi waandamana kupinga nauli mpya


WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam jana waliandaa maandamano kuelekea Ikulu kupinga ongezeko la nauli za daladala lililoanza jana nchini kote.
Wanafunzi hao kutoka shule mbalimbali hawakuweza kutimiza adhama yao hiyo bada ya Kikosi Cha Kutuliza Ghasia [FFU] kuwatimua wanafunzi hao.

Maandamano hayo yaliyokuwa na lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwa kutoridhishwa na ongezeko hilo la nauli kutoka shilingi 100 hadi 150.

Wanafunzi hao walikuwa kaitka makundi makuu mawili ambapo kundi moja lilikuwa likianzia Katika viwanja vyaMnazi Mmoja na linguine lilikuwa likianzia maeneo ya Karume ambapo lilishanya shule za wilaya ya Ilala.

Wakizunmza na NIFAHAMISHE eneo la tukio wanafunzid hao walidai wanataka wakamueone Rais wafikishe kilio chao ili warudishiwe nauli ya awali yashilingi 100 ili kuwapunguzia mzigo wazazi wao kuwasomesha.

Hata hivyo, jitihada za wanafunzi hao kufikisha ujumbe wao Ikulu ziligonga mwamba baada ya kudhibitiwa na FFU muda mfupi tu baada ya kuingia barabarani nabaadae askari hao waliweza kuwashikilia wanafunzi wawili wa kiume baada ya kuonekana kukaidi na wenzao kufanikiwa kukimbia, Wanafunzi hao walipakiwa kwenye gari la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Msimbazi.

Nauli mpya za mabasi ya daladala zimeannza jana zilizotangazwa naMamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).


Mripuko katika kinu cha nuklia Japan
Kumetokea mripuko mkubwa katika kinu cha nuklia cha Japan, ambacho kiliharibika katika tetemeko kubwa la ardhi la jana.


Mtambo wa nyuklia Japan

Waziri Mkuu amewasihi walio karibu na kinu hicho cha Fukushima kuhama.

Kuta za chuma tu za kinu hicho ndio bado zimesimama. Wafanyakazi wane wamejeruhiwa.

Msemaji wa serikali alieleza kuwa uchunguzi bado unafanywa juu ya mripuko wa kinu hicho, kilioko kilomita miambili na hamsini kaskazini mwa Tokyo.

Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kaskazini mashariki mwa Japan na kuibua mawimbi ya tsunami ambayo yamesababisha hasara kubwa.


Kulingana na habari za awali, televisheni nchini Japan, imeonesha magari, meli na hata majengo makubwa yakizolewa na mawimbi makubwa ya maji ya bahari baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 8.9 kupiga.

Tetemeko hilo pia limesababisha moto katika maeneo mengi ya Japan ikiwemo mji mkuu Tokyo, ambapo imearifiwa watu 15 wamekufa.

Limepiga kiasi cha kilometa 400 kutoka mji mkuu na mawimbi yakaingia umbali wa maili 20 ndani.

Wataalam wa matetemeko wamesema hili ni moja ya tetemeko kubwa kuipiga Japan kwa miaka mingi.

Wakati tetemeko lilipopiga, majengo mjini Tokyo yaliyumba. Mtu kutembea ilikuwa sawa na kuwemo ndani ya meli inayopigwa mawimbi baharini.

Watu walishuka chini kutoka katika ofisi zao na kusalia mitaani wakiwa wanatetemeka.

Moto mkubwa ulizuka katika eneo moja la mji na katika maeneo mengine, watu waliojeruhiwa walitolewa nje ya vituo.

Mara moja serikali ilitoa onyo la tsunami.

Katika mji mkuu Tokyo, usafiri wa umma umesimamishwa, lifti katika majengo mengi zimezimwa na maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani za wazi na vituo vya treni.

Onyo la tsunami limetolewa pia katika maeneo yote ya bahari ya Pacific ikiwemo Philippines, Indonesia, Taiwan, Hawaii, na mwambao wa bahari ya Pacific nchini Urusi na kaskazini mwa Amerika Kusini.

Mawimbi makubwa yalipiga katika miji ya Miyagi na Fukushima, na kuharibu vibaya sehemu kubwa ya makazi ya watu eneo la pwani. Shirika la habari la Kyodo limesema mawimbi yaliyofikia urefu wa mita 10 na kupiga bandari ya Sendai huko Miyagi .

Wananchi waondolea hofu
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika Kamandi ya Ulinzi wa Anga leo wanatarajia kufanya mazoezi ya kurusha ndege za kivita katika eneo la Dar es Salaam na Pwani.
Hivyo kufuatia hilo Jeshi hilo linawaondoa hofu kutoogopakutokana na halki itakayojitokeza katika mazoezi hayo.

Huu ni muendelezo wa mazoezi yaliyokwishafanyika katika maeneo mengine nchini ambapo yataanza saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.

Taarifa hii imetolewa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi
Makombora ya Gongolamboto yakutwa ndani ya nyumba -Kimara
WAKATI vuguvugu na watu wakikaribia kusahau mlipuko wa mabomu yaliyotokea katika Kambi ya Jeshi Gongolamboto, makombora mengine mawili yamegundulika yamejichimbia ndani ya nyumba mbili katika huko Kimara Baruti na Mbezi kwa Msuguri
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki alisema kuwa wanajeshi wanaendelea kukusanya mabomu yaliyotapakaa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Alisema mabomu hayo yaliingia kwa kutumia upande mmoja wa nyumba na lingine liko kwenye nyumba ambayo wamiliki wa ke bado hawajahamia.

Katika uhakiki wa jumla ya nyumba 69 ziliharibiwa na mabomu hayo lakini uhakiki bado unaoendelea na riapoti kamili kumalizika jumapili ya wiki hii

Wivu wasambaratisha maisha yake


ALLY Salum [48] anayedaiwa kuwa fundi ujenzi mkazi wa Yombo Buza, amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya mkonge kutokana na kuzidiwa na wivu wa mapenzi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kuwa marehemu huyo alikutwa amekufa juzi, majira ya saa 8.00 mchana nyumbani kwake.
Alisme Ally kabla hajachukua uamuzi wa kujinyonga aliacha ujumbe maalum uliofanya ajinyonge yeye mwenyewe.

Alisema ujumbe huo ulionyesha dhahiri kuudhiwa na mke wake baada ya kuona mabadiliko yakitabia juu yake

Ujumbe aliouacha ulisomeka , “nimeamua kujinyonga kwa hiyari yangu kutokana na mke wangu kushauriwa na mama Salehe kutoka nje ya ndoa, hivyo namuachia ukumboi aendelee na hizo starehe zake, ila naomba mke wangu asibughudhiwe.

“Mali nilizochuma naye zibaki mikononi mwake, asinyang’anywe na mtu yeyote wala ndugu yangu yoyote, napenda kuwajulisha nilikuwa na mke mwingine mdogo yupo maeneo ya Kimbiji Kigamboni, Sanda yangu nilishaandaa siku nyingi ipo kwenye sanduku,” ulieleza ujumbe huo.

Polisi wanaendelea na upelelezi huku maiti imehifadhiwa hospitali yaTemeke.

Katika tukio jingine, MTOTO wa kike [1] ameokotwa akiwa hai na wapita njia huko maeneo ya Yombo Vituka jijini Dar es Salaam.

Mtoto huyo alitupwa na mtu asiyejulikana na wasamalia wema waliopita eneo hilo walimuona na kumuokotwa nakumkuta akiwa hai

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw. David Misime, ilisema kuwa mtoto huyo aliokotwa juzi majira ya saa 2.15 usiku.

Alisema mtoto huyo alikutwa akiwa amefungwa na kufunikwa na kitenge na kulazwa katika njia hiyo.

Taarifa ilipoifikia polisi mtoto huyo amechukuliwa na amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uangalizi zaidi

No comments:

Post a Comment