KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, March 25, 2011

Maandamano Yemen




Mamia kwa maelfu ya watu walitazamiwa kushiriki maandamano makubwa katikati ya mji mkuu wa Yemen, Sanaa wiki moja baada ya watu hamsini kuuawa na vikosi vya usalama wakati wakiandamana.


Waandamanaji walikuwa wamepanga maandamano makubwa kuwahi kufanyika ya kudai Rais Ali Abdullah Saleh ajiuzulu.




Bw Saleh ameuambia mkutano wa halaiki ya wafuasi wake kuwa yuko tayari kuachia madaraka, ila tu kwa mtu anayemuamini.

Askari walifyatua risasi angani kuwazuia wafuasi wa Bw Saleh wasielekee waliko waandamanaji wanaompinga kiongozi wao.

Katika hotuba yake, Rais Saleh ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu ameshutumu mauaji ingawa aliwataka wafuasi wake wawe na msimamo imara.

Kabla ya hotuba hiyo alikanusha kuwa alihusika kwa vyovyote vile katika mauaji ya waandamanaji wiki iliyopita.

Shirika la Amnesty International limeionya serikali dhidi ya matumizi ya nguvu ya kupindukia, na kuongezea kuwa serikali haiwezi kutumia risasi kutanzua mgogoro unaoikabili.








Maadui Libya wavaana miji muhimu




Walioshuhudia wamesema waasi wa Libya wanakaribia kupambana na majeshi yanayomtii Kanali Gaddafi kwenye mji wa Ajdabiya.

Ndege za Ufaransa na Uingereza zimerusha mabomu karibu na mji ulio mashariki mwa nchi hiyo wakati wa usiku, yakiwemo makombora ya serikali.


Libya
Waasi walijaribu kuwashambulia wanajeshi wanaomwuunga mkono Gaddafi baada ya kufanyika mashambulio ya ndege, lakini walisema ilibidi waghairi.


Mji huo umezingirwa kwa siku kadhaa sasa. Wakazi waliokimbia walisema mitaa ilibaki mitupu, na majeshi ya serikali yalikuwa yakifyatua risasi kiholela.


Majeshi ya nchi za magharibi yalianza kushambulia kwa mabomu wiki iliyopita kwa nia ya kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa lililozuia majeshi ya Libya kuwashambulia raia kwa ndege.


Majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato yanatarajiwa kuongoza harakati hizo za kijeshi badala ya Marekani kwa siku zijazo.








Maafisa wamesema uvamizi huo umedhoofisha majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi kwa kiwango kikubwa, lakini mapigano yameendelea Misrata kwa upande wa magharibi na Adjabiya huko mashariki.













Milipuko yaendelea kurindima Tripoli




Waasi nchini Libya wamekabiliana na vikosi vya kiongozi wa nchi hiyo, kanali Muammar Gadhafi mashariki mwa nchi hii leo, huku ndege za jeshi la muungano zikishambulia silaha nzito zinazotumiwa na serikali kuukandamiza upinzani. Waasi hao wameapa kusonga mbele kuelekea mji mkuu Tripoli. Miripuko mikubwa ilisikika katika maeneo ya kusini mwa Tripoli, mapema leo huku mashambulizi ya angani yanayofanywa na vikosi vya jeshi la muungano kutekeleza marufuku ya ndege kutoruka katika anga ya Libya, yakiendelea. Jumuiya ya kujihami ya NATO imesema harakati ya kijeshi nchini Libya huenda ikadumu kwa miezi mitatu, huku Ufaransa ikionya kwamba mzozo huo huenda usimalizike hivi karibuni. Awali katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema mpaka sasa hakuna dalili kwamba serikali ya Libya inaheshimu matakwa ya baraza la usalama la umoja huo ya mapigano kusitishwa.








NATO yachukua uongozi wa operesheni ya Libya


Katibu Mkuu wa NATO, Jenerali Anders Fogh Rasmussen.




Uamuzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuchukua uongozi wa operesheni za kijeshi dhidi ya Libya umepokelewa vyema kwenye jumuiya ya kimataifa, huku jitihada za Umoja wa Afrika kuutatua mgogoro huu kisiasa zikiendelea.

Katibu Mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, ametangaza uamuzi wa jumuiya yake kuchukua rasmi jukumu la kuongoza operesheni ya kijeshi dhidi ya utawala wa Libya, ikiwa ni utekelezaji wa Azimio Namba 1973 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililoiwekea nchi hiyo marufuku ya kuruka ndege kwenye anga lake.

"Jumuiya ya NATO sasa imeamua kusimamia amri ya marufuku ya anga kwa Libya. Tunachukua hatua ikiwa ni sehemu ya juhudi za kimataifa kuwalinda raia dhidi ya mashamulizi ya utawala wa Gaddafi." Amesema Rasmussen.

Kwa vyovyote vile, huu ni uamuzi uliokuwa ukingojewa sana na jumuiya ya kimataifa, zikiwemo Uingereza, Marekani na Ufaransa, mataifa ambayo, hadi sasa, ndiyo yanayoongoza kampeni hiyo.

Serikali ya Uingereza imeuita uamuzi huo kuwa ni "hatua muhimu ya kusonga mbele", huku msemaji wa Waziri Mkuu, David Cameron, akisifia pia mchango wa ndege 12 za kijeshi kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Nchini Ufaransa, uamuzi huu wa NATO umemfanya mkuu wa majeshi ya ulinzi, Admirali Édouard Guillaud, kuhitimisha kuwa sasa operesheni ya majeshi ya washirika nchini Libya itaendelea kwa wiki chache tu na sio miezi.

Huko Brussels, ambako viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana kwa siku ya pili leo kujadiliana masaibu ya uchumi wa eneo lao, wamekuwa pia wakijadiliana suala la Libya



Umoja wa Afrika watafuta suluhu ya kisiasa



Viongozi wa Umoja wa AfrikaHuku hayo yakiendelea


Viongozi wa Umoja wa AfrikaHuku hayo yakiendelea, mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Jean Ping, anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa serikali ya Libya pamoja na wale wa waasi, katika jitihada za Umoja huo kuutatua mgogoro wa Libya kwa mazungumzo.

Umoja wa Afrika umekuwa ukipinga vikali uingiliaji kati wowote wa kijeshi dhidi ya Libya, na unasisitiza kuheshimiwa kwa mamlaka ya taifa hilo la Afrika ya Kaskazini.

Hata hivyo, kwa kuwa nchi za umoja huo ni wanachama pia wa Umoja wa Mataifa, na kwa kuwa Umoja wa Mataifa ndio uliopitisha azimio la kuiwekea Libya vikwazo vya anga vilivyopelekea uingiliaji kati kijeshi, mataifa kadhaa ya Afrika yanajikuta yakifungwa mikono nyuma.

Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa, Ban Ki-moon, anasema kuwa hadi sasa, utawala wa Muammar Gaddafi haujaheshimu azimio hilo la Baraza la Usalama, na kwa hivyo kuna uwezekano wa hatua zaidi kuchukuliwa.

"Hakuna dalili ikiwa utawala wa Libya umechukua hatua za kutekeleza maazimio namba 1970 na 1973. Na ikiwa Libya itaendelea kukaidi utekelezaji wa azimio namba 1973, ujumbe wangu umesema kuwa Baraza la Usalama linaweza kupaswa kujitayarisha kwa hatua nyengine zaidi." Amesema Ki-moon.







Uganda kuzuia mali za Gaddafi



Rais Yoweri Museveni wa UgandaNa katika hali isiyotarajiwa


Rais Yoweri Museveni wa UgandaNa katika hali isiyotarajiwa, Uganda, ambayo imekuwa rafiki mkubwa wa Gaddafi, imesema iko tayari kuzizuia mali za serikali ya Libya zilizomo nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Okello Oryem, ameliambia Bunge la nchi hiyo kwamba mali zote zinazomilikiwa na utawala wa Gaddafi nchini mwake zitazuiwa kwa kufuatana na azimio la Umoja wa Mataifa.

Uganda inakuwa nchi ya mwanzo ya Kiafrika kutangaza uzuwiaji wa mali za Gaddafi, ambapo inakisiwa kuwa miradi ya Mamlaka ya Uwekezaji iliyo chini ya mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam, inafikia thamani ya Euro bilioni sita kwenye nchi mbalimbali barani humo.

Nchini Uganda peke yake, mali za Libya zinafikia thamani ya Euro milioni 300, zikiwa zimeekezwa katika miradi na makampuni mbalimbali ikiwemo kampuni ya simu ya Uganda Telecom, Shirika la Ujenzi na Nyumba, hoteli ya Viktoria na mradi wa kujenga bomba la mafuta kati ya Kenya na Uganda, Tamoil.

Uganda ni miongoni mwa wajumbe wa kamati maalum ya Umoja wa Afrika inayotafuta suluhu ya mgogoro wa Libya.








Watu 100 wadaiwa kufa Libya



Majeshi ya Libya yakikagua kifusi cha jengo baada ya mashambulizi





Sauti za miripuko mikubwa ya makombora kutoka angani imesikika tena leo (25.03.2011), Kaskazini mwa mji wa Tripoli, ikiwa sehemu ya mashambulizi ya majeshi ya Muungano kuzuwia ndege kuruka katika anga ya Libya.

Akielezea tukio hilo pasipo ufafanuzi wa kina, msemaji wa jeshi la Libya amedai raia na wanajeshi kadhaa wameripuliwa na makombora hayo kutoka ndege za kivita.

Mashambulizi haya ya leo yamefanyika muda mfupi baada ya Umoja wa Kujihami wa NATO kutangaza kuanza kushiriki rasmi katika operesheni ya kimataifa nchini Libya.

Wakati majeshi ya Muungano yakiendeleza mashambulizi, msemaji wa serikali ya Libya, Moussa Ibrahim, ameonya kuhusu makombora yaliyoporomoshwa jana, ambayo yalilenga jengo la kituo cha taifa cha televisheni pamoja na radio ya nchi hiyo.

Amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati kwa kukemea kitendo hicho cha kuangamiza taasisi hiyo muhimu ya umma wa Walibya.

Raia miongoni mwa wahanga

Waombolezaji wakisubiri kuzika miili ya jamaa zao, baada ya mashambuliziTaarifa za maafisa wengine wa Libya pamoja na wahudumu wa hospitali kadhaa, zinasema raia, wakiwemo wanawake, ni miongoni mwa waliouwawa katika mashambulizi yaliyofanyika katika maeneo ya Tripoli.

Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba, mpaka jana idadi ya watu waliokufa kutokana na mshambulio hayo imefikia 100, huku ikilalamikia nchi za Magharibi kuingia vitani kwa niaba ya waasi.

Maafisa kwa upande wa vikosi vya Muungano wamekanusha kuhusika na kifo chochote kutokana na operesheni zao ambazo leo hii zimeingia siku ya saba.

Hapo jana (24.03.2011) mfanyakazi wa chumba cha maiti katika hospitali kubwa mjini Tripoli, Ahmed Hussein, aliwaonesha waandishi wa habari maiti 15 za wanaodaiwa kufa kutokana na mashambulizi hayo.

Mfanyakazi huyo aliwaambia waandishi hao wa habari kwamba maiti hizo ni kwa tukio la siku hiyo tu na kwamba bado kuna miripuko mingine katika makazi ya wanajeshi imetokea.

Miili ya watu hao ilikuwa imelazwa katika vigari vya kubebea maiti, zikiwa zimefunikwa na mashuka mazito ya rangi tofauti tofauti.

Serikali ya Libya imetilia mkazo kauli yake ya kwamba majeshi ya Muungano yanauwa kwa kutolea mfano mashambulio ya mji wa Tajura uliyopo mashariki mwa Tripoli.

Hata hivyo, waasi nao wanasema vifo vilivyotokea huko ni vya watu wao.

Kwa ujumla, bado majeshi ya Gaddafi yanasonga mbele katika mashambulio ya ardhini, ingawa inaonekana nguvu zake zimedhoofishwa na vikosi vya anga baada ya kuyashambulia makao ya uongozi wa jeshi lake anga, kama ilivyoelezwa na Uingereza hapo awali.

Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Libya, Khalid Kaim, amesema hali ilivyo katika mji wa Misrata, ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini humo, ni ngumu sana.

"Maisha hayajarejea katika hali ya kawaida Misrata kwa sababu bado kuna watu wanadungua watu kwa risasi pamoja na mashambulio ya anga kutoka majeshi ya Muungano." Amesema Kaim.

Huko katika mji wa mashariki wa Benghazi, waasi wanaendelea na mazoezi ya kijeshi, huku Baraza lao likisema lina wapiganaji takribani 1,000 walio katika uwanja wa vita.










LONGEST SERVING WORLD LEADERS


1. Sultan Hassanal Bolkiah Brunei 1967





2. Colonel Muammar Gaddafi Libya 1969





3. Sultan Qaboos bin Said al Said Oman 1970







4. Prime Minister Khalifa ibn Salman Al Khalifa Bahrain 1970






5. President Jos Angola 1979






6. President Teodoro Obiang Nguema Mbasogo Equatorial Guinea 1,979






7. President Paul Biya Cameroon 1,982




8. King Mswati III Swaziland 1,986






9. President Yoweri Museveni Uganda 1,986







10. President Blaise Compaoré Burkina Faso 1,987












Libyan Colonel Muammar al-Gaddafi





Muammar Abu Minyar al-Gaddafi, also known as Colonel Gaddafi; born 7 June 1942, has been the de facto leader of Libya since a coup in 1969. Gaddafi was born in a Bedouin family near Sirt. Although this claim is not proven, there is speculation that his biological father was Albert Preziosi, a Free French Forces air officer of Corsican origins.


•He is married to Safia Farkash . Gaddafi has eight biological children, seven of them sons. He also had two adopted children. His adopted daughter was killed. His adopted son, Milad Abuztaia Al-Gaddafi is also his nephew. Milad is credited with saving Gaddafi's life during the April 1986 bombing of the Gaddafi compound.
•His eldest son, Muhammad al-Gaddafi, was born to a wife now in disfavour, but runs the Libyan Olympic Committee.
• The next eldest son by his second wife is Saif al-Islam Muammar Al-Gaddafi, who was born in 1972 and is an architect. He runs a charity (GIFCA) which has been involved in negotiating freedom for hostages taken by Islamic militants, especially in the Philippines. In 2006, after sharply criticizing his father's regime, Saif Al-Islam briefly left Libya, reportedly to take on a position in banking outside of the country. He returned to Libya soon after, launching an environment-friendly initiative to teach children how they can help clean up parts of Libya. He is involved in compensation negotiations with Italy and the United States.
•The third eldest, Saadi Gaddafi, is married to the daughter of a military commander. Saadi runs the Libyan Football Federation and signed for various professional teams including Italian Serie A team U.C. Sampdoria, although without appearing in first team games.
•Gaddafi's fourth son, Mutassim Gaddafi, was a Lieutenant Colonel in the Libyan army. He now serves as Libya's National Security Advisor, in which capacity he oversees the nation's National Security Council. Saif Al-Islam and Moatessem-Billah are both seen as possible successors to their father.
•The fifth eldest, Hannibal Gaddafi once worked for General National Maritime Transport Company, a company that specializes in Libyan oil exports. He is most notable for being involved in a series of violent incidents throughout Europe. In 2001, Hannibal attacked three Italian policemen with a fire extinguisher; in September 2004, he was briefly detained in Paris after driving a Porsche at 90 mph in the wrong direction and through red lights down the Champs-Élysées while intoxicated; and in 2005, Hannibal in Paris allegedly beat model and then girlfriend Alin Skaf, who later filed an assault suit against him. He was fined and given a four month suspended prison sentence after this incident. In December 2009 police were called to Claridges Hotel in London after staff heard a scream from Hannibal's room. Aline Skaf, now his wife, was found to have suffered facial injuries including a broken nose, but charges were not pressed after she maintained she had sustained the injuries in a fall. On 15 July 2008, Hannibal and his wife were held for two days and charged with assaulting two of their staff in Geneva, Switzerland and then released on bail on 17 July. The government of Libya subsequently put a boycott on Swiss imports, reduced flights between Libya and Switzerland, stopped issuing visas to Swiss citizens, recalled diplomats from Bern, and forced all Swiss companies such as ABB and Nestlé to close offices. General National Maritime Transport Company, which owns a large refinery in Switzerland, also halted oil shipments to Switzerland. Two Swiss businessmen who were in Libya at the time have, ever since, been denied permission to leave the country, and even held hostage for some time. (see Switzerland-Libya conflict). At the 35th G8 summit in July 2009, Gaddafi called Switzerland a "world mafia" and called for the country to be split between France, Germany and Italy.
•Gaddafi's two youngest sons are Saif Al Arab and Khamis, who is a police officer in Libya.
•Gaddafi's only daughter is Ayesha al-Gaddafi, a lawyer who had joined the defense team of executed former Iraqi leader Saddam Hussein. She married a cousin of her father in 2006.
•His adopted daughter, Hanna, was killed in the April 1986 United States bombing of Libya. At a "concert for peace", held on 15 April 2006 in Tripoli to mark the 20th anniversary of the bombing raid, U.S. singer Lionel Richie told the audience:"Hanna will be honoured tonight because of the fact that you've attached peace to her name."
•In January 2002, Gaddafi purchased a 7.5% share of Italian football club Juventus for USD 21 million, through Lafico ("Libyan Arab Foreign Investment Company"). This followed a long-standing association with the Italian industrialist Gianni Agnelli and car manufacturer Fiat.









Bodyguards


Muammar al-Gaddafi maintains a 40 member group of women unofficially referred to as the Amazonian Guard as his personal bodyguards and protectors. Upon selection as a candidate for the group the ladies are put through a tough training regimen in firearms and martial arts. His body guards are killing machines. They are trained to protect him and die for him. They also take a vow of chastity and apparently many young women are dying to take on this role. The Amazonian guard dress in western style fatigues, can wear make up, western hair styles, high heels, and other clothing not deemed acceptable in the Muslim world. These women are supposedly all virgins.







Gaddafi is a controversial figure worldwide due to his choice of bodyguards. His 40-member bodyguard contingent, known as the Amazonian Guard, is entirely female. All women who qualify for duty must be virgins, and are hand-picked by Gaddafi himself. They are trained in the use of firearms and martial arts at a special academy before entering service.







Marilyn Monroe



The most endlessly talked-about and mythologized figure in Hollywood history, Marilyn Monroe remains the ultimate superstar, her rise and fall the stuff that both dreams and nightmares are made of. Innocent, vulnerable, and impossibly alluring, she defined the very essence of screen sexuality. Rising from pin-up girl to international superstar, she was a gifted comedienne whom the camera adored, a luminous and incomparably magnetic screen presence. In short, she had it all, yet her career and life came crashing to a tragic halt, a Cinderella story gone horribly wrong; dead before her time — her fragile beauty trapped in amber, impervious to the ravages of age — Monroe endures as the movies' greatest and most beloved icon, a legend eclipsing all others. www.allmovie.com




Castro condemns NATO's 'inevitable' war on Libya




STORY HIGHLIGHTSCastro says U.S., NATO will "take advantage" of Libya's internal conflict Castro also condemned what he called "a colossal campaign of lies" from Western media Too soon to pass judgment on his longtime ally Moammar Gadhafi, says Castro
Havana, Cuba (CNN) -- Cuba's former President Fidel Castro denounced on Thursday what he says is the inevitable U.S.-backed invasion of Libya by NATO to get its hands on that country's oil.

In an essay called "NATO's Inevitable War" and published in Cuban state media, Castro wrote that the United States and NATO "couldn't help but take advantage of the internal conflict that has arisen in Libya to promote military intervention," expressing concern because Libya is a major oil producer. Castro also condemned what he called "a colossal campaign of lies" spread by the Western media about Libya.

He has repeatedly denounced plans to invade Libya but has said it is too soon to pass judgment on his longtime ally Moammar Gadhafi.

No comments:

Post a Comment