KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, February 16, 2011

Polisi alfu 2 wapiga doria kuzuwia ghasia Yemen


Maandamano ya wanaoipinga serikali na wanaoumuunga mkono rais wa Yemen,Ali Abdullahi Saleh yameingia siku yake ya nne mjini Sa'naa.Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la AFP,kiasi ya watu wanne wamejeruhiwa kwenye purukushani hizo na waandishi wengine wa habari nao pia walipigwa na wafuasi wa Rais Saleh.Ghasia hizo zilitokea kwenye eneo lililo karibu na Chuo Kikuu cha Sa'naa pale wanafunzi walipokuwa wakiandamana wakimtaka rais Saleh ajiuzulu pamoja na wapambe wake wa chama cha GPC.Kiasi ya maafisa alfu 2 wa polisi wanapiga doria kwenye mji mkuu wa Sa'naa ili kuzuwia fujo zaidi.Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa mtu mmoja ameuawa katika maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment