KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 19, 2011

Mmiliki Dowans akamatwe -wadau


WITO umetolewa kwa wadau mbalimbali nchini kutaka aliyejitokeza na kudai kuwa yeye ni mmiliki wa Dowans Holding Tanzania Limited akamatwe ili aweze kuhiojiwa zaidi kuhusiana na mitambo hiyo.
Juzi Bw.Suleiman Mohamed Yahaya Al Adaawi, raia wa Oman alijitokeza na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari na kujitambulisha kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa mitambo ya Dowans.

Alisema yeye ndiye mwenye hisa nyingi katika kampuni hiyo na alijitokeza kuleta mitambo hiyo Tanzania ili iweze kusaidia mapungufu ya umeme yanayoikabili nchi.

Katika mkutano wake huo na wahariri alitoa masharti ya kutopigwa picha wala kurekodiwa na kameramkwa kudai hata utamaduni wa kuonekanda kwenye3 vyombo vya habari japo kuwa yueye ni mfanyabiashara mkubwa duniani.

Alaadawi alisema ameamua kuja nchini kujitambulisha kwa kuwa suala hilo limezua utata kwa muda mrefu.

Alisema ameamua kuja nchi kwa madhumuni mahususi ya kushughulikia upotoshaji na uwakilishi usio juu ya Dowans; na kujua kama kuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano juu ya mambo yaliyopo kwa sasa.

Alisema amekuja nchini kwa mualiko na serikali lakini baadae alibadili kauli na ksuema alialikwa kuja nchini kuzungumzia suala hilo na shirika la umeme Tanzania [TANESCO]

Alisema yuko tayari kwa mazungumzo yoyote inayohusiana na kampuni na kutaka kampuni hiyo iheshimiwe na isipotoshwe kama inavyofanywa sasa.

Hata hivyo serikali imekana kuhusika kumpa mwaliko mmiliki huyo na Tanesco pia imekana kumpa mwaliko mmiliki huyo.

Kuhusiana na utata huo wadau wameitaka serikali kutumia nguvu za dola wamkamate mmiliki huyo kutokana na kupinda wka maelezo yake ili aweze kuhojiwa upatikane ukweli kuhusiana na suala hilo linalozua utata serikali kwa muda mrefu.


Hata hivyo kamati ya nishati imeshauri kuwashwa kwa mitambo hiyo ya kufua umeme ili iweze kupunguza makali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini kote

No comments:

Post a Comment