KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, February 18, 2011

JK awatoa hofu wakazi Gongolamboto







RAIS Jakaya Kikwete amewataka wakazi waishio Gongolamboto na kwingineko warudi majumbani, kwa kuwa hakuna milipuko mingine itakayotokea tena na kuwahakikishia usalama wakazi hao.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati alipotembelea katika kambi ya Jeshi Gongolamboto iliyoleta mlipuko wa mabomu na kusababisha vifo na majeruhi.

Mbali na hilo Rais Kikwete pia alisema janga hilo ni la Taifa kwa kuwa kambi hiyo ni kambi kuu ya kuhifadhia vifaa vya jeshi.

“Ni janga la Taifa, mana kambi hii ndio tegemezi kwa kuhifadhia vifaa mabalimbali ya jeshi yakiwemo mabomu, silaha, mavazi na vifaa vingine vingi vya jeshi hivyo janga hili ni la taifa” alisema Kikwete kwa masikitiko

Mlipuko huo ulisabasisha maafa makubwa ukiwemo kuuungua kwa magari yapatayo matano katika kambi hiyo, maghalana inasadikiwa vifo vimefikia 4o na majeruhi zaidi ya 300 ambao wameripotiwa katika vituo mbalimbali vya afya.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Abrahman Shimbo alisema jeshi hilo huwa na utaratibu wa kukagua mabomu hayo na alibainisha kuwa walikagua mabomu hayo siku tatu nyuma kabla ya kutokea kwa mlipuko huo.

Hii ni mara ya pili kutokea kwa mlipuko wa mabomu ambapo mlipuko kama huu ulitokea Aprili 29, 2009 katika kambi ya jeshi la Mbagala na ilisababisha vifo vya watu 26 na majeruhi kadhaa.


Hadi kufika jana jioni idadi ya vifo imeongezeka na kudaiwa kufikia 20










Ben Ali wa Tunisia 'taabani'




Bw Ben Ali
Aliyekuwa Rais wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali anaumwa sana na amelazwa katika hospitali ya Saudi Arabia.

Mtu wa karibu wa familia yake ameliambia shirika la habari la AFP, Bw Ben Ali, aliyeondolewa wakati wa ghasia zilizoibuka mwezi uliopita, amepata kiharusi.

Bw Ali mwenye umri wa miaka 74 alikimbilia Saudi Arabia na familia yake baada ya kuwepo maandamano makubwa kwa wiki kadhaa juu ya ukosefu wa ajira na umaskini.

Tunisia kwa sasa ina serikali ya mpito inayoiandaa nchi kwa uchaguzi mkuu.

Jamaa huyo, ambaye jina lake halikutajwa, alisema aliyekuwa Rais yupo "kwenye hali ya kuzimia" katika hospitali moja mjini Jeddah.

Alisema, "alipata kiharusi , na hali yake ni mbaya sana."

Gazeti la Tunisia liitwalo Le Quotidien pia liliripoti siku ya Alhamis kwamba Bw Ben Ali amepata kiharusi.

Wakati huo huo, chanzo cha Saudi Arabia kilichonukuliwa na shirika la habari la Reuters limesema Bw Ben Ali alikuwa "katika hali mbaya."

Awali, msemaji wa serikali ya mpito ya Tunisia amekataa kuthibitisha au kukubali taarifa zozote kuwa Ben Ali yuko hospitali.

Ghasia za Tunisia zilimaliza miaka 23 ya utawala wake.

Japokuwa alikuwa akisifiwa kwa kudhibiti hali ya kisiasa na kuimarisha uchumi, wakosoaji wanasema alikuwa haheshimu haki za binadamu na demokrasia- madai anayoyakanusha



UWANJWA wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere umefunguliwa na kuanza shughuli zake





UWANJWA wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere umefunguliwa na kuanza shughuli zake za usafirishaji abiria kama kawaida.
Juzi usiku uwamnja huo ulifungwa na kuzuia ndege zisitue katika uwanja huo kutokana na kutokea kwa mlipuko wa mabomu katika kambi ya Jeshi ya Gombolamboto.

Taarifa iliyotolewa leo asubuhi na mamlaka yausafiri wa anga ilisema kuwa uwanja huo umefunguliwa na kuanza kuruhusu kutua kwa ndege kama kawaida.

Juzi usiku majira ya saa 3 uwanja huo ulifungwa kutokana na kuanza kwa mabomu na baadhi ya vipande vya mabomu na mabomu kuonekana kuanguka katika uwanja huo

Hivyo kufuatia hali hiyo ndege zote zilikuwa zinatakwia ziwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro [KIA] na uwanja wa ndege wa Zanzibar

Jana zaidi ya abiria 200 waliokuwa wanatarajia kusafiri kwa ngege wamejikuta wakisitishwa safari zao baada ya kuzuiliwa kwa ndege kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Dar es Salaam, kutokana na mlipuko wa mabomu.

NIFAHAMISHE ilishuhudia abiria hao wakiwa wamezuiliwa kusafiri kutokana na kuzuiliwa kwa ngege zisifanye safari zake kutokana na kadhia hiyo







Watu kadhaa wauawa kwenye mlipuko Dar




Milipuko katika ghala la silaha nchini Tanzania
Hali ya taharuki imetanda mji wa Dar Es Salaam, nchini Tanzania, huku wakaazi wakiamka kuomboleza vifo vya zaidi ya watu kumi na zaidi ya wengine 60 kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea kwenye ghala la kuhifadhi silaha za kijeshi, lililo karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege.

Wakaazi wa eneo la Gongo la Mboto lililo karibu na ghala hilo wamekesha nje baada ya makaazi yao kubomoka kutokana na mtikisiko wa milipuko hiyo iliyodumu kwa saa kadhaa. Milipuko hiyo ilisikika kwa umbali wa zaidi ya kilomita ishirini kutoka kituo hicho cha kijeshi.

Inaarifiwa kuwa milipuko hiyo ilianza mwendo wa saa mbili usiku.

Msemaji mmoja wa jeshi amesema kuwa kuna watu wengi ambao wamepoteza maisha yao lakini idadi kamili haijajulikana.

Kamanda wa polisi jijini Dar-es-Salaam, Suleiman Kova, ametoa wito kwa raia wa mji kuwa huo watulivu huku maafisa wa ulinzi wakiendelea na mikakati ya kurejesha hali ya uthabiti.

Kova amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mlipuko huo ni ajali na wala sio shambulio la kigaidi.

Ni hii mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

mwaka wa 2009 zaidi ya watu ishirini waliuawa na wengine 300 kujerihiwa






Zaidi ya 15 wapoteza maisha Kutokana na Mabomu Dar




ZAIDI ya watu 13 wamepoteza maisha hadi jana kufikia majira ya saa 10 alfajiri, usiku kutokana na kuathirika kwa mabomu yaliyolipuka katika kambi hiyo.
Mbali na vifo hivyo majeruhi walioweza kupatikana hadi usiku huo walikuwa zaidi ya 200.

Watu watano waliokufa katika tukio hilo ni wale wa familia moja waishio Gongolamboto eneo la Mzambarauni ambapo nyumba hiyo iliangushwa na bomu lililofika katika nyumba hiyo.

Idadi hiyo ya vifo iliripotiwa katika hospitali ya Amana ambapo walikutwa maiti 13, Temeke maiti 2, na Muhimbili maiti 2.

NIFAHAMISHE ilifika hospitali ya Amana hapo majira ya alfajiri ya leo na kukuta umati wa watu wakifika hospitalini hapo kukagua miiili hiyo bada ya kupoteana na ndugu zao na marafiki.


Imefahamika bungeni leokwua idadi ya vifo na majeruhi hivyo inaweza ikaongezeka kwa kuwa bado jeshi lnjazidi kukusanyamajeruhi na miili iliyoanguka njiani wakati wakazi wakinusuru uhai wao





Tume ya uchaguzi Uganda yatoa maelekezo



Kampeni za uchaguzi mkuu wa Urais pamoja na wabunge nchini Uganda zilimalizika rasmi na sasa tume ya uchaguzi imetoa maelezo kuhusu uchaguzi wa kesho.


Mfanyakazi wa Tume ya uchaguzi Uganda




Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi kipindi cha kutafuta kura kwa wagombea Urais na ubunge kilikuwa kati ya tarehe 28 mwezi wa Oktoba mwaka 2010 hadi tarehe 16 mwezi wa Febuari mwaka huu wa 2011. Hivyo mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, Mhandisi Badru Kigunddu, akihutubia waandiahi habari wa ndani na nje,katika makao makuu ya tume hiyo ,ametoa ushauri kwa wagombea viti hivyo.

Asema kufuatia muda wa mwisho wa kampeni kumalizika,tume inawahimiza wagombea kusitisha mikutano yote ya hadhara pamoja na mikutano na waandishi habari yenye nia ya kutafuta kura kwa viti vya urais na ubunge.

Kuhusu matayarisho ya upigaji kura wa siku ya Ijumaa mkuu wa tume ya uchaguzi amesema tume yake imekamilisha usambazaji wa vifaa vitakavyo tumika katika wilaya zote 112.

Ameongeza kuwa vifaa hivyo vitasambazwa kutoka makao makuu ya wilaya hadi tarafa ndogo , ambapo wakuu wa vituo vya kupigia kura watavichukua mapema asubuhi. Pia amesema matayarisho yote yanayohitajika kuona kama vituo vyote vya kupigia kura nchini vipatavyo 23,968 vitakuwa na vifaa vya kutumiwa na kuanza kwa wakati. Ameongeza kuwa ni wale tu ambao waliandikishwa katika daftari la kupigia kura ndio pekee watakaokubaliwa.

Upigaji kura unaanza saa moja asubuhi na kumalizika saa kumi na moja jioni.






Mabomu yaridhima kwa mara nyingine-Dar



GHALA namba tano la Kuhifadhia mabomu katika kambi ya Jeshi La Wananchi Tanzania [JWTZ] Gombolamboto limelipuka na kuleta maafa kwa wakazi karibu na kambi hiyo.
Mabomu hayo yalianza jana kwenye mishale ya saa 2 usiku katika kambi hiyo.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo, Luteni Abrahaman shimo alisema ghala namba tano katika kambi hiyo ililipuka na kuleta athari hiyo.

Akizungumza na vituo vya redio na Televisheni vya Taifa, majria y a saa 3:30 usiku alisema, ghala hilo lilianza ghafla na kuleta mlipuko wa mabomu katika kambi hiyo.

Shimbo aliwataka wakazi waishio maeneo hayo waondoke mara moja maeneo hayo kwa kuwa mabomu hayo yalikuwa na uwezo wa kuruka zaidi ya mita 10 alibainisha.

Katika tukio hilo wakazi wa karibu na maeneo hayo walionekana kuhaha huku na huko kukimbia kunusuru maisha yao na wengine kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.

Katika harakati za kukimia wengi walijeruhiwa na wengine wakianguka kwa hofuna hjuku wengine wakiacha watoto wao na kukimbia na kuacha watoto wao wakihaha na kulia kwa kuachwa.

Hadi kufikia leo asubuhi majria ya saa 2, shimbo amesema chanzo cha kutokea kwa mabomu hayo badohaijafahamika ila jeshilikokatika harakati za kuendelea kusaka majeruhi na kuendelea kutafuta chanzo hicho



Baadhi ya wakazi walala Uwanja wa Taifa


MARA baada ya kuanza kwa mlipuko wa mabomu hayo majira ya saa mbili usiku gari za Polisi zilikuwa zikipita barabarani kutangaza wakazi waishio Gongolamboto na Vitongoji vyake wasirudi maeneno hayo kutokana na mabomu yaliyokuwa yakiendelea kulipuka.

Pia magari hayo yalikuwa yakiamrisha usafiri wa mabasi ya abiria [daladala] yasifanye safari zake kuelekea huko kutokana na athari watakayoipata kuelekea maeneo hayo.

Hivyo magari hayo yalikuwa yakiwataka wananchi kuelekea Uwanja wa Taifa kwa ajili ya malazi ya usiku wa kuamkia leo.

Hivyo wananchi kwa makundi walionekana kuelekea uwanjani huko kutokana na damri hiyo y a serikali iliyowataka kuelekeka huko na kuahirisha kurudi majumbani mwao.

Hata hivyo baadhdi ya wananchi wameonekana wakiwa pembezoni mwa barabara na wengine wakiwa wamechukua uamuzi wa kulala barabarani kutokana na kukosa uwezekano wa kuelekea maeneno hayo na kusitishwa kwa usafiri kuelekea maeneno hayo.








MARA baada ya kuanza kwa mlipuko wa mabomu hayo majira ya saa mbili usiku gari za Polisi zilikuwa zikipita barabarani kutangaza wakazi waishio Gongolamboto na Vitongoji vyake wasirudi maeneno hayo kutokana na mabomu yaliyokuwa yakiendelea kulipuka.

Pia magari hayo yalikuwa yakiamrisha usafiri wa mabasi ya abiria [daladala] yasifanye safari zake kuelekea huko kutokana na athari watakayoipata kuelekea maeneo hayo.

Hivyo magari hayo yalikuwa yakiwataka wananchi kuelekea Uwanja wa Taifa kwa ajili ya malazi ya usiku wa kuamkia leo.

Hivyo wananchi kwa makundi walionekana kuelekea uwanjani huko kutokana na damri hiyo y a serikali iliyowataka kuelekeka huko na kuahirisha kurudi majumbani mwao.

Hata hivyo baadhdi ya wananchi wameonekana wakiwa pembezoni mwa barabara na wengine wakiwa wamechukua uamuzi wa kulala barabarani kutokana na kukosa uwezekano wa kuelekea maeneno hayo na kusitishwa kwa usafiri kuelekea maeneno hayo.

NIFAHAMISHE ilishuhudia makundi ya watu maeneo ya Kariakoo, barabara ya Nyerere wakiwa katika mkusanyiko na kuweka kambi maeneno hayo baada ya kusikitishwa kwa usafiri wa kuelekea maeneo hayo.

Taarifa iliyotolewa asubuhi hii kutoka Bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema zaidi ya watu 4000 walipokea katika uwanja huo na wanaendelea kuwahifadhi uwanjani hapo






Wito wa 'siku ya ghadhabu' Libya




Watolewa na wanaharakati kupitia mitandao ya kijamii


Wanaharakati wanaopinga serikali nchini Libya wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kupata watu wa kuwaunga mkono kwenye maandamano ambapo wanaelezea kama "siku ya ghadhabu."

Kulikuwa na ripoti za mapigano katika miji miwili siku ya Jumatano, huku takriban watu wanne wakiripotiwa kufariki dunia katika mji wa al-Bayda mashariki mwa nchi hiyo.

Idadi kubwa ya watu walijeruhiwa katika maandamano yaliyo na vurugu siku ya Jumanne usiku katika mji wa Benghazi.

Ghasia hizo zimeibuka baada ya mkosoaji wa serikali kutiwa kizuizini.

Maandamano ya kuunga mkono demokrasia hivi karibuni yameenea katika mataifa ya kiarabu, huku marais wa Tunisia na Misri walipolazimika kujiuzulu kutokana na ghasia hizo.

Lakini maandamano ya wiki hii ni mara ya kwanza kuonyesha ujasiri wa kweli nchini Libya, nchi ambayo kupingwa hakustahamiliwi.








Jeshi latoa tahadhari kwa wananchi



WAZIRI wa Ulinzi, Dokta Hussein Mwinyi aliwataka wakazi wa Gongolamboto na vitongoji vyake kuwa makini na kuwataka wasiokote vyuma na wasisogee karibu na maeneo kwa kuwa mabomu yanaendela kuruka na vipande kuonekana kuzagaa katika maeneo mengi.
Akizungumza majira ya saa 5:23 za usiku jana, Mwinyi alisema chanzo cha kutokea mlipuko huo bado hakijajulikana na hadi kufika leo asubuhi bado chanzo hicho bado hakijajulikana.

Hivyo aliomba kwa wananchi na kuwataka wawe na subira katika kipindi hiki kigumu na kuwataka wakazi wafate maelekezo yanayotolewa na serikali na wasikiuke maelekezo hayo.

“Wakazis wasiokote vyuma, wala wakikuta bomu linazagaa katika nyumba zao” utaratibu wa kuokota vipande vilivyoruka vitafanywa na jeshi lenyewe” alisisitiza









Watoto wengi wapotea waonekana mitaani wakiwa hawana muelekeo



MAKUNDI ya watoto wameonekana asubuhi hii wakiwa hawana muelekeo baada ya kupoteana na wazazi wao katika harakati za kunusuru uhai wao kwa kuhofia kuuawa kwa mabomu.
Zaidi ya watoto 50 wameonekana eneo la Ubungo asubuhi hii, maeneo mengine ambapo watoto hao wanaonekana ni maeneo ya Ilala, Buguruni, Tazara na Kigogo ambao wameonekana kuchoka na wengine wakiwa wamelala pembezoni mwa barabara kutokana na uchovu waliopata kwa kukimbia jana usiku.

Hata hivyo wananchi wametakiwa wakiona makundi ya watoto wanaozagaa mitaani waliokosa muelekeo wawakusanye kwa pamoja watoto hao ili waweze kupelekwa katika maeneo ya wazi ukiwemo uwanja wa Uhuru, Karume ili wazazi waliopotelewa na watoto wao wafike maeneo hayo wawakague.

Wakazi walioathirika zaidi kutokana na kukibmia huko na huko ni wale waishio maeneno ya Gongolamboto, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kinyertezi, Kitunda, Yombo, Ulongoni na maeneno mengine karibu na kambi hiyo





Polisi wakabiliana na waandamanaji Bahhrain




Waandamanaji nchini Bahrain

Maafisa wa usalama katika Himaya ya Bahrain wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga Serikali ambao wamepiga kambi katika bustani kati kati mwa mji mkuu wa Manama.

Walioshuhudia maandamano hayo wanasema polisi waliwasili wakati waandamanaji walikuwa wakijiandaa kulala.

Makundi ya upinzani yanasema kuwa watu wawili walifariki na wengine wengi kujeruhiwa.

Wanasema polisi waliwasili mahala hapo na kuanza kuwarushia mabomu ya kutoa machozi na wakati huo huo kufyatua risasi za mipira; jambo lililowafanya watu kukimbilia mitaa iliyo karibu.

Jana maelfu ya waandamanaji walishiriki kwenye maandamano ya kupinga serikali kwa siku ya tatu mfululizo katika mji mkuu wa Manama.









Bunge laahirishwa asubuhi hii


BUNGE la Jamuhuri la Muungano wa Tanzania, limeahirisha kuendesha shughuli zake asubuhi hiii kutokana taharuki iliyoikumba nchi na kupisha kamati husika kushughuilikia maafa hayo.
Spika wa Bunge , bi, Anna alitangaza kuahidiriha bunge hilo mara baada ya kuongea kwa Waziri Mkuu Mizengo panda kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika tukio hilo.

Hivyo kutokana na taharuki hiyo, spika ametangaza kuahirisha bunge hilo hadi kesho asubuhi ili kupisha wabunge waliochaguliwa kwenye kamati kushughulika na janga hilo lililoikumba taifa.




Waziri Habineza wa Rwanda ajiuzulu




Joseph Habineza
Waziri wa michezo na utamaduni nchini Rwanda Joseph Habineza amejiuzulu.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kujiuzulu kwake lakini hatua hiyo imefanyika siku chache tu baada ya kuhusishwa katika kashfa ya ngono.

Vyombo vya habari nchini humo vilisambaza picha kadhaa alizopigwa akiwa na wasichana kadhaa wakistarehe kwenye nyumba moja mjini Kigali.

Rais Kagame aridhia
Kutoka Kigali mwandishi wetu Yves Bucyana ametuma taarifa ifuatayo.

Taarifa ya kujiuzulu huko kumetolewa na ofisi ya waziri mkuu ambapo ilisemwa kwamba waziri huyo wa utamaduni na michezo Joseph Habineza amejiuzulu na Rais wa Jamuhuri ameridhia hatua hiyo.

Mwandishi wetu wa Kigali Yves Bucyana alisema kwamba Bw Habineza amekuwa akiandamwa na vyombo vya habari kwa kusambaza picha zake za siri alizopigwa akiwa pamoja na wasichana watano.

Waziri huyo pamoja na mabinti hao walikuwa katika hali ya starehe kwenye nyumba moja mjini Kigali.

Kitendo hicho kilitangazwa na vyombo vya habari kama kashfa kwani alikuwa na mabinti hao huku akiwa ni mume wa mtu na pia ikizingatiwa kuwa yeye ni waziri ambaye pia ana majukumu ya kulinda utamaduni wa Wanyarwanda.

Lakini akizungumza na waandishi wa habari Bwana Habineza amepinga namna watu walivyotafsiri picha hizo anazosema ni za zamani.

"Mimi sikuwa na kosa lolote la kujishtaki. Sikuwa na hatia yoyote ila namna watu wanavyozungumzia sakata lenyewe, jinsi wanavyotafsir zile picha na kujaribu kuitia chumvi hiyo wanaoita kashfa. Hiyo ndiyo iliyonifanya kujiuzulu."

Kwa miaka sita aliyotumikia wizara hiyo, pamoja na kuonekana kuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame pia alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa na kuwavutia vijana

No comments:

Post a Comment