KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, February 16, 2011
Homa ya uchaguzi mkuu Uganda yapanda
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais wa sasa wa Uganda, Yoweri Museveni Uchaguzi mkuu nchini Uganda utafanyika kesho Ijumaa. Uchaguzi huo wa Rais na Bunge unafuatia ule wa 2006 ambapo kwa upande wa urais kama ilivyokua 2001, mshindi alikuwa rais wa sasa, Yoweri Museveni.
Hata hivyo, watazamaji wa nje na ndani wakisema kulikua na mizengwe na udanganyifu. Kwa mara nyengine mpinzani mkuu wa Museveni ni Dr Kizza Besigye aliyeteuliwa na Ushirika wa vyama vinne vya kisiasa vya upinzani. Uchaguzi huo utafanyika wakati ambapo Uganda inaweka matumaini ya kuimarisha uchumi wake kutokana na kupatikana kwa mafuta katika ziwa Albert na utulivu baada ya uchaguzi ni zingatio kubwa la wawekezaji .
Kampuni ya mafuta yenye makao yake makuu nchini Uingereza Tullow Oil ni mtafutaji mkubwa wa mafuta nchini Uganda na inasema licha ya mgogoro kuhusu ulipaji kodi na serikali, itaanza kuchimba mafuta na gesi mwaka ujao 2012.
Mafuta yamegeuka sehemu ya kampeni ya Uchaguzi. mgombea mmoja wa upinzani Bbiira Kiwanuka akigusia juu ya rushwa anasema biashara ya mafuta ni biashara muhimu kwa Museveni na familia yake. Rushwa ni jambo la wasi wasi kwa makampuni ya mafuta na lilitawala katika kampeni.
Wagombea wa upinzani wanadai kama makampuni husika hayatazingatia maendeleo ya watu wa maeneo hayo ya mafuta basi wataachana nayo. Mji wa Bulisa ulioko katika eneo ambalo sehemu kubwa ni ya kilimo, haujabadilika sana, tangu miaka mitano iliopita yalipogunduliwa mafuta. Ni jengo la kampuni ya mafuta Tullow oil Uganda pekee linaloonekana ku´ngara kuliko mengine.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Mmoja wa wagombea urais wa Uganda, Kizza Besigye
Mgombea wa chama tawala National Resistance Ernest Kiize anasema ugunduzi wa utajiri mpya wa mafuta utakua wa manufaa kwa kila mtu. Yeye anasema licha ya kuzungumziwa rushwa , lakini serikali na polisi wanafanya kila jitihada kupambana nayo.
Malalamiko mengine ya wapinzani ni kuwa chama tawala NRM kinatumia fedha na vitisho dhidi ya wapiga kura maeneo ya wakaazi masikini vijijini.
Ingawa wachambuzi wanaseama ushindani katika uchaguzi wa rais utakua mkali kati ya Museveni na Besigye lakini wanatarajia Museveni kushinda. Lakini Besigye aliyeshindwa mara mbili chaguzi zilizopita amewatia hofu wawekezaji wa kigeni na wafadhili kwa kutamka kwamba atakua na tarakimu zake mwenyewe za uchaguzi huo na kuonya wafuasi wake watasababisha machafuko pindi ikifanywa mizengwe. Anadai aliibiwa kura 2006. Mahakama ilikiri kulikuweko na dosari 2001 na 2006 lakini ikasisitiza kwamba wizi huo wa kura haukuathiri matokeo na kuwa mshindi bado alikua ni Museveni.
Wengi wanasema ni hali ya usalama na utengamano itakayowafanya kumchagua Museveni ambaye ameshatawala kwa miaka 25. Baada ya uhuru 1962, Uganda ikaingia katika kipindi cha vurugu na machafuko kwa kuanzia na utawala wa kimabavu wa Idi Amin baada ya kumpindua Milton Obote na kufuatiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na watawaa wengine wa kijeshi.
Museveni binafsi alitwaa madaraka baada ya miaka mitano ya vita vya msituni. Mama mmoja alisikika akisema, "sasa tunaweza kutembea bila ya hofu. Wengine waliua watu hasa Idi Amin. Museveni hakuuwa mtu, kwanini basi kumjaribu rais mwengine ambaye pengine atafanya kinyume na hayo ? Aliuliza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment