KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 19, 2011

Afa kwa kushambuliwa na paka


MWANAMKE Modesta Bungala [45] mkazi wa kitongoji cha Mshikamano, Shinyanga amefariki dunia kwa kushambuliwa, kung’atwa na paka aliyehisiwa kuwa na kichaa.
Mwanamke huyo alikutwa na dhoruba hiyo Februari 16, mwaka huu, wakati alipokuwa akipita katika nyumba ya jirani yake na paka huyo kumvamia na kuanza kumnga’ata.

Marehemu Modesta alikuwa akipita kwa jirani yake wakati alipokuwa akitoka kuchota maji na alipofika katika nyumba hiyo alimkuta paka huyo na alimrukia na kuanza kumng’ata.

Alijaribu kumfukuza paka huyo lakini haikuwezekana na paka huyo aliongeza mashambulizi ya kumng’ata katika sehemu mbalimbali za mwili na alianza kupiga kelele na mayowe ya kuomba msaada kwa majirani wengine.

Hata hivyo aliweza kujeruhiwa vibaya na paka huyo na alipoteza maisha muda mfupi baadae

No comments:

Post a Comment