KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Zambia Magharibi nao wanataka kujitengaRais Rupia Banda wa Zambia

Polisi magharibi mwa Zambia wamepambana na waandamanaji wanaotaka eneo hilo la magharibi kujitenga na kujitawala wenyewe.

Watu wawili wameuwawa katika ghasia hizo mmoja wao akiwa mwandamanaji aliyepigwa risasi na polisi alipokuwa akijaribu kukiteketeza kwa moto kituo cha mafuta, na wa pili ni mtoto aliyeingia katika mkumbo wa waandamanaji.

Idadi ya majeruhi haijulikani, lakini takriban watu 120 wamewekwa kizuizini.

Waziri wa mambo ya ndani wa Zambia, Mkhondo Lungu, amesema serikali itafanya kila juhudi kudumisha amani baada ya ghasia zilizotokea jana.

Polisi wanasema wamemkamata Maxwell Mututwa, ambaye ni kiongozi wa kundi la Black Bull, linaloshutumiwa na serikali kwa kuchagiza kujitenga kwa Zambia magharibi.

No comments:

Post a Comment