KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Watunisia waendelea kuipinga serikali



Wanajeshi wakisimama karibu na tangi, Tunisia


Maandamano mapya yameibuka katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, saa chache kabla ya tangazo rasmi la kutajwa serikali mpya ya kitaifa kutolewa.

Polisi wametumia mizinga ya maji kuwatawanya waandamanaji wakitoa wito wa chama cha Rais Zine al-Abidine Ben Ali aliyefukuzwa nchini kuachia madaraka.

Nchi hiyo imekuwa katika hali ya tahadhari tangu alipokimbia siku ya Ijumaa.

Waziri mkuu Mohammed Ghannouchi alisema makubaliano baina ya vyama vya siasa yatatolewa baadae.

Bw Ben Ali, ambaye alikuwa madarakani kwa miaka 23, alikimbilia Saudi Arabia siku ya Ijumaa baada ya kuwepo maandamano makubwa nchini kote ya kupinga ukosefu wa ajira, ongezeko la bei ya vyakula na rushwa.

No comments:

Post a Comment